Sasa mkubwa, ntawezaje kukuelezea mimi ni nani wakati hautaki maelezo?
[/CENTER]
Hili swali nilikua najiuliza sana kipindi nikiwa mdogo.Hasa nikikaa sehemu tulivu isiyo na kelele yoyote.Hadi nikawa najikuta najishangaa mwenyewe!
Lakini siku hizi kila nikijaribu nashindwa sijui kwanini!
Asante sana. Finally umeweza kuchambua kimoja kimoja na kutoa taka zote na kubakia na ambacho ni wewe. Ubarikiwe nawe pia. Asante sana.
the same to me...nahisi dhambi au mfumo wa maisha umeondosha hayaa
Nimesoma kichwa cha mada tu na nimeaumua kuanika utata nilioupata kabla sijaendelea kusoma zaidi....
Nikiwa mdogo wa miaka kama 9 au 10 nilijiuliza sana mi ni nani na kwanini? nilijitazama kwenye kioo kikubwa nikawa najiuliza maswali mengi juu yangu kwann nina jina, baba, mama, kwanini naweza kuwaza na kuongea moyoni bila kutoa sauti, nipoje, wengine wananionaje, ipo siku nitakufa na nitaenda wapi. Nilijiuliza sana ila sijui mawazo yale yalikuja potelea wapi ila Mungu mkubwa nilikuja kupata majibu hayo toka kwenye biblia. Nilijikuta kwenye mawazo hayo tena ktk usingizi wa nusu kaputi nilipofanyiwa upasuaji mdogo wa pua ila wakati huo nilijiuliza juu ya mungu na kwanini katuumba
dhambi hasa ya uzinzi na uasherati ndio chanzo
duh..kwa kweli inawezekana...
Hahaha huu uchambuzi inabidi uupandishe kule juu kwenye thread yako kwa ajili ya jamii pana ya JF. Fanya ku copy na kupaste then edit thread yako hapo juu utakuwa umepandisha huu uchambuzi!
Barikiwa sana!
Naomba kuendelea kuchokoza hii mada:
Nimebaini kuwa watu wengi mabilioni kwa mabilioni wana hali ya kutojifahamu wao ni nani. Hali hii ni tangu enzi na enzi. Je, ni kwanini hali hii?
cc: Apollo
Nimesoma kichwa cha mada tu na nimeaumua kuanika utata nilioupata kabla sijaendelea kusoma zaidi....
Nikiwa mdogo wa miaka kama 9 au 10 nilijiuliza sana mi ni nani na kwanini? nilijitazama kwenye kioo kikubwa nikawa najiuliza maswali mengi juu yangu kwann nina jina, baba, mama, kwanini naweza kuwaza na kuongea moyoni bila kutoa sauti, nipoje, wengine wananionaje, ipo siku nitakufa na nitaenda wapi. Nilijiuliza sana ila sijui mawazo yale yalikuja potelea wapi ila Mungu mkubwa nilikuja kupata majibu hayo toka kwenye biblia. Nilijikuta kwenye mawazo hayo tena ktk usingizi wa nusu kaputi nilipofanyiwa upasuaji mdogo wa pua ila wakati huo nilijiuliza juu ya mungu na kwanini katuumba
Swala la mungu ndio lina utata maana tangu nimepata akili sijalipatia jibu mpaka leo.
Swala la Mungu, kila dini ipo sahihi lakini ni sawa na kutazama anga na kuona mawingu na kusema kuwa anga ni mawingu. Utakuwa sahihi lakini kuna kitu ambacho ukikijua utaweza kufunguka zaidi na kutambua kuwa Sky is above clouds na clouds ni hali ndogo sana ya anga.
Same to God. Huwezi kujua ukweli bila kujitambua. Kila mwanadamu ana nature ya Mungu ndani yake ambayo inaweza kumuongoza na kukutana na Mungu ambaye ndio nature kuu.
Kwa kukusaidia sana ningependa kukushauri usome Easten Spirituality na kujifunza mtazamo wao kuhusu Mungu ni nani. Hasa Buddhism na Tao.
Ni kisa kizuri sana ambacho nami kimenigusa sana. Watu wengi sana waliowahi kujitambua na kupata majibu wamekuwa walimu wazuri sana wa kuelekeza watu.
Nimefurahi kuwa ni exerience ambayo umeitambua wewe, kwani kwa wanaoamini Biblia bila kuutafuta ukweli ndani yao nao bado hawajajua jibu. Nimefurahi kwani nawe umejiuliza na ukashuhudia mbali na kusoma kwenye BIblia tu.
Ubarikiwe sana.
amina, mtu anapojitambua huona kila kitu hapa dunian hakina thamani na hupuuzia mambo mengi ambayo wengine wanayaona ndo majibu ya ndoto zao pia hujikita ktk kile kilichowaleta dunian japo hukabiliwa na changamoto nyingi wengine wakistahimili wengine wakianguka kama ilivyokuwa kwangu baada ya kupata changamoto nyingi toka kwa ibilisi kupitia kwa wazazi wangu, marafiki, mazingira n.k ila naamini ipo siku nitarudi ktk mstari kabla ya kifo changu Mungu nijalie
Mimi na wewe sio kitu kimoja mkuu,hebu rekebisha hapo