Siku gari yangu inaenda kupata ajali iliyo I write off iliniambia na mimi na upumbavu wangu sikuielewa ile lugha.
2010 tuko Brajeck tumemaliza kula na kunywa, mshikaji ananiambia twende tumpeleke msichana wake na rafiki yake Tegeta.
Naingia ndani ya gari, na engage gear, gari ikagoma kwenda. Baada ya dakika mbili likakubali, najiuliza hiki ni nini kimetokea?
Tukaenda Tegeta, tukawaacha wale warembo, tukiwa tunarudi tukagongwa na gari ingine, gari ikaharibika beyond repair.
Baada ya ajali ndipo nikaelewa, gari ilikuwa I anikataza nisiende kwenye hiyo safari.