Umeshawahi kujutia kumsaidia mtu?

Mkuu umenikumbusha machungu binafsi niliwahi kumsaidia brother shukrani aliyo nipa iliniumiza mno,Nikamsaidia tena rafiki kwa Sasa nimejifunza bora kuwa na roho mbaya. Allah anisamehe.
 
Inawezekana biashara zao au mafanikio yao yana mikataba katika ulimwengu wa Roho.
Si rahisi hata kidogo kumuacha ndugu yako porini masaa ya saa nne za usiku wakati uwezo wa kumsaidia unao.
Lakini muhimu ni kwamba saidia tu, wewe saidia kwa namna yoyote ile unaweza kusaidia.
Usitegemee chochote kutoka kwa unae msaidia.
 
Lakini hata yeye anaweza Kukosa hela. Kwani mwalimu anakuwa na hela kilasiku?
Wengine Wana miradi ya Maendeleo akiipata tu anapeleka huko.
Usipokipata unacho kihitaji kwa mtu fulani, usifikirie moja kwa moja kuwa umenyimwa.
Wanakuwa hawana wakati mwingine.
 
pole sana bwana ndugu, huwa wanasema ukitoa toa bila kukumbuka na ukipokea pokea bila kusahau.
 
Wakati fulani nilikuwa Sina hela kabisaa. Kukawa na rafiki yangu nilimkopesha hela siku za nyuma, akawa hakulipa hela yangu.
Mie nikakausha.
Wakati huo Sasa amepata shida tena anataka nimsaidie na Mimi hela Sina.
Nikamwambia siko vizuri, lakini huyu ndugu yangu aliendelea kunisumbua kila Mara anataka hela wakati ukweli Sina.
Lakini akilini mwake anajua hela ninayo, sitaki kumpa kwasababu mwanzo hakurudisha wakati sivyo.
Na Kama ningekuwa na hela ningempa Mimi sijali.
Nikiwa nacho natoa tu, Kama msaada na Kama mkopo. Ukidhulumu nashukuru.
 
sijuti maana nilifanya nililoweza. nimeshawahi kumkopesha mtu pesa ambayo niliikopa kwa mtu mwingine ili tu nimsaidie kutokana na kushibana kwetu. Cha ajabu mimi nilimaliza mkopo wangu kwa mtu mwingine lakini yeye alinilipa theluthi tu na hapo anaishi good life kinyama huku mimi nakaa kishida tu. Halafu hata hashtuki ila sijutii maana kashajipa termination na somo gumu kanipa. Sasa hivi ninakupa ninachoweza kutoa, sijitoi mbuzi wa kafara tena
 
Mi nilimsaidia jamaa gari akaenda nalo kijijini kwao kaenda kutangaza ni lake siku amerudisha nikwa napita nalo njiani nasikia baadhi ya waliomuona nalo wananiuliza naona nanii kakuuzia gari yaani nilichoka ghafla
 
Dah kaka inawezekana lakini unafanya hivyo kwa ndugu zako hadi kwa mama mzazi aliyekuzaa(Mungu amrehemu shangazi)...Mwaka 2012 baba mdogo aliumwa sana wakati anaumwa akasema kabisa iwapo atakufa basi Likologeka(huyo mkuda) akitoa gari na tukizipokea hatutafika salama maana ameshindwa kumsaidia matibabu akiwa hai japo walimtaka sana msaada,,,,alipokufa ni kweli alitoa fuso 2 kitu cha ajabu hazikuwaka zile gari ikabidi zikakodiwe zingine msiba ulipoishi gari nzima.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mi nilimsaidia jamaa gari akaenda nalo kijijini kwao kaenda kutangaza ni lake siku amerudisha nikwa napita nalo njiani nasikia baadhi ya waliomuona nalo wananiuliza naona nanii kakuuzia gari yaani nilichoka ghafla
 
Kuna wanoua Mama na Baba zao mpaka na wadogo zao karibu wote kwa mikataba ya aina hiyo, inategemea masharti.
Sasa jijui jepesi ni lipi.
 
Pole sana
 
Exactl exactly full exactly mkuu inakatisha tamaa sana hasa akiwa ndo pekee unaemtegemea

Kwa kipindi hki kigumu nachopitia sifahamu kama roho ya upendo na huruma kama itaendelea kuwapo
 
Mkuu wote hao mzazi wao n MMAKONDE
 
Amina umeongea jambo la msingi sana mkuu
 
Tunapofeli ni pale tunapowasaidia watu na kutegemea kupokea sawsawa, zaidi au Pungufu ya misaada tunayotoa.
Huu ni mtazamo wa ajabu Sana, Binafsi sijawahi kuwa na mtazamo wa namna hii.
Fikiri kidogo juu ya ma Global wanaokuja kutoa misaada mbalimbali huku kwetu Kama wangekuwa mitazamo ya aina hiyo.
Ingetoka hela kweli ukizingatia jamii ambazo hawa watu huenda kutoa misaada?
Ukiwa na uwezo wa kumsaidia mtu fanya hivo.
Sijui mnajifunza kutoka wapi kutoa kunakotazamia kupokea.
Msaada ni tofauti na Mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…