Umeshawahi kuachana na mpenzi wako kwa sababu umeona mahusiano yenu "hayatofika mbali" (hamjagombana kabisa)

Umeshawahi kuachana na mpenzi wako kwa sababu umeona mahusiano yenu "hayatofika mbali" (hamjagombana kabisa)

Haki ya Nani,na ambavyo sipendagi tuhuma ambazo SI za kweli Wala SI za muhimu ..huyo mwanaume mbona atajichosha bure..atakapomaliza namjibu sawa/ndiyo.
Yeye: kwa hiyo ulifanya makusudi kukaa kimya/kuchelewa kupokea
Mimi:ndiyo
Yeye:unajidai unaosha vyombo masaa yote kumbe ulienda kwa wajinga wenzio eeh
Mimi: ndiyo
Yeye:Una kiburi siku hizi
Mimi:sawa

Sipendagi ujinga
😂 😂 😂 😂 😂
Kaah'.. Umenifurahisha mno walaqhi'
Nikipata furushi lingine I'll apply this one walaqhi..
 
Kwa mimi nimeshawahi kukatisha safari baada ya kuona hili gari hili sitoboi nalo Kigoma,safari lazima iishie njiani tu maana sio kwa ma mushkeli haya.

Nilipata mpenzi huko nyuma tukapendana vizuri tu,maisha yakawa yanaendelea Si unajua tena mnapokua wapenzi lazima kila mtu ajue ratiba za mwenzake hata kama hatupo pamoja ila akiulizwa sasa hivi CONTROLA yuko wapi anajua cha kujibu kadhalika na kwangu.

Jumapili ni siku ya ibada yeye yupo kwao na mimi kwangu kila ikifika jpli mimi naenda zangu kanisani nikirudi namcheki mwenzangu namuuliza vipi za ibadani,ananijibu kua hakwenda,ukimuuliza kwanini anakwambia alikosa nguo, basi unauchuna.

ikifika jpli ijayo hivyo hivyo haendi sababu yake ni nguo/uchovu/kuumwa aseee nilimwambiaga ukweli mkavu kabisa ila bado tabia ikawa ile ile,Nguo za kutoka mitoko anazo kama 100 NA USHEEE ila za kanisani hana,ikikaribia jpili nguo zote Znachafuka.

Yule dada nilimpiga chini maana nilijihisi na date na PEPO maana hata tukiwa pamoja ukimwambia Ombea chakula "hataki" ukimlazimisha ataishia kuanza kula bila kuomba,nikaona isiwe kesi Nikaachia nafasi wengine.

Another one

alikua ni mpenzi wangu tulipendana haswaaa,siku 1 nilikua zangu nimekaaa nacheki Tv nikamuuliza "hivi una salio kwenye simu yako nataka kumtumia mama" akaniambia simu haina hata salio kuna 5000 tu",nikamwambia hiyo hiyo mtumie mama kwa vocha itamtosha sana akanijibu asee unawezaje mtumia mama sh.5000 ya vocha mwanaume mzima?

nikamuuliza swali "eti umeniulizaje??" akarudia swali lake "unamtumiaje mama 5000 ya vocha mwanaume mzima?" nikamwambia huo ndio uwezo wangu kuliko nisimpe hiyo 5000 akae bila vocha si bora nimtumie hiyo najua atajiunga vifurush kidogo kidogo na hatoitumia yote,ila yule mwanamke alinikatalia katu katu..

Akaniambia wewe mtumie mama hata 10,000 kidogo ita leta maana,nikamsisitiza siwezi tuma zaidi,akasema basi mwache akae hivyo hivyo au kakope hata kwa mtu umtumie,aseee tukiacha masihara yule dada nilimwambia live pale pale "naomba uondoke kwako niache kidogo" kweli akaondokaa

sikumtafuta tena na ndio ukawa mwisho wangu na yeye,ki ufupi nina list ya magari kadhaa niliyositisha nayo safari kutokana nakuona huko mbeleni hatutokuja kuwezana kabisaaa,so nikaamua tu kujiongeza.

