Habdavi
JF-Expert Member
- Mar 5, 2011
- 788
- 804
19. Je, mbegu bado ziko ghalani? Akimaanisha msimu wa kuvuna ulikuwa bado, na mazao ya nafaka ya msimu uliopita yamekwisha. Mbegu za nafaka tayari zimepandwa mwezi huu, na hakuna dalili zaidi za kuzaa kwake mazao mazuri;sehemu nyingine, walipoasi, Mungu alitumia miti hii hii ya matunda kama mfano kuonyesha, alivyowafunguia milango ya Baraka na mafanikio katika mambo yao maovu, soma.
Hagai 1:18 “Tafakarini, nawaomba; tangu siku hii ya leo na siku zijazo; tangu siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kenda, naam, tangu siku hiyo ulipowekwa msingi wa hekalu la Bwana tafakarini haya.
19 Je! Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki”.
Mwaka huo kulikuwa na ukame hivyo dalili za kuvuna mazao mazuri ni hafifu sana. Lakini ninawaahidi kutoka siku hii (kwa kusisitiza kwa kurudia uhusiano wa baraka na siku ya utii wao) baraka katika mavuno mengi. Vivyo hivyo mzabibu, mizeituni pamoja na mikokomanga ambayo hapo awali ilizaa kidogo au haikuzaa chochote, itabarikiwa kwa kuzaa sana
Hata leo hii, unaweza ukaona hakuna dalili za kuvuna Baraka ulizoahidiwa; lakini bado unapaswa kumtegemea Mungu.