Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?


Kweli kbs
 
Who am I ,swali zuri na umebana kotekote kwa kusema jina lako sio wewe,akina amina wapo wengi,huu ni uthibitisho kuwa hilo jina ni kibandiko tu na unaweza kubadili jina na ukabaki yuleyule,hili swali linaweza kukuchanganya lakini kuna viashiria vitakubainisha kuwa wewe ni nani
Kwanza wewe ni mtoto wa mtu fulani ,ambaye amejipa utambulisho na amepokea utambulisho mwingine wa babu yako na babu wa babu yako na kuendelea,hii inamaanisha utajitambua wewe ni nani kwa kuangalia umetoka familia na mizizi yake
Pili kwa kuangalia DNA yako,hapa duniani hakuna mwenye DNA zinazofanana,hata mapacha wana DNA zinazotofautiana,huu ni utambulisho tosha kuwa binadamu hatufanani na kila mtu ana nasaba/DNA yake.
Nini kingine kinachokutofautisha baina ya wewe na mimi?mahali na muda kwa kiingereza wanasema space and time,mahali nilipo mimi na mahali ulipo wewe ni tofauti hata kama wote tupo tabata na tunakaa nyumba moja,chumba kimoja,kitanda kimoja bado wewe utalala pemben yangu au juu yangu ila hatutaweza kuwa katika sehemu moja kwa asilimia 100,lazima tupishane space.kwa nadharia yako kusema kuwa sisi ni wamoja haina ukweli,tupo tofauti na hatuwez kuwa sawa hata siku moja,mazingira uliyokulia na mimi ni tofauti,mazingira uliyokulia yanaweza kukufanya uwe mtu wa hasira wakati mimi nimekulia mazigira tofauti ni mpole,kila mtu anapata tabia yake kulingana na makuzi aliyokulia na namna gani alivyofanikiwa kukabiliana na changamoto alizokutana nazo,kama alipokuwa mdogo akiwa ana hasira anafanikisha jambo lake basi tabia yake itakuwa hivyohivyo.
 
Mimi ni Mimi ,nilivyo Mimi nitabaki kuwa Mimi , nisipo Mimi sio Mimi na wala sio mimi
 
Mimi ni Mimi ,nilivyo Mimi nitabaki kuwa mimi , nisipo Mimi sio Mimi wala sio Mimi
 
Iam a Spiritual bro,covered by a body sorrounded by contextual..! daily living for preparing destiny that is my better place.!
 
Iam a Spiritual bro,covered by a body sorrounded by contextual..! daily living for preparing destiny that is my better place.!
 

Samahani sana kwa kuchelewa kuiona hii comment. Umejitahidi sana kujibu. Lakini mkuu hata hivyo ulivyovitaja navyo vinapita. DNA sio identity yako bali ni identity ya Mwili ulio nao sasa. Ukifa unaacha DNA zako kwenye mwili wako. DNA ni kama code ambayo inajitengeneza pale mbegu mbili zinapoungana na chembechembe zako zinakutana na kushuffle kutengeneza code mpya ambayo haitapishana sana na code za mbegu zilizoumba. Ndio maana unafanana na ndugu zako.

KUhusu space na time, space na time is an illusion. NI kama vile ilivyo kwenye matter. Matter is energy. Hivyo kila uonacho ni energy na sio matter kama unavyoona. Ukichunguza deep labda ka microscope nzuri utaona ni energy zinavibrate katika shapes tofauti na katika vibration tofauti kutengeneza reallity.

Ila ukitaka kujua wewe ni nani angali ndani yako. Usijidefine kwa vitu vinavyopita kama vile jinsia, muonekano, mawazo, maisha n.k kwani vyote hivi unaviacha hapahapa duniani.
 
mimi ni mimi hamna mtu kama mimi

Usijidanganye. Ndio maana unafundishwa usimtendee mwenzio usichopenda kutendewa, lengo kuu ni kuwa wewe ni mimi na mimi ni wewe. Ukinitendea mabaya umejitendea wewe na sio mimi. Life is an illusion. Wazo la kujiona wewe ni wewe ni jaribio la kupima akili yako. Ni kama vile mbwa anayeona mkia lakini hajui kuwa ni wake. Amka na uione dunia kwa undani, ina siri kubwa sana ndugu yangu.
 
Iam a Spiritual bro,covered by a body sorrounded by contextual..! daily living for preparing destiny that is my better place.!

Mwanadamu ni sehemu ya ulimwengu iliyojitambua. Ufahamu wako wa kuwa wewe upo na ndiye huyu ni tofauti kuu kati yako na viumbe vingine na ni tofauti kati yako na vitu ambavyo havina uhai. Lakini utambue kuwa kila kitu kinategemeana ulimwenguni. Unachokiexperience sio hakipo nje yako bali kipo ndani yako. NI sawa na kujitazama kwenye kioo bila kujua kuwa unayemuangalia ni wewe.

Wewe sio huo mwili, maisha yako na huo mwili ni mafupi sana kulinganisha na uwepo wako wa milele. Wangapi walikufa zamani na waliishi miaka mingapi na umepita muda gani? Mfano ukiishi miaka 90 katika body yako miaka itapita na miaka hiyo inapitwa kulinganisha na miaka ya uwepo wako wa milele.

Kujua wewe ni nani, usitumia ufahamu wa mwenzio anavyosema, kwani hujui naye amejua wapi kwani kila mwanadamu anaishi katika reality yake. Kujua wewe ni nani ondoa unachofundishwa ni jiangalie ndani yako, jichunguze kwa makini na hakikisha unapata jibu. JIbu lipo ndani yako.
 

Na tukishaviacha vyote hapa duniani sisi tunaenda wapi?
 
swali hili nilikuwa najiuliza zaman. na nilkuwa nabaki kujishangaa. lkn kwa sasa hata nikitafakar haitokei tena hali ile.
 
Fahamu kwanza wewe ni nani. Utapata majibu yote. Huwezi kujua unaenda wapi kama hujui wewe ni nani. Kwa sababu hutajua asili yako.

Kwahiyo njia ya kujua hayo yote ni kwa kujiuliza maswali kuhusu mimi? Maana mimi nikianza tu kujiuliza hayo maswali huwa mawazo Yanakuwa mengi sana.
 
Nawazaga sana hayo mawazo nikilewa " all in all mimi ni mimi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…