Lucas philipo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2017
- 2,039
- 2,676
Siasa za bongo ngumu.
Kipindi Dr Kalemani anatumbuliwa JF tulishangilia na kupongeza uteuzi wa January, Sukuma gang tukasinyaa kusubiri weledi wa waziri aliyeshangiliwa na wengi.
Muda si muda akaanza reshuffling, watu wakaula wa chuya, bodi ikajazwa wabobezi wa nishati. Tukapongeza humu.
Baada ya siku tukaambiwa sukuma gang waliharibu nchi, kwa miaka mitano mitambo ya umeme haikuwahi kufanyiwa marekebisho , watu wakashangilia humu. Sukuma gang tukaendelea kusinyaaa.
Kali ya waziri akasema Bwawa la umeme halitakamilika Kama ilivyopangwa awali, kwani tunahitaji Cranes kutoka mamtoni sijajua ilifikia wapi lakini sisi sukuma gang tukaendelea kusinyaa.
Tukaenda mikanganyiko ikawa mingi, huku wanasema mgao wa umeme huyu anasema hatutalala gizani huyu naye anakana hadi sasa nachokumbuka ni kwamba Rais ametoa agizo mgao wa umeme usiwe kama ilivyopangwa mjengoni yakasikika makofi lakini uhalisia
Hakuna umeme mtaani, wenye biashara zinazohitaji umeme wanajua, tumehamia kununua tochi hapa nina betri 10 reserved kwa ajili ya tamko la tanesco.
Sisi sukuma gang tunaendelea kunyamaza..Watu wale kulingana na urefu wa kamba zao wavimbiwe vya kutosha.
Hallelujah!!
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app