Ni kwamba, kipindi hicho ambacho Tanzania ilianza kutumia umeme ilikuwa inatawaliwa na Wajerumani.
Mapinduzi ya viwanda yalitokea tangu karne ya 17 huko Ulaya hivyo mambo kama umeme yalikuwa ni kitu cha kawaida kwa wazungu!
Pia, baadhi ya Wazungu walipohamia Afrika katika karne ya 18 wengine waliamua kuyafanya makoloni kama makazi ya kudumu hivyo walianza kuweka miundombinu na teknolojia mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha maisha yao.
Baada ya wazungu kuondoka Afrika, nchi nyingi za Kiafrika zilishindwa na zinaendelea kushindwa kuendeleza vile vitu walivyoacha Wazungu.
Zipi ni sababu za nchi za Kiafrija kushindwa kuendeleza mazuri yaliyoachwa na Wazungu mimi na wewe ndio tuulizane, mana kwa sasa bongo kama unavyooan tuna watu kama kina Mwijaku, Doto Magari, na yule binti wa Aslay sijui Lilian wanatrend mtandaoni na Watanzania wanapenda kuwafuatilia, lakini mambo sirias hayafuatiliwi.