Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.
Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.
Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.
Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.
Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.
Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.
Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).
Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.
Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa
..............Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu. ..............
Naona ndugu hapo hujaelewa kinachozungumziwa kabisa
Kwanza nikueleze, kikwete hajaonyesha dalili zozote za kiukweli zaidi ya unafiki mtupu katika kulitafutia swala la rushwa suluhu, kwa sababu nyingi tu, unakumbuka watu walipowataja mafisadi wakuu alitoa kauli gani ya kuwajibu wapinzani? lakini umeyaona yaliyoibuliwa na Slaah sasa,
Unakumbuka wakati anaongea na wazee wa mkoo wa Dar alieleza nini kuhusu EL na baadae alieleza kitu gani kuhusu Kamati teule ya BUNGE, kama unayo majibu hapo utakubaliana nami kuwa JK anatupuliza uku akitungata.
Na kinachozungumziwa hapa, sio kuwa JK anatakiwa kukumbusha mppaka mafuta ya Generate, swana ni kwamba kutokana na kasumba mbovu ya kuindesha serikali, ambapo anashindwa kuwawajibisha mawaziri wake, haya ndo yanatokea, na ndo maana watu wanamuona JK kama responsible person, kwa sababu hafanyti kazi zake huko juu, kama juu hawawajibiki inategemea nini huku chini kaka??
Tafakari haya mambo kaka
Wanabodi ,
Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.
.....Ndugu Dar Es Salaam...kwa hili nakuunga mkono na kw ahiyo swali la msingi la kujiuliza ni
1. Standby Generator Ipo au haipo?
2. Kama ipo nani yuko resonsible nayo? (nafikiri hapa ni uongozi mzima)
3. Kama haipo WHY?.....je ni suala la bajeti? je ilikuwa knocked out kwenye bajeti? (again hapa ni uongozi mzima unawajibika)
.........kuna vitu vingine ni very basic katika institution nyeti kama hii ambayo huwezi kukwepa kwa kusingizia bajeti au sababu yeyote ile......ni lazima kuwepo na Standby Generator tena iwe ina-chekiwa na kupashwa moto mara kwa mara
Kwanini JK analaumiwa........
mikataba mibovu na kushindwa kwake kuwashughulikia viongozi wabovu ndio unasababisha uzembe kama huu uliotokea Muhimbili.........this may not be seen by many of us.....lakini ndio ukweli wenyewe.....................kila mtu serikalini ameuchapa usingizi mnono.........mikataba mibovu hawaioni na hata wakiona hawasomi na hata wakisoma hawaelewi na hata wakielewa.............kwa sababu ya interest ambazo hazijulikani.............WANASAINI!!!............shame on them!!!..................all these blunders have a knock on effect ktk idara nyingine za serikali kiuchumi na ndio sababu mambo kama yaliyotokea Muhimbili yanakuwepo
Jamani Jenereta ya kukaa standby kama pale Muhimbili inagharimu karibu dola laki moja hivi na kidogo. Kimsingi mnachosema ni kuwa katika Wizara yetu ya Afya hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua dakika chake kuangalia mtandao na kugundua kuwa zipo "Standby Generators" ambazo tunaweza kuzimuda na tunaaweza kununua moja kwa moja toka kwa watengenezaji.
kwa vile mimi ni mzalendo nimewapa website ya kampuni ambayo ni "maslahi" kidogo. Nawashauri wawasiliane nao na wakiulizwa nani amewarefer waandike, http://www.klhnews.com ili na miye nipate katenda kidogo.
http://www.generac.com/Default.aspx
Dar es Salaam,
Kuwa muelewa hapa sio manual Generate, watu hapa wanazungumzia kuhusu automatic standaby generate, yaani amabyo umeme ukikatika wala uwezi kujua kama umeme umekatika, hili ndo swala linalozungumziwa hapa, na sio generata za kufuta na kamba ndo ziwake jamani, ebu utuelewe tunachojaribu kueleza hapa
Ingekuwa ni hivyo usemavyo wewe basi kila siku tungesikia tatizo hilo.
.. Mwafrika, kikwete hawezi kukwepa lawama kama hizi. Na ndio maana katika nchi za magharibi mambo kama hayo yanapotokea anayewajibika ni waziri anayehusika na hiyo sekta.
Lakini tujitizame na sisi wenyewe tunapofanya kazi. Je tunatimiza wajibu wetu??? Nadhani unakumbuka ulipokuwa Mlimani mkuu wa idara alikuwa anaweza kuikalia dissertation yako kwa miezi kadhaa kabla ya kupelekwa kwa external examiners. Sasa jamani, hapa kweli tatizo ni la waziri wa elimu ya juu au mkuu wa idara???
Kimsingi, nakubaliana na wewe kwamba kikwete hawezi kukwepa hizi lawama. Lakini uongozi wa hospitali unawajibika kwa huu uzembe.
Mkuu! Automatic Generator haichukui dakika KUMI kuwashwa. Inajiwasha yenyewe. Hizo dakika kumi ni kutokana na maelezo yao.