Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Hili ni tukio la kihistoria katika mchakato wa nishati safi nchini China na hata duniani, na linaashiria kuwa enzi ya umeme kwa nishati ya visukuku inamalizika, na enzi ya umeme wa nishati safi ikiwemo jua, upepo, na maji inastawi.
Nyuma ya takwimu hizo kuna mabadiliko halisi. Nishati ya jua inachangia asilimia 31.5 katika uzalishaji wa umeme nchini China. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, matumizi ya jumla ya umeme nchini China yaliongezeka kwa asilimia 5.3 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, huku sekta ya huduma ya mtandao na sekta ya huduma ya kuchaji na kubadilisha umeme wa magari ya nishati mpya zikikua kwa asilimia 44 na 56.9 mtawalia. Ongezeko hili kubwa la mahitaji ya umeme limetoshelezwa na nishati safi haswa jua.
Mafanikio haya yametokana na mipango ya kimkakati ya muda mrefu ya China. Mpango wa 15 wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa China unasisitiza kutekeleza kwa kina mkakati wa usalama wa nishati na kuharakisha ujenzi wa mfumo mpya wa nishati safi, usioleta kaboni nyingi, salama, na wenye ufanisi, na kuweka wazi lengo kuu: hadi kufikia mwaka 2030, asilimia 50 ya umeme itazalishwa kwa nishati safi.
Ongezeo la haraka la uzalishaji wa umeme wa jua pia linatokana na teknolojia za juu za kutumia nishati ya jua za China. Hivi sasa, China inashika nafasi ya juu zaidi duniani katika teknolojia hizo zikiwemo polisilicon, wafer za silikoni na viunzi, na kuunda mnyororo kamili wa viwanda vya kuzalisha umeme wa jua. Na viunzi vinane kati ya kumi vya fotovoltaic duniani huzalishwa nchini China. Mafanikio hayo si kama tu yamepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za ujenzi wa fotovoltaic nchini China, bali pia yamepunguza sana vikwazo vya kutumia nishati safi duniani kote, na kuruhusu nchi zinazoendelea kupata umeme wa kijani kwa bei nafuu.
Ongezeko la uzalishaji wa umeme wa jua nchini China lina maana kubwa. Linaashiria kuwa muundo wa nishati wa China unaelekea kuwa safi zaidi. Kama mzalishaji na mtumiaji mkubwa zaidi wa umeme duniani, hali hiyo si kama tu inaingiza nguvu ya kijani kwa maendeleo ya China, bali pia inatuma ishara wazi kwa dunia nzima: mageuzi ya kijani si wazo la mbali, bali ni ukweli unaoweza kufikiwa kupitia sera sahihi, uvumbuzi wa kiteknolojia, na nguvu ya soko. China inachangia busara yake katika mwitikio wa kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia vitendo halisi.