Umekula tunda gani leo?

Mlo wangu wa kila siku jioni saa 2 ni matunda. Tikiti, parachichi, nanasi, maembe, papai. Nikila hii mchanganyiko huo situmbukizi kitu kingine mpaka kesho. Nakula sana mpaka kushiba
 
Pilipili nalo tunda!?
 
Hapana pilipili sio tunda
Sehemu nyingine ni ngumu kupata matunda ya asili, inakuwa ngumu sana kula matunda lakini kwa wale wenzetu na mie tuliokulia maeneo kama Mbeya, Kilimanjaro, Kagera, Ruvuma, Arusha, nk matunda tunakula kama mgonjwa na daktari.
 
Dar sahani full matunda buku kwa nini umalize wiki hujala matunda wakati yapo pia Hadi ya 200?
Mikoani sawa
 
Kipindi cha nyuma nilikuwa naona wanaokula apple kama watu wanaopenda ufahari, kumbe apple linaondoa sumu kwenye ini, nilikuwa naangalia videos za faida za matunda YouTube nikajua apple lina faida kubwa sana.

Alafu kuna matunda yameadimika mf Stafeli, Mzaituni siyaoni, mimi nilipokulia yalikuwa kibao, watu wamejenga na miti yenyewe wakaikata.
 
Wengi hawajui umuhimu wa matunda mwilini kiafya matokeo yake ndio hayo
 
Mi nimekuja tunda lile TUNDA LA KIMASIHARA.

#YNWA
 
Sijui ni mazoea au la ila ni mara chache sana kula chakula bila matunda hasa ndizi, na kingine napenda sana miwa na juisi yake sa sijui nayo ipo kwenye category ya matunda au la

Kingine pia nilianza kupenda matikiti ila baada ya kusikia hekaya za baadhi ya matikiti kama sio yote (huko mashambani) kudungwa sindano ili yasifanye nini sijui..., nikapoteza interest nayo kabisa.

Kilichobaki ni kuongeza idadi ya matunda ili kuondoa domination ya ndizi mbivu pekee, hivyo nina mpango wa kujikita zaidi kwenye machungwa, matango, parachichi, nanasi, papai na maembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…