"Tuunde tume, kuna tume imeundwa, tusubiri matokeo ya tume, tume yatembelea vijjij kukusanya maoni, tume yafanya majadiliano, tume tume tume'!
Tume ya Muhimbili kuchunguza upasuaji, tume ya Raisi ya Madini, tume ya uchunguzi BOT, tume ya Dawasco, tume uratibu wa tume!
This is what our government has become. everything has a tume that is given a time frame that allows last minute uhujumu!
Okay, kwanza ni pole kwa wafiwa.
Pili je ni nini kilichotokea?
- Je ni kwa nini umeme wa Tanesco ulikatika? ni sababu za kiufundi, kiutendaji, uzembe, ajali au...?
- Je kwa nini ilichukua dakika 10 kwa Muhimbili kuanza kutumia umeme wa jenereta? je fundi alikuwa amelala, walikuwa hawana mawe kwenye kurunzi kuona swichi ilipo? je mafuta yalikuwa yamepungua kina cha kuwasha jenereta? je walisubiri mhandisi mkuu aongee na mkurugenzi mkuu wapate kibali cha kuwasha jenereta na kutumia mafuta ya dharura?
- Yameshatokea, je ni mipango gani itfanyika kuhakikisha kuwa patakapotokea tatizo kama hili wakati mwingine, ile mitambo ya kisasa inayojiwasha katika sekunde moja itakuwa ipo na inafanya kazi?
- Je hospitali na sehemu nyingine nyeti zina mipango gani madhubuti ya kuwa na mitambo ya kisasa kuhakikisha kuwa panapotokea matatizo kama haya, basi kuna back na recovery inafanyika katika sekunde na si dakika?
- Je Tanesco hawana powersource maalumu ambazo zitalisha sehemu nyeti daima kwa kualternate hata kama powersource moja imepata shida?
Tunadai uwajibikaji, je ni nani awajibike? Mhandisi mkuu, fundi wa zamu, mganga mkuu, wakurugenzi wakuu Muhimbili na Tanesco?, Waziri wa Afya, waziri wa Nishati, waziri mkuu, Raisi?
Kwa kuwa awamu ya nne imejijengea sifa ya kufanya mambo at ease, na kujivuta, sishangai ghadhabu za wana JF kudai ni uzembe wa Serikali hata kudai Rais awajibike. Iwapo Raisi angekuwa anafanya maamuzi mengine swiftly bila kuonekana na kigugumizi au kutafuta "win-win situation" inayoishia kumuonyesha kuwa hana uwezo wa kufanya maamuzi ya kuwajibisha watu, tusingekuwa na malezi komau ya watu na watendaji wasiojituma na kuwajibika bila kusukumwa!