Umeme unakatwa saa sita usiku, hadi saa 12 jioni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Hamna mbinu zozote za kupunguza makali ya mgao wa umeme. Umeme umekuwa ukikatwa saa sita usiku na kuwashwa saa 12 jioni.

January Makamba na naibu wake wamelidanganya bunge, waliahidi kuchepusha gesi asili kutoka kwenye njia ya mwekezaji na kuingiza kwenye njia ya TPDC, lakini hadi sasa maumivu ya mgao ni makali sana.
 
Hii Nchi ina matatizo. Umeme mgawo, Maji mgawo! Tufaika kwelli??
 
Wanadanganya mpaka bunge!! Mama Samia mpaka sasa hajui kuwa wanamdanganya nae pia?
 
Kama nakuona vile ulivyoshika mshumaa.😂😂😂
 
Siku moja niliwahi kutukana sana hii wizara humu jamvini, kukawa na utetezi mwingi nikashangaa!

Ndipo nilipojua kwamba kipindi hiki waTz tumegawanyika pakubwa kimsimamo!

Majibu ya uongo wa wazi ya NW jana na mgao wa umeme unaozidi kuendelea nchini pamoja na makofi ya rejareja ya Wabunge ya kupiga meza yalinifadhaisha sana kwa kweli!

Hivi hili genge la watawala, wanatuchukuliaje sisi waTz?

Kadri ninavyozidi kuandika, ndiyo hasira inavyozidi tu kunipanda.

Ngoja niishie hapa kwanza!
 
Alisema mwendazake. Kumpa mwekezaji mradi wa umeme ni kuliua taifa. Sikiliza mkataba wa kuchepusha gesi ya mwekezaji utakalivyolitafuna taifa.
 
Mwendazake aliua taifa
Aliuaje wakati huduma zote zilitolewa kwa viwango vya juu kuliko sasa. Ulimsikia waziri wa afya akilalamika bohari wamepewa fedha lakini hawanunui dawa, umeme ulikuwa 24/7, lakini leo tumeingia kwenye mgao.

Huduma katika taasisi za umeme zimeanza kuwa za rushwa.
 
2019 simu yangu iliungua kwa umeme kukata mara kwa Mara,tiliangalia mpira kwa jenereta Mara kwa Mara,hospitali na zahanati nyingi tu hazikua na dawa,sijui ilikua tz gani!?
 
Waziri akumbushwe michepuko sio dili, hayo mambo ya kuanza kuchepusha umeme wanaweza kuunguza gridi nzima nchi ikae gizani mwezi mzima

 
Swala la umeme limekuwa changamoto kubwa sana mimi najiuliza maswali mengi sana huu usiku wanafanya matengenezo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…