Umepata somo gani la maisha 2022?

Kama Ya Jana yamepita hata haya ya Leo yatapita

Tupunguze kujiumiza tunapopitia magumu, kesho tutayatizama Kama historia tu

2022 imekuja na miujiza mingi na mitihani mingi sana

Mungu ni mwema [emoji120]
 
Umemaliza
 
Mimi nmejifunza yakua ili upate msaada inatakiwa uwe umeshajisaidia kwa hatua kadhaa,Msaada ama connection hua zikija lazima zikute strong foundation ili iwe rahisi kutopoteza nafasi .

Kingine kuna watu tunachart nao tunacheka nao na tuna shida zetu very sensitive usitegemee akusaidie bila ya kumweleza shida yako...Unaweza saidiwa na mtu ambae hatokuomba hata cent yako tena msaada mkubwa sana ila tu kazima uombe msaada huo

Inawezekana kupiga hatua kama utakua na nidhamu katika kila kitu

Watu wenye bidii na wavumilivu hua wanapata matokeo hata kama ni kwa kuchelewa

Usipende kua karibu na watu ambao hawana mawazo ya kujenga maisha sanasana wanaumbea wa watu wengine na hadithi hasi tu

Jali sana afya yako kwa kujiepusha na ngono zembe,ulevi usiokua na tija na ulaji wa hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…