Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

Nangojea majibu ya hii kitu, mimi niko na Subaru Forestet 2008, tangu nije Dar inakula 6.8 - 7.2 km/L. Hizi foleni zinachangia huu ulaji?

Ila nikiwa Moshi inafika mpaka 10.5 km/L
 
Toyota Ist inapoendeshwa ikipiga bamz hasa zile bamz ndogo-ndogo ikiwa speed, nasikia kelele(kelele kama za upepo unatoka) kwenye tairi la upande wa dreva mbele, kisha gari inawasha taa ya check Engine na inazima. Ukiwasha inaendelea. Baada ya muda inatokea tena. Shida ni nina wakuu?
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
 
Ka Ushakutana na shida yoyote kwenye gari yako ikakutatiza share Hapa Usaidiwe
Toyota Ist inapoendeshwa ikiwa kwenye foleni mwendo mdogo sana inazima redio kisha inawaka dashboard inawakataa zote gari inazima na kisha ukiwasha gari inawaka na kwenye mwendo usio wa foleni haiizimi nini tatizo?
 
Mkuu ulirekebisha? Nina same issue kwa Rav 4 Old
Cheki gearbox mounting,kama inashida badilisha funga nyingine,kingine katazame diff ya kwenye gearbox je haina shida yoyote
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
Gari kuvibrate ukiwa umekanyaga brake ,shida huwa ni disk rotor,na vile vile ikivibrate baada ya kuwasha ac ,shida huwa ni engine mounting
 
Toyota passo, inawaka taa ya over speed na ikibadili gear inakua kama inastuka. Kwa hiyo inabidi ukiona inataka kubadili gear uachie pedo ndio ibadili. Shida yaweza kuwa ni nini maana nishabidili mpaka gear box.
 
Kimeo changu Duals leo kimenigomea ghafla

Natoka zangu posta nakwenda TbT kufika jangwani ikazima, nikatoa gia nikawasha ikawaka, kabla sijafika kigogo ikazima
Mwendo umekua ndio huo
Hapa nipo nimeipaki hapa kigogo napoza kiu nimtafute fundi wangu

Shida ni gani labda?
 
Honda CR-v, manual, year 2002

● Inakula sana mafuta
● Gari inakua nzito
● Inakosa nguvu kwenye kupanda mlima au ku overtake hadi unalazimika kushusha gear na kutumia gear kubwa 1 au 2 ili kukusanya nguvu na kupelekea matumisi makubwa zaidi ya mafuta
● ikifika speed 60 au 80 inaleta miss
● Taa ya SRS airbag inawaka na haizimiki

Shida itakua nini hapa?
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
Nahizi ubadili Engine mount mkuu
 
Gari yangu nikipark, kwa siku 1 au 2, nikija kuwasha nasikia harufu kali ya petrol ndani na nje ya gari, tatizo nini?

Ila nikiitumia mfululizo nikiwasha sisikii hyo harufu, shida ni ikikaa hata siku 1 bila kuitumia, kesho yake ukiiwasha harufu inatoka
 
Hivi naweza kupata engine ya aina hii ya gari? Pia ningependa kujua bei na uzima wake,yaani sitapigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…