Umekutwa na hatia bado unaingia na bangi kituoni uunao ni usela au..?

Koloko

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2026
Posts
285
Reaction score
531
Katika purukushani za maisha huku na kule, kuna kipindi nilishawahi kukamatwa na kuwekwa ndani

Kesi yangu ilikuwa bado inaendelea, lakini ndani ya moyo wangu nilikuwa naamini kwamba, kwa namna yoyote ile, ipo siku nitatoka. Changamoto kubwa ilikuwa hata kuwafikishia wazazi taarifa kwamba nilikuwa ndani.

Mungu alisaidia, taarifa ikawafikia mzazi wangu. Nilifanikiwa kuongea naye na kumweleza kwamba niko ndani. Baada ya hapo, akafanya kila alichoweza kunisaidia, na hatimaye nikaja kutoka.

Lakini kipindi nilichokaa ndani kilinifundisha mambo mengi sana.

Nilikutana na watu wa aina tofauti. Kila mmoja alikuwa na pressure yake, historia yake na sababu zake za kuwa pale. Wengine walikuwa bado na matumaini makubwa ya kutoka, lakini wengine walionekana tayari wamekubali kwamba mwisho wao ulikuwa kwenda jela.

Lakini kuna kijana mmoja ambaye mpaka leo nikikumbuka nabaki na maswali mengi.

Alikuwa kijana mdogo wa makamo (18+), alikuwa mjanja sana. Katika vitu vya kijinga.

Kitu kilichonishangaza ni kwamba, licha ya kuwa tayari alikuwa ndani, bado alikuwa anaendelea kufanya mambo ambayo yangeweza kumuongezea matatizo.

Lakini huyu kijana alikuwa na mbinu zake za kuficha baadhi ya vitu. Alikuwa ameingiza vitu ambavyo sikutarajia kabisa mtu angeweza kuvificha ndani ya mazingira yale. Aliingia na bangi.

Kulikuwa na chupa za maji yakuunywa ambayo huwa watu wanaleta pamoja na chakula, chakula huwa tuna tia kwenye sehemu moja kwa kuchanganya na vya wengine walivyo letewa ili kusubiri mda wakula saa 18 jioni

Wakati huo zile chupa ambazo huwa zinakuja na maji wale jamaa walikuwa wana chukua wanajaza maji nusu alafu wanavutia mule ili moshi usisambae kituoni.. alooh

Kituoni kulikuwa na utaratibu wa kukagua kila mtu kabla ya kuingia. Vitu vya chuma na vitu vingine vilivyoweza kugundulika vilitolewa.

Nilipogundua hilo nilishangaa sana.

Nilijiuliza:

“Huyu kijana mama ake anapambana kumtoa nje, lakini mtoto still bado anaendelea kufanya mambo yanayoweza kumuongezea kesi sisi wengine atujui hatima yetu mpka sasa..?

Nilikuwa namuangalia tu na kushindwa kuelewa.

Kijana huyu alikuwa bado mdogo, lakini maisha aliyokuwa anaishi yalikuwa yamenishangaza sana.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba yeye alitoka kabla yangu.

Licha ya yale yote niliyomuona akifanya ndani, siku yake ya kutoka ilifika kabla yangu.

Hapo ndipo nilipojifunza kwamba maisha ya mtu huwezi kuyaelewa kwa kumuangalia kwa nje tu.

Kila mtu ndani alikuwa na story yake. Kila mtu alikuwa na pressure yake. Kila mtu alikuwa anapambana kwa namna yake.

Na mimi nilipotoka, nilibeba somo moja kubwa:

Usimhukumu mtu kwa kile unachokiona tu. Huenda nyuma ya tabia yake kuna story ambayo huijui.

Sasa nataka kuuliza wakuu:

👉 Umewahi kukutana na mtu ambaye mazingira yake, tabia yake au namna alivyokuwa akiishi ilikushangaza kiasi cha kushindwa kuelewa anawezaje kuishi hivyo?

Au kama umewahi kupitia mazingira ya kituo cha polisi, rumande au sehemu nyingine yenye mazingira magumu, ni tukio gani ulilokutana nalo ambalo huwezi kulisahau mpaka leo?
 
Wew ulipelekwa kwa kesi gani...
 
Umewahi kukutana na mtu ambaye mazingira yake, tabia yake au namna alivyokuwa akiishi ilikushangaza kiasi cha kushindwa kuelewa anawezaje kuishi hivyo?

Kisa kiko Tofauti kidogo.

Shuleni kuna Jamaa alikuwa mtundu, ameanza kuvuta Bangi toka form 2. Darasan anaingia , ila muda wa prepo usiku kuanzia saa 2 had saa 4. Haudhurii.
Kumkuta anasoma Vitabu au daftar nje ya muda wa kawaida wa darasa ni nadra. Labda discusion.

Ajabu Alikuwa anashika 3 bora. Na form 4 alipiga div 1.17..
Kaenda PCB, kapiga Div 1.8 , alaf Kaenda MuHas.
Na Sasahivi ni Dokta Amana.

Ukimuiga huyu. Unapotea.
Yuko Gifted
 
Nikweli mkuu awa watu wana staajabisha sana aisee mmi nilishuhudia jamaa aliondoka na kuniacha selo aisee kweli wapo gifted 😅
 
Tulikuwa tunaishi kijijni, bwenini darasani kuonekana nadra labda matukio muhimu suspension za kutosha nyingine mwezi tu kabla ya necta cha ajabu nkatoka division 1.08 wakina John visomo wengi walitaga mwamba yuleee wakasema eti mm mchawi.. Hata wazee wangu hawakuamini maana sio Kwa kesi walizokua wanaletewa
 
Back
Top Bottom