Umemuoa/Kakuoa kwa kuwa unampenda?

Umemuoa/Kakuoa kwa kuwa unampenda?

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
1,736
Reaction score
408
Kwa wale waliooa au hata wale ambao wanatarajia kuoa au kuolewa karibuni hebu nijuzeni kama huyo mwenzi wako umemuoa/kakuoa kwa kuwa mnapendana au ni kwa kuwa amekuonea huruma tu kwani akikuacha anaona utahangaika sana.

Hii ni hali halisi ambayo imemtokea rafiki yangu ambaye amefunga ndoa hivi karibuni kwa kinywa chake anakiri kuwa amemuoa huyo aliyemuoa kwa kuwa tu anamwonea huruma tu kwani walishakuwa katika uhusiano kwa takribani miaka saba lakini moyoni mwake anaona kuwa hana mapenzi nae.
 
Kupenda maana yake ni nini? Au unajaza tu kurasa hapa JF!
 
Kwa wale waliooa au hata wale ambao wanatarajia kuoa au kuolewa karibuni hebu nijuzeni kama huyo mwenzi wako umemuoa/kakuoa kwa kuwa mnapendana au ni kwa kuwa amekuonea huruma tu kwani akikuacha anaona utahangaika sana.

Hii ni hali halisi ambayo imemtokea rafiki yangu ambaye amefunga ndoa hivi karibuni kwa kinywa chake anakiri kuwa amemuoa huyo aliyemuoa kwa kuwa tu anamwonea huruma tu kwani walishakuwa katika uhusiano kwa takribani miaka saba lakini moyoni mwake anaona kuwa hana mapenzi nae.

watu wamevunja uhusiano wa miaka kumi, sembuse saba? huyo rafiki yenu hasemi ukweli, ukweli anao mwenyewe
 
Amefanya kosa kubwa sana maishani mwake. Atakaa akijutia uamuzi wake huo mpaka kaburini. ina maana miaka saba yote kakaa tu na mtu ambae hampendi? ye aseme amepata mwingine kulekule tunarudi mambo ya kuoneana huruma, unamwonea huruma umezaliwa nae huyo binadamu??
 
Mimi nadhani huyo rafiki yako siyo mkweli. Huwezi kuishi na msichana kama mpenzi wako kwa miaka 7 halafu unasema humpendi, kama moyo wako haumpendi msichana ni vigumu sana kukaa nae muda wote huo especialy mvulana. Huyo rafiki yako haja komaa ki-utashi na bado hajajua maana ya ndoa, ndio maana amesha-oa halafu anasema hampendi msichana. Lazima atumbue kuwa hakuna mwana mke au mwana ume mwenye miujiza ndani ya ndoa, kitu kikubwa ndani ya ndoa ni kumpata mwenza mnaelewana ki-mtazomo hizi taama za kujamiiyani ni kitu kidogo sana ndani ya ndoa kwa upana wake. Mwambie rafiki yako aache mtazamo hasi ya kuwa amemuoa huyo binti kwa ku-msaidia bali ajue ni mke aliye mchagua mweyewe na angalie ni jinsi gani ya kushirikiana na mkewe kujenga maisha yao yanayo wakabili.
 
Kwa wale waliooa au hata wale ambao wanatarajia kuoa au kuolewa karibuni hebu nijuzeni kama huyo mwenzi wako umemuoa/kakuoa kwa kuwa mnapendana au ni kwa kuwa amekuonea huruma tu kwani akikuacha anaona utahangaika sana.

Hii ni hali halisi ambayo imemtokea rafiki yangu ambaye amefunga ndoa hivi karibuni kwa kinywa chake anakiri kuwa amemuoa huyo aliyemuoa kwa kuwa tu anamwonea huruma tu kwani walishakuwa katika uhusiano kwa takribani miaka saba lakini moyoni mwake anaona kuwa hana mapenzi nae.

Ndoa nyingi ziko kwa mtindo huu. Hizi kitchen party zinawadanganya watu wengi. Wengi wanajiingiza kwenye ndoa ambazo ni ndoana kwa kweli. Ukisikia fulani kaoa/kaolewa na wewe unataka mtalia!! hahhaha ndoa za bongo bana kama movie vile
 
Huruma ya nini bana pata kitu roho inapenda ndio wale maharusi ukiwaona mbele wamenunaaa mpaka wageni waalikwa mnaulizana kulikoni
 
Nitaoa kama atakuwa ananijali na kuniheshimu.
Huruma itakuwepo ili nisimuumize.
 
Tumeoana sababu tunapendana sanasana hakuna jingine mengine ni majaliwa ya mwenyezi mungu,
 
Back
Top Bottom