Watu kama hao wasiokumbuka walipotoka mwisho wao huwa mbaya sana...Sasa Si afadhali huyo kaka,,,Ngoja nikupe stori wengine watajifunza mimi baba yangu alimlea mtoto wa dada ake tangu akiwa ana umri wa miaka 5 mpaka anapata mke,,ni yeye ndiye alimfundisha biashara za sokoni na pia alimpata mtaji baada ya kuzoea akawa anapiga kazi lakini kulala na kula home.
Mungu akamsaidia akatoboa ikafikia jamaa anamiliki magari Daladala zaidi ya 10+ maroli na maduka acha nyumba za kuishi...ila huyo jamaa kwake hataki hata ndugu hata akikuta njiani hata kusaidia hata kwa lift tu salamau hadi umuanze wewe.Alikua yuko radhi ambipu mzee kuliko kumpigia ajabu sana mtu mwenye biashara za maana alikuwa anabipu ili aonekane hana kitu.
Mzee hata kama aliomba laki akopeshwe hatapata hata aombeje,Mwaka 2014 bro wangu alikua anatoka Tunduru na gari ndogo alipofika sehenu moja katikati ya muhoro na somanga gari ikaharibika na pale ni pori kwa bahati akaona fuso inakuja akasimamisha aimbe msaada wa kuvutwa ikasimama,,dereva wa fuso akawa ameshuka amsaidie akakubali kumvuta ila akamwambia ngoja amwambie boss maana yupo nae basi kunwambia aah kumbe ndo jamaa bro akajua kwa sababu ni mtoto wa shangazi mambo yangekuwa poa lakini jamaa alikataa katakata na kusema gari imebeba mzigo mzito hawezi kumvuta mpaka dereva alishangaa baada ya kujua wale ndugu lakini boss analeta ukuda usiku wa saa 4 kumuacha ndugu yake porini.
Bro aliporudi home akamwambia baba kuwa kuanzia leo hana undugu na yule jamaa,maana si binadamu.Jamaa mama alipokuwa anaenda kwake mara nyingi alishindwa kukaa kwa tuhuma za uchawi,siku moja mjukuu wake aliwahi kulalamika kuwa ameibiwa chupi na mjukuu wake Hiyo siku shangazi alilia sana akaondoka n kuaapa hatarudi kwa mtoto wake tena,,,japo walikuja kupatanishwa lakini still maelewano hayakuwa mazuri.
Nifupishe stori,mwaka juzi shangazi alikufa ninavyozungumza sasa yule jamaa amefirisika sana amepoteza karibu 50% ya utajiri wake na hata rafiki zake waliwahi kunfuata mzee kumwambia afanye namba amsaidie mjomba wake anapoelekea ni kubaya.
Kwa hiyo kaka usisikitie kuna watu wana roho mbaya sana na mwisho wao huwa mbaya.