Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

System ya umeme ina shida na prolly alternator. Vua hio kitu weka ingine utakuja kunishukuru. Najua laki na 80 inakuuma ila lipa hio hela weka alternator ingine. Umeme ukiwa hautoshi au unafuliwa chini ya kiwango ndio shida kama hizo hujitokeza provided battery sio chakavu.
Nibadilishe alternator?
Sasa 180,000 na January hii naitoa wapi mie?
 
Nikiwasha ac nitatembea baada ya muda gari itajizima, haitowaka mpaka battery icchajiwe.
Kuhusu battery nishaipima sehemu tofauti haina shida, why nikiwasha ac inajizima?
Kuna fundi alisema alibadilisha jino la altenator, na akasema alternator haina, mwingine akasema alternator haina shida.
kuna mmoja akabadilisha kifaa sikumbuki jina.

Hii ni mara nyingi mafundi washanilia hela sana.
Nimeipaki, siku ikinilazimu kutumia inabidi nisshushe vioo.
Nawaza mvua zikianza itakuwaje?
Maana mwenyewe kinanisave hatari kwenye mafuta.
Nikiwa na 10,000 nauhakika wa kwenda na kurudi.
Ila kuna jini hapa mpaka nitoke niwe na 30,000.
Upo wewe ndugu. Nimekumiss
 
Nibadilishe alternator?
Sasa 180,000 na January hii naitoa wapi mie?

Hahaaa basi tuuze gari ununue alternator[emoji23]

Hii imenitokea jana natoka kazini nawasha gari taa ya battery haizimi..hee nkajua tu hapa nshaua alternator

Nkamwita fundi kaja kweli issue alternator

Ikabidi ifunguliwe,bahati nzuri ikuwa ni brush na diode
So wakabadili chapu nkaondoka zangu kwa amaani[emoji2972]
 
Taa ya ABS inawaka na speedometer wakat mwingine haitembei. Gari ni Carina. Tatizo inaweza kuwa nini mkuu
 
Uskani kutetemeka inamaanisha magurudumu yako out of balance. Hii inatokea unapofunga tairi mpya au tairi zinapoanza kuisha tread. Dawa yake ni kwenda kufanya kitu kinaitwa wheel balance. Ukifanya wheel balance njoo utupe mrejesho. Tatizo litaisha kabisa.

Mafundi wengi hutengeneza magari kwa kubahatisha. Mf. Aliyekwambia kuwa mtetemeko wa uskani husababishwa na engine mounting, plugs, plug wire, alignment n.k siyo fundi huyo, atakuaribia gari. Kafanye wheel balance halafu rudi unishukuru.
Upo sahihi sana, kama kweli engine au plug kwann ikiwa imesimama haitetemeki kwanin mpak itembee ndio inatetemeka..? Hapo umesema kweli shida ni wheel balance ndio maana mim nlinunua tairi mpya dukan nkaweka shida ikaisha kabisa...
 
Uskani kutetemeka inamaanisha magurudumu yako out of balance. Hii inatokea unapofunga tairi mpya au tairi zinapoanza kuisha tread. Dawa yake ni kwenda kufanya kitu kinaitwa wheel balance. Ukifanya wheel balance njoo utupe mrejesho. Tatizo litaisha kabisa.

Mafundi wengi hutengeneza magari kwa kubahatisha. Mf. Aliyekwambia kuwa mtetemeko wa uskani husababishwa na engine mounting, plugs, plug wire, alignment n.k siyo fundi huyo, atakuaribia gari. Kafanye wheel balance halafu rudi unishukuru.
Wewe Mbute bora ukauke uwe bhutaga sasa. Gari ile inatetemeka ikiwa Silence ikianza kutembea inatulia tuliiiii unapiga hadi 160 safi. Tatizo ikisimama tu lazima utoe kwenye D uweke kwenye P au N ndio hutosikia mtetemo lkn ikiwa imesimama ikawa engaged kwenye D ni kasheshe
 
Nikiwasha ac nitatembea baada ya muda gari itajizima, haitowaka mpaka battery icchajiwe.
Kuhusu battery nishaipima sehemu tofauti haina shida, why nikiwasha ac inajizima?
Kuna fundi alisema alibadilisha jino la altenator, na akasema alternator haina, mwingine akasema alternator haina shida.
kuna mmoja akabadilisha kifaa sikumbuki jina.

