Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I am the image of the invisible God and joint heir with Jesus Christ.[h=3]Asante.[/h]
Wewe ni nani?
Wewe sio kazi yako unayofanya, wewe sio kundi la watu unalojihusisha nalo.
Wewe sio mawazo yako,
Wewe sio Akili yako,
Wewe sio mwili wako,
Wewe sio mtu mwenye furaha, huzuni, hasira wala shida kama unavyojifahamu,
Wewe sio tafsiri uliyozoea kuifahamu.
Wewe ni nani?
Wewe sio ambaye wazazi wamekuambia,
Wewe sio ambaye marafiki wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye viongozi wa dini wamekuwa wakikuambia,
Wewe sio ambaye serikali imekuwa ikikuambia,
Wewe sio maelezo unayotumia kujielezea kuhusu wewe.
Achia mbali majina unayoitwa, maelezo unayojielezea kwenye mitandao kama Facebook au mitandao mingine ya kijamii.
Achia mbali jina lako, aina ya mtu unayejijua wewe ndiye, sifa ulizonazo, muonekano, asili, tamaduni yako au sifa ulizoandikiwa kwenye kitambulisho chako cha kazi au masomo,
Je unajisikiaje hivyo vyote ukiviachia mbali na kujiuliza wewe ni nani.
Nini kinabakia ukitoa mali zako, mwili, akili, shida, mawazo yako, imani yako, mazoea yako, tamaa zako, jina unalopewa na watu au unalojipa wewe, na sifa unazopewa na watu na sifa unazopewa wewe?
Wewe ni nani?
Kama wewe sio unachofanya,
Kama wewe sio unachofikiria,
Kama wewe sio unachopenda,
Kama wewe sio maelezo unayotumia kujitambulishia,
Je Wewe ni nani?
Tambua kwa kina...
Hauzuiliwi na mipaka ya mwili,
Wala wewe sio mapigo ya moyo wako,
Wewe sio Akili yako, mawazo yako na hisia zako,
Je kama wewe sio hivyo vyote je wewe ni nani?
Vuta pumzi taaratibu, hewa hiyo inaingia kwenye mapafu halafu inaingia kwenye kila seli ya mwili wako.
Funga macho, acha kuwaza, acha kuweka mawazo nje yako, hisi nafasi inayobakia iliyo kimya, na isiyo fikiria, waza, wala isiyokuwa na hisia yoyote kutoka kwenye milango ya ufahamu.
Kumbuka wewe ni nani, kumbuka hauna mipaka, mwili utakufa utauacha, jinsia yako nayo unaiacha, mali utakuwa nazo bali nazo utaziacha, hisia ulizonazo ambazo chanzo chake ni mwili wako nazo utaziacha mwilini, hasira na mawazo nayo yote utayaacha, sifa ulizopewa kama vile ulikuwa mchoraji bora au mwimbaji bora n.k nazo utaziacha kwani nazo zinategemea mwili mfano unaimba kwa kutumia mdomo lakini ukifa unauacha na huo mdomo na sifa zake ulizozizoea.
Je kama maisha yako ya hapa duniani yatakapoisha vyote hivi unaviacha...
Je wewe ni nani???
Wewe ni ufahamu unaofahamu vyote hivyo,
Jiangalie ndani yako kwa kina,
Wewe ni empty,hauna kitu
Wewe ni sehemu ya muumbaji,
Kila ukionacho, unachokiwaza, unachokitenda, na unachokizungumza kinawakilisha ulimwengu wa ndani yako.
Wewe na mimi ni kitu kimoja, wewe upo kama mimi na mimi nipo kama wewe.
Tunachopaswa kufanya katika safari ya maisha ni kujijua na kujitambua. . .
