Umeshawahi kuachana na mpenzi wako kwa sababu umeona mahusiano yenu "hayatofika mbali" (hamjagombana kabisa)

Umeshawahi kuachana na mpenzi wako kwa sababu umeona mahusiano yenu "hayatofika mbali" (hamjagombana kabisa)

Wadada wengi wanaachwa sababu ya vizinga, wanaume wengi wanaachwa kwa sababu ya kutojali...
Vizinga, vizinga...dah! hapa nipo najiandaa kutema mzigo maana sio kwa mizinga hii, kibaya zaidi mimi huwa sisubiri aniombe ila sasa imefikia wakati kila nikiona msg yake najua ni mzinga! Pumbaf sana.
 
Umenikumbusha mbali pia my dear, iliwahi nikuta mkaka anachamba kama muimba taarabu na ana wivu sio mchezo siku moja alipiga bahati mbaya nikawa mbali na simu aliongeaaa, alitukanaaa alichonikera ni kunitukania mama angu nilijibu jibu moja tu nikamwambia hapa hujanioa ukinioa si utanitukania ukoo mzima?? Nilinyala kimya kimya mpaka leo
😂 😂 😂
Eti si utanitukania ukoo mzima??
Mwanaume akishakuwa na vijitabia vya 'uswahili' that's a turn off to me!
Unakuta mwanaume anachamba MwaJ ndalandefu anasubiri.!!
 
muda wa kujiburudisha huwa ni mchache

hamna anaependa kujiburudisha kwenye miili ya wadada kila leo

labda ziro aikyuuu ila wengine sisi tuna wish kama Lait angepatikana mmoja tu halafu tuendane Daaah

Amri 10 unaziona chache eee,ila usiombe kujaribu zifatisha kwenye matendo,unaeza jihisi uko JELA (Gwantanamooo)
Sasa kama umeamua kutozifuata si uachane na hizo habari uwe baridi kabisa kuliko kuwa vuguvugu
 
SweetieLee kumbe watu mna mapito yenu ya kimya kimya

pole sanaaaa

huyo jamaa ako wa kwanza sikua mimi kweli jamani

maana nimejirekebisha hata wiki sina,na hayo malamiko ndio yale yale yaniiii
Haha.!!
Me nahisi yangu yanajaza kitabu walaqhi.!!
Mie mwanaume mwenye maneno anipitie mbali sina hamu nao walaqhi'..!!
Pambana, utampata atakayevumilia mpaka tone la mwisho mwaya 'controller'..!!
 
Hahhaaa..!!
Mwanangu hiyo ya pili nayo ina kero zake usiombe mama! Usitumike, usipokee, uchelewe ku reply, uende mahali hujaaga utajuta kusema yes I do..! mambo ni mengi sana yanakera.!!
Bora wa 2 ntamvumilia.
Ila mwanaume mwema sabufa mdomoni hafai.
Halafu mbona Kama hizo sifa zote zinafuatanaga kwa mtu MMoja huyohuyo[emoji2]
 
Ugomvi wa kila saa, utabwaga manyanga mapema mno walaqhi'.!
Utabaki una act 'perfectinism' ili tu usimkwaze seriously??
Haki ya Nani,na ambavyo sipendagi tuhuma ambazo SI za kweli Wala SI za muhimu ..huyo mwanaume mbona atajichosha bure..atakapomaliza namjibu sawa/ndiyo.
Yeye: kwa hiyo ulifanya makusudi kukaa kimya/kuchelewa kupokea
Mimi:ndiyo
Yeye:unajidai unaosha vyombo masaa yote kumbe ulienda kwa wajinga wenzio eeh
Mimi: ndiyo
Yeye:Una kiburi siku hizi
Mimi:sawa

Sipendagi ujinga
 
Back
Top Bottom