Hii ni mara nyingi mafundi washanilia hela sana.
Nimeipaki, siku ikinilazimu kutumia inabidi nisshushe vioo.
Nawaza mvua zikianza itakuwaje?
Maana mwenyewe kinanisave hatari kwenye mafuta.
Nikiwa na 10,000 nauhakika wa kwenda na kurudi.
Ila kuna jini hapa mpaka nitoke niwe na 30,000.
Mafundi wengi WA Tanzania ni unga mwana wazee WA kuotea, Bora waganga WA kienyeji kuliko Mafundi gari WA Tanzania

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wewe Mbute bora ukauke uwe bhutaga sasa. Gari ile inatetemeka ikiwa Silence ikianza kutembea inatulia tuliiiii unapiga hadi 160 safi. Tatizo ikisimama tu lazima utoe kwenye D uweke kwenye P au N ndio hutosikia mtetemo lkn ikiwa imesimama ikawa engaged kwenye D ni kasheshe
Akijibu unistue

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo imewahi kunisumbua sana. Badilisha fuel pump utaniambia
Mimi ilinitokea, ila plug, zilikua zimekufa gari ikakosa nguvu, kugundua hili wala sikuhitaji fundi, fundi amehusika kutoa na kuweka plug mpya, baada hapo gari ilirudi kuwa mpya.
 
Uskani kutetemeka inamaanisha magurudumu yako out of balance. Hii inatokea unapofunga tairi mpya au tairi zinapoanza kuisha tread. Dawa yake ni kwenda kufanya kitu kinaitwa wheel balance. Ukifanya wheel balance njoo utupe mrejesho. Tatizo litaisha kabisa.

Mafundi wengi hutengeneza magari kwa kubahatisha. Mf. Aliyekwambia kuwa mtetemeko wa uskani husababishwa na engine mounting, plugs, plug wire, alignment n.k siyo fundi huyo, atakuaribia gari. Kafanye wheel balance halafu rudi unishukuru.
Nikiwasha gari ABS na taa ya handbreak inawaka muda wote,fundi aliniambia miguu ya mbele lazma itakua na hitilafu hapo ni baada ya kukagua switch,mafuta ya break,break pads kote fresh tairi mpya kabisa zina wiki 2, nikafungua miguu ya mbele ni kweli nilikuta Bering zimekufa nimebadilisha zote but shida ya taa ya ABS na handbreak kuwaka inaendelea fundi hana majibu anataka azizime kihuni nikamkatalia,nipe maujuzi boss,Ndinga ni Premio X.
 
Uskan kutetemeka.
Mara Engine Mounting ... hola.
Mara plugs ... hola.
Mara alignment .. hola.
Mara plug wire ... hola.
Kitu kipo bandani kimepaki.
Nilioatwa na hiyo shida, nilibadili vyote hivyo.., kumbe shida ringi ya piston moja wapo ilikuwa inapitisha oil, hivyo engine inatetemeka, ibabidi nibadilishe yote complete. Au la angalia kama tairi haijavimba, check na allignmemt
 
Nikiwasha gari ABS na taa ya handbreak inawaka muda wote,fundi aliniambia miguu ya mbele lazma itakua na hitilafu hapo ni baada ya kukagua switch,mafuta ya break,break pads kote fresh tairi mpya kabisa zina wiki 2, nikafungua miguu ya mbele ni kweli nilikuta Bering zimekufa nimebadilisha zote but shida ya taa ya ABS na handbreak kuwaka inaendelea fundi hana majibu anataka azizime kihuni nikamkatalia,nipe maujuzi boss,Ndinga ni Premio X.
Anti-locking Braking System (ABS) ni mfumo wa kuzui tairi zisiji-lock unapofunga breki ghalfla. Lengo ni kukuweza kulimudu gari hata kama wakati wa hatari. Taa ya ABS ikiwa on muda wote inamaanisha mfumo huu haufanyi kazi au una shida.

Taa ya handbrake kuwa on inaweza kuwa mafuta ya brake yamepungua
 
Back
Top Bottom