Samahani sana kwa kuchelewa kuiona hii comment. Umejitahidi sana kujibu. Lakini mkuu hata hivyo ulivyovitaja navyo vinapita. DNA sio identity yako bali ni identity ya Mwili ulio nao sasa. Ukifa unaacha DNA zako kwenye mwili wako. DNA ni kama code ambayo inajitengeneza pale mbegu mbili zinapoungana na chembechembe zako zinakutana na kushuffle kutengeneza code mpya ambayo haitapishana sana na code za mbegu zilizoumba. Ndio maana unafanana na ndugu zako.
KUhusu space na time, space na time is an illusion. NI kama vile ilivyo kwenye matter. Matter is energy. Hivyo kila uonacho ni energy na sio matter kama unavyoona. Ukichunguza deep labda ka microscope nzuri utaona ni energy zinavibrate katika shapes tofauti na katika vibration tofauti kutengeneza reallity.
Ila ukitaka kujua wewe ni nani angali ndani yako. Usijidefine kwa vitu vinavyopita kama vile jinsia, muonekano, mawazo, maisha n.k kwani vyote hivi unaviacha hapahapa duniani.
Kwahiyo njia ya kujua hayo yote ni kwa kujiuliza maswali kuhusu mimi? Maana mimi nikianza tu kujiuliza hayo maswali huwa mawazo Yanakuwa mengi sana.
Kuuliza maswali ni moja ya hatua. NI sawa na kuanza kuangalia ramani kabla ya safari. Kujiuliza ni kujua unatafuta nini na nini kimemiss katika majibu na utapata jibu wapi.
Wengi wanaogopa kuuliza kwani wanaogopa watakuwa wanakufuru, lakini sio kweli. Kuuliza si ujinga. Anayeuliza kwa lengo la kujua jibu ana akili na busara kuliko anayekubali kilakitu bila kuuliza, au asiyeuliza kabisa.
Mkuu, umejuaje kama huo ufahamu hatutauacha?
Nadhani bado hujajitambua, wewe ni wewe na mimi ni mimi,, wewe ndani yako mpo wa2 ukijumlisha na mwili mnakua watatu, mmojawapo akikosekana na wewe unapungukuiwa, huwezi kuangalia mwili wa ndan bila kuangalia na mwili wa nje, kama bado hujanielewa naomba nivitaje hivyo vi3 vinavyokukamilisha1 mwli wako, huu mwili utakufanya ufanye maamuzi kulingana na mahitaji yake mfano kula, kunywa, kufanya mapenzi, kukwepa moto 2.akili yako , hii nayo ina sehemu katika kukudefine wewe ni nani, 3.ni roho.mfano mzuri ili kujua kuna zaidi ya akili ndani ya mwili wako ni kutatizwa katika kufanya maamuzi ,halafu inabid uchague moja, ukitumia logic ina maana umetumia akili, ukitumia hisia hio ndio roho ingawa wengine wanatumia matumbo yao kufikir ambayo ni mwili
Hii ndio hali halisi, kimoja kati ya hivyo kikipungua huwez kua wewe.siku nyingine unapoenda deep kwenye meditation zako, kumbuka njaa
Nihitimishe kwa kusema DNA ni uthibitisho tosha binadamu hatufanani, na hata akili zetu hazifanani ndio maana hatufikiri kitu kimoja sawa, wote tunaweza kufikiria njaa ila namna tunavyofikia hitimisho ni tofauti, hata kiroho hatupo sawa , we unaweza ukawa na uelewa mkubwa kuliko mimi ama mimi nikawa na uelewa kuhusu mambo ya kiroho, hii inasababishwa na utofauti wa experience na ndio maana leo hii watu wawili apollo na mwananthropolojia wanatofautiana kwenye mada moja.we una dna yako, akili zako na roho yako kama na mm nilivyo na zangu.
Lipo ndani ya Biblia ambayo ndio Neno la Mungu.Asante kwa jibu lako zuri. Labda niulize, jibu hilo umelitafuta mwenyewe, umeambiwa, umesoma, umechunguza na kupata jibu au umepata wapi?
