Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.
Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa