Umepatwa na Emergency ya milioni 10, Unatoboa?

Umepatwa na Emergency ya milioni 10, Unatoboa?

Umepatwa na emergence inayohiitaji pesa cash milioni 10 ndani ya lisaa

1. Tatizo la kiafya (Kufa au kupona)
2. Mapolisi (Ujichomoe haraka au kifungo cha maisha)
3. Mtoto katekwa (wakivuka mpaka wa nchi ndo bas tena)

n.k.
Unaongelea milioni kumi wakati watu hata pesa ya kula kesho hawana. Kutavokucha Mungu ataleta ridhiki
 
Kwa huu ukwasi nilionao nahisi hata nikiwa nayo sitatoa. Labda niwe na zaidi ya hiyo
 
Basi kwa hapa bongo hata watumishi wa serikali wa kada za chini hawajafikia standard life.
Wengi kipato wanachopata ni kwa ajili ya kuendeshea maisha tu.
Kipindi kile cha korona kilituvua nguo kwamba sekta binafsi hawawezi kusavaivu kwa miezi miwili kutegemea mshahara.
Hizo hesabu ni za ku maintain maisha ya kawaida bila kutetereka kwa miezi 6 kwa familia ya baba, mama na mtoto mmoja.

Maana yake familia ikiongezeka au muda ukiongezeka na hiyo amount inatakiwa kuongezeka.

Ila kama ulivyosema, Watanzania wengi hawaishi maisha standard. Yani wengi hata kivuli cha standard tu hawafikii.
 
Kumbe wewe una million 100 tu watu kichwani tuna trilion 2 tunaisubiri mda wa kuziwithdraw kutoka "kichwani" ufike anytime
Kwa maisha standard ya sasa unatakiwa kuwa na access ya shilingi milioni 80 mpaka 100 ya haraka wakati wowote. Bila kumsumbua mtu, kuomba mkopo, wala kuharibu biashara zako zingine
 
Hapa nilipo siwezi kupata emergency ya 10m, emergency zangu hazijawahi kuzidi 200k
Zipo ila umezitoa tu kwamba zipo nje ya bajeti yako na maisha yako.

Ukipata ugonjwa (sikuombei iwe hivyo, natoa mfano tu) wa kutakiwa usafirishwe hata hapo India tu kwa matibabu, hiyo ni emergency lakini sasa hujaiweka katika bajeti yako kwa sababu umeona hayo si maisha yako.
 
Gang gang..
Mimi nimeishi kwenye mazingira magumu ya gang, skuweza hata ku maint..
Skuweza hata kufikilia furaha mana kila siku same pain.....
 
Zipo ila umezitoa tu kwamba zipo nje ya bajeti yako na maisha yako.

Ukipata ugonjwa (sikuombei iwe hivyo, natoa mfano tu) wa kutakiwa usafirishwe hata hapo India tu kwa matibabu, hiyo ni emergency lakini sasa hujaiweka katika bajeti yako kwa sababu umeona hayo si maisha yako.
Upo sahihi mkuu
 
Kwa mtoto hapo nitabargain na watekaji wanipunguzie kutoka million 10 hadi elfu 50, nitawaruhusu wampunguze hata masikio ili bei ishuke, hiyo 50k yenyewe kuna sehemu nimekopa saa hiyo
Watekaji dawa yao unawaambia tu sitoi hata senti njooni mnichukue na mimi hata mniue mnimalizie matatizo ya dunia.

Wataona hapa hamna diki bora tumrudishe tu huyu mtu.

Kuna tapeli mmoja alimpigia simu Mpemba anataka kumtapeli kimtandao, Mpemba akaanza kumtajia matatizo yake, madeni anayodaiwa, vurugu za maisha yake, mpaka yule tapeli yeye ndiye ikawa anaombwa pesa amsaidie yule Mpemba ikabidi tapeli mwenyewe akimbie.
 
Unaongelea mil 10? Wengine hata kesi ya laki hatutoboi!

Uzuri wake matatizo huwa yanakuja proportional na uwezo wako!
Kweli 10M nyingi sana, niliwahi kupata emergency ya 20k sikutoboa
 
Sijasema wanafika, nimesema kwa maisha ya standard ndiyo unatakiwa kuwa hivyo.

Sasa wengi bado wanakufa kwa kipindupindu Simiyu huko Meatu, maana yake wanakula au kunywa mavi bado, hayo si maisha ya standard.
Eeeh..nchi ina miaka 60+ years old bado watu wanakunywa mavi? Duh..
 
Back
Top Bottom