mtoa mada kwa hili usisingizie wanawake tu , kumbuka hapo hapo hata wanaume wa umri huo kuendelea mnakua mme ruka ruka na bado mnaruka ruka sana na hujui unako ruka ruka kuna nini, kusema wanawake tu ndo tunabeba laana sio, kifupi ni kwamba wote tuna laana za mambo tuliyofanya nyuma, na mtu unapotaka kuoa au kuolewa hufanyi toba kukataa vyote tulivyofanya nyuma ili tuanze upya ila unaingia kwenye ndoa na laana zako. Na swala la kwamba zamani waliolewa ma bikra hapa tutofautishe zamani na saivi, umri wa mtoto wa form one saiv ndo umri ambao bibi ake mzaa bibi alikua anaolewa , na hiyo miaka 25 mtu wa zamani alikua tayari ana watoto kadhaa wakati saivi bado una somaga tu. Kwahiyo kama shida ni bikra utaratibu wa zamani wa kuolewa mapema ungekuwepo mpaka sasa zingekuwepo sana tu, japo bado wapo watu umri huo bado wanajitunza.