Naomba kuendelea kuchokoza hii mada:
Nimebaini kuwa watu wengi mabilioni kwa mabilioni wana hali ya kutojifahamu wao ni nani. Hali hii ni tangu enzi na enzi. Je, ni kwanini hali hii?
cc:
Apollo
Asante kwa swali zuri sana.
Ni kwamba mwanadamu anasahau na jamii inavyozidi kwenda watu wanazidi kusahau kwani specialization zinaongezeka. Mtoto anazaliwa, anapelekwa shule, anaambiwa anasoma ili apate kazi nzuri, anatamani kupata kazi nzuri na anajitahidi kusoma na anafanikiwa, anapata kazi na kuanza stress za kazi, anakutana na changamoto za kazi, bado familia anaanza kufikiria jinsi ya kuiunda, anaoa, anaanza kujianda kujenga, kuandaa makazi ya maisha, anazeeka, na anasubiria kufa na mwishowe anakufa, lakini hajawahi kujiuliza ni kwanini yupo. Lengo la maisha ni nini? Kwanini yupo na anapaswa afanye nini?.
Tofauti na zamani ambapo unakuta mtoto anazaliwa, anakua, anakutana na mazingira na kujifunza mazingira, specialization ya watu haijapanuka na kunakuwa na specialization chache hivyo kuna kuwa na watu wengi wenye interest moja ya kujifunza siri za maisha ni nini.
Medias, utandawazi, na urahisi wa kushare informations umeongezeka hivyo ujinga unaweza kuongezeka na kusambaa kwa urahisi au busara inaweza kusambaa sana kwa faida hiyo pia. HIvyo jinsi tunavyozidi kuenda mtu akija kuuliza ni kwanini tunazaliwa, tunakua na mwishowe tunakufa ataonekana ni kama kichaa.
Lakini ukiwa mtafutaji, mwepesi kujifunza lolote utajikuta tu unakutana na signs ambazo zinaweza kukufanya ukaanza kujiuliza mengi.