SweetieLee Ulishawahi anzisha thread fulan hivi ya kumkinai "crushiee" wako sasa ile situation ebu fanya hakua just a crushie ila mliendelea hadi mkawa wapenzi then baada ya wiki mbili au mwezi unamkinai au inatokea tu kitu anakufanyia "kinakuchefua kabisaaa"....

Kuna dada nilimuuliza hili swali akaniambia yeye pia kashawahi muacha mtu,kisa ilikua kampenda jamaa vizuri jamaa alikua mtu mstarabu kupita maelezo ila hakuamini siku wanafanya mapenz jamaa akawa anasisitiza anataka TIGO asee yule dada akaniambia CONTROLA nilimuangalia yule kaka juu mpk chini kisha nikainuka nikavaa nguo nikasepa,na ndio ikaawa mwisho wa mazoea na yule mkaka.

Haya na wewe tuambie ilikuaje ukamuacha ukasitisha safari

Note : sababu isiwe UGOMVI au mkwaruzano wa aina yeyote ile.
Nimewahi.
Alikuwa muislamu na ana mtoto tayari. Mwanzoni nilijipa moyo nitawezana ila kadri simu zinavyoenda nikawa naona hapana inaongezeka wigo.
Niliachana nae kimahusiano na hatuna ugomvi.
 
Kwahyo choice yake ila mfuko wako
IONIC dah
Kuna mmoja huyu Juzi Juzi nimeona niachane nae maana niliona Safari ya kuanzia Mtoni kwa azizi ally mpaka Mbagala Tu haiwezekani

Kisa kiko hivi beibe nimeichoka IPhone yangu 7+ nataka XR, nikamwambia Mfuko wangu unaweza ku Afford 8+ hiyo XR siwezi si kwamba sina ila siwezi weka bajeti huko kwenye mambo ya fashion na luxury ambazo Kimsingi hazina mwisho na kila siku zinatoka mpya

Majibu yake sasa ooooho hauwezi kunipangia choice unayotaka wewe mimi natumia brand ninayotaka Mimi, nikajisemea Dooh hapa gari haiwezi kufika Safari nikashuka njiani

Nb; Sikulalamika nikamuacha na Maisha yake, Jaribu kumbadilisha mwenzi wako ukiona haiwezekani Walk away Don’t kill yourself [emoji120]
 
Hehehehe dah
Nikishawahi kutongoza kidemu flani kizur zur cha mtaani kipindi hcho nasoma chuo siku hyo kikaniambia "yaan mimi sijawah kutongozwa na mwanachuo naona kama bahati" nilimshangaa sana anyway kuna siku natoka zangu chuo napita mtaani nakiona kimekumbatiwa na mshkaji flani kama teja teja hiv nikapita ye hakuniona. Kama dk 40 hv kikaja geto nikakauliza ulikumbatiwa na nani pale..?? Kakashtuka balaa palepale nikaenda kufungua mlango bila kuongea nikamuonesha njia ya kutoka toka apo sikuwah kupokea simu wala kujibu txt ya kile kimanzi na ndo ikawa mwisho wangu kutongoza videmu vya uswahilini na vilivyokimbia shule.
 
Mifumo yetu ya kiafrika inawafanya wanawake waendelee kua chini milele
Mtu hadi nauli anaomba at the same time anataka haki sawa kwa wote si maigizo haya
Yeah it’s the biggest challenge that most of us African Men facing, lucky you if you can understand

Na hata hayuko polite wala kutumia lugha yenye ushawishi as if she earned it,

nilikuwa na jamaa yangu kutoka Benin alikuwa na mwanamke wake from Russia ananisimulia

Anadai Binti wa kirussia alikuwa so independent inafika kipindi anafanya zake job anatafuta nauli lengo Tu akakutane na Mpenzi wake, and she was doing for love na jamaa akawa ananiambia yeye alikuwa anajihisi Fahari hata kumpa zawadi na kumfanyia mambo mengine out of love

Lakini mifumo yetu ya kiafrika baadhi ya wanawake ndiyo inawalemaza na kuwadidimiza shimoni kabisa.
 
Back
Top Bottom