Who am I ,swali zuri na umebana kotekote kwa kusema jina lako sio wewe,akina amina wapo wengi,huu ni uthibitisho kuwa hilo jina ni kibandiko tu na unaweza kubadili jina na ukabaki yuleyule,hili swali linaweza kukuchanganya lakini kuna viashiria vitakubainisha kuwa wewe ni nani
Kwanza wewe ni mtoto wa mtu fulani ,ambaye amejipa utambulisho na amepokea utambulisho mwingine wa babu yako na babu wa babu yako na kuendelea,hii inamaanisha utajitambua wewe ni nani kwa kuangalia umetoka familia na mizizi yake
Pili kwa kuangalia DNA yako,hapa duniani hakuna mwenye DNA zinazofanana,hata mapacha wana DNA zinazotofautiana,huu ni utambulisho tosha kuwa binadamu hatufanani na kila mtu ana nasaba/DNA yake.
Nini kingine kinachokutofautisha baina ya wewe na mimi?mahali na muda kwa kiingereza wanasema space and time,mahali nilipo mimi na mahali ulipo wewe ni tofauti hata kama wote tupo tabata na tunakaa nyumba moja,chumba kimoja,kitanda kimoja bado wewe utalala pemben yangu au juu yangu ila hatutaweza kuwa katika sehemu moja kwa asilimia 100,lazima tupishane space.kwa nadharia yako kusema kuwa sisi ni wamoja haina ukweli,tupo tofauti na hatuwez kuwa sawa hata siku moja,mazingira uliyokulia na mimi ni tofauti,mazingira uliyokulia yanaweza kukufanya uwe mtu wa hasira wakati mimi nimekulia mazigira tofauti ni mpole,kila mtu anapata tabia yake kulingana na makuzi aliyokulia na namna gani alivyofanikiwa kukabiliana na changamoto alizokutana nazo,kama alipokuwa mdogo akiwa ana hasira anafanikisha jambo lake basi tabia yake itakuwa hivyohivyo.