Umepata somo gani la maisha 2022?

Umepata somo gani la maisha 2022?

Kwa maisha ya kibongo piga ua galagaza hakikisha kila sh 1000 unayoiingiza weka akiba ya sh 150 (15%) ambayo hutaigusa...
 
1.Epuka kuforce mahusiano na mtu ambaye Hadhamini upendo wako.
2.jipende and have fun life is short.
3.kuna muda wale ambao ulikuwa unawategemea Kwa jambo Fulani watakukimbia utabaki mwenyewe.
4.jifunze kuongea Kwa break,usiwe mropokaji,ongea Kwa timing.
5.epuka mikopo isiyokuwa ya lazima.
6.kila siku penda kujifunze kitu kipya .
7.usipoteze mda na kitu kisichokuwa Cha maana.
8.jilinde na utunze afya yako.
9.mwamini Muumba wako.
10.jiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
Be blessed
 
Mimi nmejifunza yakua ili upate msaada inatakiwa uwe umeshajisaidia kwa hatua kadhaa,Msaada ama connection hua zikija lazima zikute strong foundation ili iwe rahisi kutopoteza nafasi .

Kingine kuna watu tunachart nao tunacheka nao na tuna shida zetu very sensitive usitegemee akusaidie bila ya kumweleza shida yako...Unaweza saidiwa na mtu ambae hatokuomba hata cent yako tena msaada mkubwa sana ila tu kazima uombe msaada huo

Inawezekana kupiga hatua kama utakua na nidhamu katika kila kitu

Watu wenye bidii na wavumilivu hua wanapata matokeo hata kama ni kwa kuchelewa

Usipende kua karibu na watu ambao hawana mawazo ya kujenga maisha sanasana wanaumbea wa watu wengine na hadithi hasi tu

Jali sana afya yako kwa kujiepusha na ngono zembe,ulevi usiokua na tija na ulaji wa hovyo.
Afya ya akili na mwili ni mtaji tosha.
 
Haya ndio niliyojifunza na yamenijenga kianza upya vizuri next year.

1- Usijipe umuhimu kwenye maisha ya watu. Watu niliowasaidia na kutoa muda wangu kumake sure they make it hata kama sina na nikasaidia hata kwa kutoa muda wangu, mawazo na kufanya kwa kadri nilivoweza, lakini mambo yalivoniendea vibaya ndio hawakutaka hata kunisikia, hata simu yangu haikupokelewa, wala sikuona hata text kujua unaendeleaje nk, pia kila nilipohitaji msaada wao basi jibu lilikua either kutojibiwa kabisa, kuambia pia sina kwa sasa etc, hahaha nikajua wale i thought mimi ni wa muhimu kwao na nikawasaidia wakati naweza ndio hawa wananikataa live baada ya kupata shida, well somo nimelielewa.

2- Ukiwa kazini just do your work usitake kujibebesha mizigo ya wengine isije kuangusha wewe, kifupi usimuamini yoyote ukiwa kazini, just be you and do your work. Kuna my friend kwenye place yake mpya ya kazi baada ya kupanda cheo last year, alipofika wakati wa makabidhiano yule alietakiwa kumkabidhi akawa kaondoka kaiba kiasi kikubwa cha pesa (kama 10M), akasema itabidi areport uongozi wa juu zaidi cas hawezi kabidhiwa ofisi haijakamilika, yule kiongozi wa ukaguzi na issue usimamizi wa fedha akamlilia sana ofisini akasema usitoe taarifa maana akitoa basi staff wote wa ile ofisi watafutwa kazi kwa uzembe ikiwemo yeye na watu wanafamilia zao awaonee huruma ila wataji organize hiyo pesa waweze kuireplace within few months ye aandike tu everything is ok, kibinadamu mtu mzina kukulilia na kukwambia situantions na akaona kabisa boss alieondoka aliiba hizo pesa na hakuna njia ya kumpata, ikabidi jamaa akubali. To make story short, after some months pesa haikua replaced then yule yule aliemlilia alamtengenezea zongo na akatoa taarifa yake ya ukaguzi kwa uongozi na kusema kakuta 10M haipo na wakati wanamkabidhi ofisi eti ilikuepo, jamaa anafika asubuhi ofisini anakuta ujumbe kwa secretary aende HQ kuna kosa limefanyika na pia wakaguzi wanakuja kutoka HQ, basi akasema hapa najua kila kitu kiko sawa isipokua ile 10M , bila kujua kua kashachomewa akaazima 10M kwa rafiki zake wengine aiweke tu then ukaguzi ukiisha awarudishie, na akamshirikisha yule yule jamaa mkaguzi wa hapo kua anaazima pesa ili ile isilete shida, akasema poa, kumbe pale pale jamaa katuma email HQ na ma sms kua kasikia jamaa amereplace ile pesa iliopotea ili ionekane ipo na kaazima kwa flani bank flani, dah jamaa anafika anajiamini alafu akakuta masaibu hayo na kila kitu kiko mezani.... hahah kifupi na kujutetea kote jamaa alipoteza kazi na vile alikua nchi ya watu basi kazi aliokua kaanza kufaidi matunda yake makubwa ikaisha within 7 month tu. Just do your job na usipende kujibebesha mizigo isokua yako.

