Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

Ilinitokea
Gari kila nikikunja kona hadi mwisho (kulia) inajizima. Naiwasha inawaka naendelea na safari.
Baadaye ikaacha, lakini hadi leo sijui tatizo
 
Gari kutoa moshi mweupe, ilipinduka matairi juu, hakuna leakage kwenye engine, naambiwa oil ilingia kwenye exszost ndo mana inaunguza oil je ni sahihi?
Mie ya kwangu ililala hvo hvo ila ikaanza kunisumbua inamisi hovyo na kupandisha oil kwenye plug. Ikabidi mpaka niifunge ring piston tu.
 
Wheel alignment ni uwekaji (setting) wa matairi katika ufanyakazi wa urari. Kama tairi haziko katika urari (alignment) ukinyoosha uskani gari itaenda kushoto au kulia. Kwa ufupi wheel alignment inahusiana na

wheel alignment inahusiana na suspension ya gari hasa sehemu zinazoshikilia tairi. Hivyo unapofanya wheel alignment tairi haiguswi.

Wheel balance inahusiana na ujazo wa tairi linapotoka kiwandani. Kama tairi halina ujazo uliyojaa kwa vipimo sawa basi litasawazishwa kwa kuongezewa baadhi ya vitu na hii ndiyo wheel balance.

Dalali za kuwa gari yako inahitaji wheel alignment ni gari kwende kushoto au kulia ili hali uskani upo katikati.

Dalili za kuwa gari yako inahitaji wheel balance ni uskani wa gari kutetemeka unapofikia speed fulani na pia tairi kuisha sehemu mmoja pia inaweza kuwa dalili.
Ahsante mkuu
 
Nikiwasha ac nitatembea baada ya muda gari itajizima, haitowaka mpaka battery icchajiwe.
Kuhusu battery nishaipima sehemu tofauti haina shida, why nikiwasha ac inajizima?
Kuna fundi alisema alibadilisha jino la altenator, na akasema alternator haina, mwingine akasema alternator haina shida.
kuna mmoja akabadilisha kifaa sikumbuki jina.

Hii ni mara nyingi mafundi washanilia hela sana.
Nimeipaki, siku ikinilazimu kutumia inabidi nisshushe vioo.
Nawaza mvua zikianza itakuwaje?
Maana mwenyewe kinanisave hatari kwenye mafuta.
Nikiwa na 10,000 nauhakika wa kwenda na kurudi.
Ila kuna jini hapa mpaka nitoke niwe na 30,000.
Samahani mkuu ni gari gani kama hutojali
 
Suzuki Escudo engine G 16 automatic transmission ikitembea inakuwa kama ipo free mafundi huku kjijini wanasema ni tatizo la gearbox utatuzi wengine wanasema nifunge gearbox nyingine wengine wanasema kuwa ndani ya gearbox huwa kuna plates za kubadili tu nipo kijijini sijui kipi ni sahihi
 
Suzuki Escudo engine G 16 automatic transmission ikitembea inakuwa kama ipo free mafundi huku kjijini wanasema ni tatizo la gearbox utatuzi wengine wanasema nifunge gearbox nyingine wengine wanasema kuwa ndani ya gearbox huwa kuna plates za kubadili tu nipo kijijini sijui kipi ni sahihi
Fafanua vizuri ikitembea inakuwa free, yaani, gear haziingii au wewe ndiye unayehisi kama gear hazi-engage?
 
Hii ni gari gani inatetema hivyo kama mayele?
Mkuu angalia balance ya upepo pia. Kama moja ya tyre ina pressure kubwa kuliko nyingine hilo tatizo haliepukiki.
Mimi nimekosa muda wa kuziba moja ya tyre langu hilo tatizo nakutana nalo kila baada ya siku tatu. Nikibalance upepo natembea vema kabisa kama niko na Range.
 
Gari kutoa moshi mweupe, ilipinduka matairi juu, hakuna leakage kwenye engine, naambiwa oil ilingia kwenye exszost ndo mana inaunguza oil je ni sahihi?
Gari kutoa moshi mweupe hapo kuna gasket zinavuja oil inachanganyikana na mafuta. Au coolant inavuja. Au fuel injector imekufa hivo kupelekea gari kutumia mafuta mengi kwa umbali mdogo.
 
Premio Automatic Gia D inazingua ukiwa speed ndogo gar inapunguza speed,Gia L na 2 gar inaenda vizur
 
Gari kustuka unapoweka gear river, na pia inawaka taa ya over driver na kulalamika kubadili gear. Hii inasababishwa na nini???
 
Wewe Mbute bora ukauke uwe bhutaga sasa. Gari ile inatetemeka ikiwa Silence ikianza kutembea inatulia tuliiiii unapiga hadi 160 safi. Tatizo ikisimama tu lazima utoe kwenye D uweke kwenye P au N ndio hutosikia mtetemo lkn ikiwa imesimama ikawa engaged kwenye D ni kasheshe
Hadi leo hajakujibu hii😁😁😁
 
System ya umeme ina shida na prolly alternator. Vua hio kitu weka ingine utakuja kunishukuru. Najua laki na 80 inakuuma ila lipa hio hela weka alternator ingine. Umeme ukiwa hautoshi au unafuliwa chini ya kiwango ndio shida kama hizo hujitokeza provided battery sio chakavu.

Gari la bro wangu likiwa kwenye speed linatetemeka amelipeleka kwa mafundi tofauti but wote wamechemka wa mwisho alimuambia achange tire kachange lakini tatizo bado lipo, shauri chochote mkuu.
 
Gari la bro wangu likiwa kwenye speed linatetemeka amelipeleka kwa mafundi tofauti but wote wamechemka wa mwisho alimuambia achange tire kachange lakini tatizo bado lipo, shauri chochote mkuu.
Hahahahah mkuu gari inatetemeka ana hakika bearing ziko sawa pamoja na mountings? Kama viko byee basi afanye mpango wa wheel balance. Isipofaa hapo acheki mfumo mzima wa uchomaji kuanzia air filter, fuel filter, nozzle, oxygen sensor, plugs n.k.

Hakika atapata suluhu katika hayo.
 
Back
Top Bottom