Umeme bado ni kizungumkuti licha ya mito na mabwawa kujaa maji

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Serikali ilitamka kuwa upungufu wa umeme umetokana na ukame lakini sasa hivi mabwawa na mito imejaa kutokana na mvua kuendelea kunyesha.

Pamoja na sababu hiyo kuna maeneo hapa Mwanza tangu asubuhi hakuna umeme. Hivi tunaishi nchi gani hii kila siku ni porojo tu?
 
Mi Niko gizani dasilamu huko vijijini Hali ikoje?

Bora kuhamia Burundi!
 
Tanzania Mgao Ni Endelevu Sana Mpaka Tuhakikishe
Maji Yanaitwa Mmmaa
 
Waziri mwenye dhamana tunaomba ufanye kazi na Tanesco Dar. Sisi wananchi wachini tunashinda gizani kwa masaa 24. Leo wamekata umeme saa nne asubuhi na wamerudisha saa 12 jion ndani ya nusu saa wakakata tena hadi sasa hakuna umeme wala taarifa zozote. Hatukatai umeme kukatwa ila basi tuzingatie utu huwezi kukata umeme mara mbili na joto hili la Dar.
 
Kimara hapo mtakuwa na shida zenu tu. Umeme haujakatwa kwa wiki ya pili Sasa. Lkn Kimara kila tatizo linakuja kwenu tu;
1 . Kubomolewa nyumba ili kupanua barabara ....Kimara.
2. Lori kugonga maduka .....Kimara.
3. Kukatika kwa umeme ...Kkmara
 
Waziri mwenye dhamana tunaomba ufanye kazi na Tanesco Dar. Sisi wananchi wachini tunashinda gizani kwa masaa 24. Leo wamekata umeme saa nne asubuhi na wamerudisha saa 12 jion ndani ya nusu saa wakakata tena hadi sasa hakuna umeme wala taarifa zozote. Hatukatai umeme kukatwa ila basi tuzingatie utu huwezi kukata umeme mara mbili na joto hili la Dar.
Hili ttz litaisha hadi pale mkiambiwa muandamane kuipinga CCM mkakubali wito.
 
Mwalimu Nyerere alisema tuna maadui watatu wa kuweza kupambana nao:
1. Umaskini
2. Ujinga
3. Maradhi
Kwa sasa Kuna adui wa nne ameongezeka (tena adui wa kutengenezwa na binadamu). [emoji116]
4. Umeme usiokuwa wa uhakika. Umeme Tanzania umeshakuwa kero (Wagosi Wakaya, 2001)
 
Si walitoa kipindi cha miezi 6 ,mambo ya maintenance ...muda si bado au

Ova
 
Waziri mwenye dhamana tunaomba ufanye kazi na Tanesco Dar. Sisi wananchi wachini tunashinda gizani kwa masaa 24. Leo wamekata umeme saa nne asubuhi na wamerudisha saa 12 jion ndani ya nusu saa wakakata tena hadi sasa hakuna umeme wala taarifa zozote. Hatukatai umeme kukatwa ila basi tuzingatie utu huwezi kukata umeme mara mbili na joto hili la Dar.
Mkiambiwa tokeni nje mdai haki zenu mnakimbilia ndani na maneno kibao, sasa kaeni humohumo na joto lenu.Siku zote mabadiriko makuu ya nchi yoyote yale uanzia kwenye miji mikuu lkn nyie sijui aliyewaroga nani, ubinafsi tuu unawasumbua.
 
Huenda ni mchezo wa Wafanyabiashara wa Vifaa vya Solar na Majenerata kutaka bidhaa zao ziuzike!
 
Uliwaamini wana siasa. Mvua ikiwa haijanyeesha wanasema bwawa limekauka, ikinyeesha wanasema maji yamezidi. na umeme haupo.
 
Waziri mwenye dhamana tunaomba ufanye kazi na Tanesco Dar. Sisi wananchi wachini tunashinda gizani kwa masaa 24. Leo wamekata umeme saa nne asubuhi na wamerudisha saa 12 jion ndani ya nusu saa wakakata tena hadi sasa hakuna umeme wala taarifa zozote. Hatukatai umeme kukatwa ila basi tuzingatie utu huwezi kukata umeme mara mbili na joto hili la Dar.
Kuwa wa juu.
 
Tatizo sio maji kama shida ni maji huo unao takiwa kuuzwa nje utatoka wapi.
Tuliambiwa wa gesi mgao upo palepale.
Wa bwawa kubwa hali ni ileile
Inabidi tuwazoee tu ukiwaka sawa Usipowaka haya!
 
Back
Top Bottom