3- Ukiwa na pesa wekeza, hasa kwenye mali na vitu vya thamani, kuliko kutumbua tu, sometimes nunua hata viwanja sehemu za.mbali vinapouzwa bei rahisi hata mikoani, nunua hata vito vya thamani vya dhahabu, diamond, pete za dhahabu, cheni, Tv za bei ghali, friji , makochi ya thamani, na vitu vingine vya thamani, sababu hivi vinaweza kua.mkombozi wako mkubwa wakati unapopata changamoto, kuliko kukopa na kubaki na madeni basi vitu hivyo vitakua mkombozi wako kwa wakati usioutarajia.

4- Usikope kama unajua wakati huo sio rahisi kwako kurudisha kutokana na changamoto mfano kama huna kazi, usikope. Ni bora uombe usaidiwe kuliko kukopa, epuka kukopa, hasa kwa watu wako wa karibu. Watu this year wamevunja sana uhusinano na ndugu na marafiki na.kuishi kwa wasiwasi sababu ya kushindwa kulipa madeni, sio kwa kupenda ila ni kweli wamekosa ya kulipa, please USIKOPE. Inaondoa hata baraka watu wakiwa wanakudai na kukuwazia vibaya.

5- Tumia pesa zako kujinufaisha wewe na familia yako, watu wengine wasaidie ukiona kuna umuhimu na una cha ziada, sababu watu hawathamini msaada kabisa, ukishawasaidia basi imetoka, na utaumia zaidi pale siku wewe unapata shida na huna wa kukusaidia.

6- Ni bora kutokua na marafiki (best friends) kuliko kua na marafiki ambao hawana msaada wowote kwako yani hawakuongei wala kukupunguzia chochote zaidi ya wao kutegemea wewe na kukunyonya na vya kwao wanabana. In 2023 jitahidi kujipenda wewe kwanza na kufanikisha mambo yako na ya wengine yanaweza kusubiri kwanza. Mrafiki ambao ukiwa na shida hawakusaidii na hawana uwezo wa kukusaidia ila wao huomba msaada kwako na unawasaidia kila wakati just leave them ama waweke kwenye ignore lists.

7- Usitangaze shida zako, usimwambie mtu shida zako, pambana how to solve it ila usiwaambie watu unayopitia.

8- Siri ndio njia ya kufanikiwa, kua na siri usiwaambie watu mipango yako, hata kama unataka kujenga, usiambie watu, hata friends. Hata kama unataka kubuy gari usiambie mtu. Hiki ndio chanzo kikuu cha kufail mambo mengi sana. Try this next year uje hapa kunishukuru.

Let 2023 be about you, and you
Iko bien
 
BE CAREFUL OF THOSE PEOPLE WHO ARE CURIOUS ABOUT YOUR PROGRESS IN LIFE BUT DON'T ENCOURAGE OR SUPPORT YOU.
 
Back
Top Bottom