Umeota nini?

Umeota nini?

Hii nfoto hua inajirudia, naota nakimbizwa(haijalishi kitu gani, inaweza kuwa mtu au mnyama) ila kila akinikaribia inabidi nipae nimuache, style ya kupaa naanza kwanza kukimbilia miguu minne kama chui halafu na take off kama ndege.
Kuna baadhi ya maadui nikipaa na wao wanapaa.
ila nikiona wamenikaribia sana hawakati tamaa nasema acheni ujinga najiamsha kutoka usingizini.
 
ongeza juhudi, uzuuiyaji unakutaka
 
Tuko boarding tunapigania ndoo za kuogea, halafu nyingi zimepigwa makufuli chini ya vitanda.
ila kukawa na ndoo moja imezubaa ila tukiikimbilia tu mwenye nayo anatokeza from nowhere, halafu tunaiacha.
Tunarudi kutafuta tena baadae tuaniona tena ile ndoo imezubaa....tukiifuata tu, mwenye nayo anatokea from nowhere, yani kama anatutega vile
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28] Aisee! Nimecheka sana sio poa
 
kila mar namuota Ex, majuzi nimemeota ananitambia kwamba huko alipo mambo shwari, jana nimeota nimepita maeneo fulani nikamkuta anaosha vyombo na kimuonekano alikuwa kidesign kama kachoka hivi then akawa kama akijaribu kunikwepa nisimuone na mimi nikajifanya kama sikumuona.
 
Achana nae bhana
 
Kuna siku niliota narudi nyumbani wakati narudi kwa mbali nikamuona mdogo wangu na mmama fulani ambaye ni jiran wamekaa mlangoni yule mama akaniambia nakuomba unichumie jani la boga mdogo wangu nae akasema mletee jani la boga nikasema siwezi rudi nyuma kwann hamjaniambia toka nilipopita hapo,mbele palikuwa na matope nikawa na pita lakini sichafuki mbele nikaona mti una matunda nikatembea mbele ila nikawaza kwann nisirudi nichume yale matunda nikarudi nikawa na hangaika kweli man yapo mbali halafu mti una wadudu ila nikafanikiwa kuyachuma ila tunda moja likawa kama lina doa jeusi wakati nmemaliza nikamuona kuna mbaba ana pita na baiskeli ila kwenye baiskel kafunga shela nyeupe(gauni refu)nikawa najiuliza huyu amepitaje pale kwenye matope na hilo gauni linaonyesha halijachafuka wakati ni refu linaburuta hadi chini nikapotezea nkawa nakuja nyumbani yake matunda nikawa nmeyaficha kwa nyuma.
 
Ndoto nyingine nmeota nipo stand nmemsindikiza X akawa anasema mbona usafiri shida akasogea mbele kuna sehemu kuna meza akawa amenipa mgongo nikawa namuita namwambia mbona usafiri huo panda hanisikii basi mimi nakawa naelekea uelekeo alipo ili niende nyumbani, nikapita alipo simama nikawa namwambia endelea kusimama hapo usafiri huo Subiri uchelewe nakaona bajaji mbili moja nyekundu moja nyeupe nikajua atapanda ile nyekundu nikaona ana elekea ilipo ile nyeupe mimi nikawa na endelea kutembea sikufatilia huku nyuma kwamba alipanda au laah wakati natembea kurudi nyumbani nikawaona ng'ombe wawili wakubwa tu wanavutia machoni ila wana rangi mbili mabaka baka nyeupe na nyeusi halafu mmoja ana pembe ndefu zimechongoka,nikawa naogopa kupita napita pembeni ila nilivyoona hawana madhara sikuwaogopa ten ila walikuwa wana nitazama sana kwa huruma hasa mwenye pembe nikawapita wakati nazidi kutembea nyuma yangu kuna mkaka nae alikuwa ana tembea ila sikugeuka kumuona sura alikuwa ana niongelesha naitwa nani?,nafanya kazi wapi?nikawa na mjibu tulivyo maeneo ya nyumbani nikamwambia kwetu ni hapa akasema ooh mimi bado naendelea na safari basi akapita huko na mimi huku nikawa nawaza huyu kaka mbona hajaniomba namba nikashtuka.

NOTE:[emoji24]nashangaa nilikuwa najibu ninapo fanyia kazi wakati kazi sina ni mlinzi wa nyumba [emoji24].
 
Back
Top Bottom