Kwa mimi nimeshawahi kukatisha safari baada ya kuona hili gari hili sitoboi nalo Kigoma,safari lazima iishie njiani tu maana sio kwa ma mushkeli haya.
Nilipata mpenzi huko nyuma tukapendana vizuri tu,maisha yakawa yanaendelea Si unajua tena mnapokua wapenzi lazima kila mtu ajue ratiba za mwenzake hata kama hatupo pamoja ila akiulizwa sasa hivi
CONTROLA yuko wapi anajua cha kujibu kadhalika na kwangu.
Jumapili ni siku ya ibada yeye yupo kwao na mimi kwangu kila ikifika jpli mimi naenda zangu kanisani nikirudi namcheki mwenzangu namuuliza vipi za ibadani,ananijibu kua hakwenda,ukimuuliza kwanini anakwambia alikosa nguo, basi unauchuna.
ikifika jpli ijayo hivyo hivyo haendi sababu yake ni nguo/uchovu/kuumwa aseee nilimwambiaga ukweli mkavu kabisa ila bado tabia ikawa ile ile,Nguo za kutoka mitoko anazo kama 100 NA USHEEE ila za kanisani hana,ikikaribia jpili nguo zote Znachafuka.
Yule dada nilimpiga chini maana nilijihisi na date na PEPO maana hata tukiwa pamoja ukimwambia Ombea chakula "hataki" ukimlazimisha ataishia kuanza kula bila kuomba,nikaona isiwe kesi Nikaachia nafasi wengine.
Another one
alikua ni mpenzi wangu tulipendana haswaaa,siku 1 nilikua zangu nimekaaa nacheki Tv nikamuuliza "hivi una salio kwenye simu yako nataka kumtumia mama" akaniambia simu haina hata salio kuna 5000 tu",nikamwambia hiyo hiyo mtumie mama kwa vocha itamtosha sana akanijibu asee unawezaje mtumia mama sh.5000 ya vocha mwanaume mzima?
nikamuuliza swali "eti umeniulizaje??" akarudia swali lake "unamtumiaje mama 5000 ya vocha mwanaume mzima?" nikamwambia huo ndio uwezo wangu kuliko nisimpe hiyo 5000 akae bila vocha si bora nimtumie hiyo najua atajiunga vifurush kidogo kidogo na hatoitumia yote,ila yule mwanamke alinikatalia katu katu..
Akaniambia wewe mtumie mama hata 10,000 kidogo ita leta maana,nikamsisitiza siwezi tuma zaidi,akasema basi mwache akae hivyo hivyo au kakope hata kwa mtu umtumie,aseee tukiacha masihara yule dada nilimwambia live pale pale "naomba uondoke kwako niache kidogo" kweli akaondokaa
sikumtafuta tena na ndio ukawa mwisho wangu na yeye,ki ufupi nina list ya magari kadhaa niliyositisha nayo safari kutokana nakuona huko mbeleni hatutokuja kuwezana kabisaaa,so nikaamua tu kujiongeza.
SweetieLee Ulishawahi anzisha thread fulan hivi ya kumkinai "crushiee" wako sasa ile situation ebu fanya hakua just a crushie ila mliendelea hadi mkawa wapenzi then baada ya wiki mbili au mwezi unamkinai au inatokea tu kitu anakufanyia "kinakuchefua kabisaaa"....
Kuna dada nilimuuliza hili swali akaniambia yeye pia kashawahi muacha mtu,kisa ilikua kampenda jamaa vizuri jamaa alikua mtu mstarabu kupita maelezo ila hakuamini siku wanafanya mapenz jamaa akawa anasisitiza anataka TIGO asee yule dada akaniambia
CONTROLA nilimuangalia yule kaka juu mpk chini kisha nikainuka nikavaa nguo nikasepa,na ndio ikaawa mwisho wa mazoea na yule mkaka.
Haya na wewe tuambie ilikuaje ukamuacha ukasitisha safari
Note : sababu isiwe UGOMVI au mkwaruzano wa aina yeyote ile.