Mimi nadhani huyo rafiki yako siyo mkweli. Huwezi kuishi na msichana kama mpenzi wako kwa miaka 7 halafu unasema humpendi, kama moyo wako haumpendi msichana ni vigumu sana kukaa nae muda wote huo especialy mvulana. Huyo rafiki yako haja komaa ki-utashi na bado hajajua maana ya ndoa, ndio maana amesha-oa halafu anasema hampendi msichana. Lazima atumbue kuwa hakuna mwana mke au mwana ume mwenye miujiza ndani ya ndoa, kitu kikubwa ndani ya ndoa ni kumpata mwenza mnaelewana ki-mtazomo hizi taama za kujamiiyani ni kitu kidogo sana ndani ya ndoa kwa upana wake. Mwambie rafiki yako aache mtazamo hasi ya kuwa amemuoa huyo binti kwa ku-msaidia bali ajue ni mke aliye mchagua mweyewe na angalie ni jinsi gani ya kushirikiana na mkewe kujenga maisha yao yanayo wakabili.