Look deeply within you, Ask your self "who am I?" Then every identity that come to the mind, observe it and criticize it if it have limitation of time and space. The whole concept is to eliminate all the negative identity we have learnt from the society, parents (who didn't spend time to find the truth), and to find our true identity that last and not taken by wordily end/death.
Lipo ndani ya Biblia ambayo ndio Neno la Mungu.
Ndio maana ninamsoma Kweli ambaye ni Yesu aliye hai. Hakuna zaidi ya Yesu ambaye ndie Kweli maana Neno la MUNGU linasema kuwa, mtaifahamu KWELI na KWELI itawaweka Huru.Asante. Ni vyema, pia usiache kuendelea kusoma neno la Mungu kwa kujifunza. Tafuta ukweli ulipo bila kujali umetoka wapi. Upime, Uchunguze, Chunguza mwelekezaji wa neno lake amelitoa wapi na je wewe unaweza kupata wapi majibu hayo kama yeye alivyopata.
Kila sekunde inavyoenda na miili yetu inachoka, na mwisho wa maisha yetu unazidi kukaribia. Tutumie kila muda na wakati kujitambua na kujifahamu zaidi.
Asante sana.
Kwahiyo njia ya kujua hayo yote ni kwa kujiuliza maswali kuhusu mimi? Maana mimi nikianza tu kujiuliza hayo maswali huwa mawazo Yanakuwa mengi sana.
kuna muda huwa najiuliza pia, matokeo take huwa naishia kukosa raha, sijui kwanini?!! Huwa sipendi hali hiyo initokee!!
Huu uzi ndio maana vilaza wasiopenda kutumia akili wanupiga madongo umekaa kimtego mtego na unamlazimisha msomaji kutumia milango ya faham kuutafuta ukweli ipo poa sana
Nimeipenda hii
tunasema kuna mwili ambao una sifa nyingi ambazo kwazo tunajipamba nazo na kujiona kupitia sifa hizo tunaweza kujitambulisha nazo mwandishi anasema mwili unapita
Ila naona amezahau kuwa ukuaji wa mwili hienda sawa na ukuaji wa ubongo (akili) kitu kinachopelekea binadam kujitambua na kuweza kuucontrol huo mwili na binadam kupata sfa mbalimbali mfano upole huzuni nk
Kuna roho ambayo naweza sema hii ni complex issue kuna wanosema ni consiousness ila huu ufaham ni wa kinamna gani ule unaotumiwa na mwili au kama wanavyosema ni software ya miili yetu ambayo ni hardware
Ndio maana kuna some time tunasema akili inaweza kubali kuwa kitu fulani ni muhim kukifanya mwili una nguvu kukifanya ila ukajihis uzito hata usiujue huo uzito unatokea wapi unaweza tenda kwa kujilazimisha au kuliacha kuhofia kujikera
Nahis tunapoamua kujitafutia ukweli who we are hatuwezi acha baadhi ya vitu vinavyo vinavyo tufanya tuwe tunafanya mambo tofauti na wengine
Yeah mada nimeipenda sana kuliko kawaida! Hadi nimetokwa machozi kwa jinsi nilivyofurahi! Nimesoma juzi na leo tena nimependa kurudia kuisoma!
Wewe ni: roho + mwili + nafsi kwa pamoja. Wala wewe sio huyo unaembiwa kuwa ni wewe!
Mwanadamu anakuwepo kwenye mwili na roho exactly at the same time. Kazi ya nafsi ni kuitafsiri lugha ya roho/mwili. Nafsi ni mtafisiri kwa maneno mengine ni mkalimani wa roho na mwili. Kama nafsi hakuna maana yake ni kuwepo mwili na roho hazitaweza kuelewana!
Ikumbukwe roho ana lugha yake na mwili una lugha yake. Ili zipate kuelewana mtafsiri anapaswa kuwepo naye ni nafsi. Huyu nafsi ndo ufahamu kwa maneno mengine, kumbuka kuwa kama huna ufahamu huwezi kutafsiri.
cc: Apollo na nifah
Hii mada imenibariki sana!