Umekula tunda gani leo?

Umekula tunda gani leo?

Hapana my dear ukishalimenya na kulikatakata nanasi lako vile vipande vitie kwenye chombo chenye maji kiasi na chumvi kiasi ...acha kwa dakika kadhaa kisha anza kula , ukichukua toka chomboni..the flavor is amazing
Ok so meno hayatauma kabisa?! Napenda nanasi ila tatizo meno ntajaribu hii njia, ila sasa ile the real taste haitokua diluted na hayo maji+chumvi? Just thinking 🤔
 
Ndizi mbivu mbili .
Ni desturi... Naamka saa kumi na moja...
nakula ndizi mbivu mbili...Nafanya mazoezi...
30minutes.. naoga
Nameditate 30mins
Nasoma 1hr.
Napata breakfast.
[emoji1548][emoji1548][emoji1548]
 
Kwa hakika kama kuna mtu kati yetu asubuhi ya leo kala tunda lolote lile basi ni wale waliolala zile hotel zenye bed n breakfast full course. Wengine wetu kwa uchache mno ni wale wafanya diet na kwa uchache zaidi wale wanaotambua umuhimu wa matunda mwilini kiafya. Wengi wetu humaliza mpaka wiki bila kula hata kipande kimoja cha tunda lolote.

Wengi huwa hawali matunda mpaka waandikiwe na daktari kama sehemu ya tiba. Kwao kula tunda ni sehemu ya anasa na kupoteza pesa..

Matunda yana faida kubwa mwilini kiafya kuliko hata nyama. Matunda ni sehemu muhimu ya tiba. Matunda yana uwezo wa kukujenga kiafya na kukukinga na maradhi mengi. Ni afadhali mara mia ukala matunda ya buku kuliko kula mchemsho wa buku 2, Matunda ni tiba ya magonjwa mbalimbali.

Matunda ni sehemu muhimu ya tiba mbadala na ujenzi wa mwili imara na wenye nguvu.
Baadhi yetu hupendelea shurubati zaidi kuliko matunda yenyewe. Ni sawa pia lakini shurubati isiyo halisi inakuwa imechanganywa na vionjo vingine hivyo kupunguza kwa kiasi fulani nguvu ya kutenda.

Huu ni ushauri wangu kwako pamoja na kunywa maji mengi na kupangilia milo yako lakini usisahau kitu hiki muhimu sana TUNDA. Jitahidi kupata kipande cha tunda kwenye kila mlo wako.. kuna siku utanikumbuka na kunishukuru kimoyomoyo
Je, umekula tunda gani leo?

Asante mkuu kwa kutuhamasisha,, ila chakuongezea hapo tunda linaliwa kabla ya kupiga menu kubwa. Maana ukila baada ya msosi kuna enzymes zinakuwa zimeshaachiwa ambazo kuzuia uyeyushaji wa vitamin C. Kwa hiyo unaweza kukosa hiyo vitamin ya muhimu kabisa inayopatikana kwenye matunda. Kwa hiyo basi tupige tunda angalau nusu saa kabla ya kupiga menu!
 
Back
Top Bottom