Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

safi sana uliwakomesha mbwa wale
 
Watu Kama nyie acha nikuite mbinafsi unaroho mbaya sana inakuaje unasahau majukumu yako tambua hapo ulipo sio kwa sababu yako upo kwa ajili ya watu na ipo siku utaondoka hapo
 
Watu Kama nyie acha nikuite mbinafsi unaroho mbaya sana inakuaje unasahau majukumu yako tambua hapo ulipo sio kwa sababu yako upo kwa ajili ya watu na ipo siku utaondoka hapo
Hujaelewa.

Pia waweza ita utakavyo. Ni juu yako.

MF. Umeleta bahasha yako napokea inapotakiwa kufika wenyewe hawapo. Inanibidi niweke kwa droo, mambo mengi mtu unajikuta umesahau utakuja ona wakati mwingine. ..

Usahaulifu upo, najua unajua.

Kitu kingine msichokijua, Inapopelekwa kwa HR, MD, AD ye HAISOMIIIII anakwambia tu file sehemu husika. Imeisha hiyooo. Kukiwa na uhitaji wa watu flani ndio file inafunguliwa na barua zasomwa kutafuta nani kakidhi vigezo.

Ushauri. Mnapopeleka bahasha omba kumuona mwenyewe muhusika., me kams wahusika wapo uwa napanda kuwaambia kuna mgeni wako. Siku nyingine ye tu anakwambia sina appointment na mtu, sihitaji mgeni yeyote. Kwahiyo wakija inabidi tu uwaambia muhusika hayupo.
 
Salaam wakuu! Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, katika mihangaiko yako ya maisha ya kila siku, umewahi kwenda sehemu kupata huduma fulani na ukaletewa nyodo na mhudumu husika, kwa sababu tu aidha mmiliki ni mpenzi wake, au vyovyote?

Karibuni!
Mi nilimtukana nikasepa
 
Muhudumu mmoja toroka uje kimara aliniletea nyodo, nilifika zangu pale mida kama ya saa kumi jioni, nikaenda kukaa hatua kama tatu na alipokuwa amesimama, nilikuwa nimechafuka balaa huku nimevaa ndala na kaptula. nilipita pale nipate bia za baradiii ndo niende home nikijua kwa nilivyochoka na ni juma pili nikifika home lazima nilale.

Binti hakuja kunihudumia, nikamuita hakuja na ananiangalia macho makavu, akapita muhudumu mwingine nikamwita akanihuhudumia, nikapiga windhoek zangu tano nikawa nimetosheka, wakati huo aliyenihudumia na yule kilaza mpya wakawa counter nikaenda pale pale, yule muhudumu akaniambia nadaiwa 15,000 nikatoa wekundu wawili nikampa nakumuambia chenji utakunywa maji, yaani yule kilaza aliyenifanyia nyodo alishtuka mpaka macho yakatanuka hakuamini kuona makusudi niliyomfanyia.

baada ya siku kadhaa, nikaenda kez pub, jumapili kucheki mechi mchana kama saa nane, nikakaa zangu counter, kufika mida ya saa kumi mechi ikaisha wadau wakapungua, mara kaja muhudumu mkali sana ananisalimia huku anajichekesha, maaambo!!!! mi nikamjibu short tu huku nashangaa huyu vipi mbona ananishobokea, kakomaa "inamaana umenisahau" mimi no, samahani sikumbuki tumeonanana wapi.

ikibidi anaieleze namna tulivyokutana toroka uje, na yaliyojiri, lakini hakusema juu ya keep change ya 5,000. nikamkumbuka, sasa kwa namna alivyokuwa mkali ikabidi nimchangamkie fasta na kumkaribisha hoo mimi hapa ndo sebureni kwangu, karibu sana na nini na nini, ghafla tu nikasikia yule dada wa counter anasema "hey hey hey nyie mnapitiliza sasa" huku amesimama still mikono kiuononi na , anatuangalia kwa jicho la hasira sana,ikabidi niache hizo story haraka sana na yule binti akajua amevuka red line akaondoka fasta.
 
Na wewe palikuwa na haja gani ya kusema ulipita na crown? Okee ilikuwa ni C. Athlete, Royal Saloon au Majesta?
ATHLETE...nikiwa na hela inatosha ntanunua Mustang ya 2011...maisha ndio haya haya...na nlisema crown sababu kulikuwa na vx za serikali so aliona kama me nipo kwenye gari chafu chafu mbuzi yule....mkuu ni kosa kusema crown ?

Na wewe palikuwa na haja gani ya kusema ulipita na crown? Okee ilikuwa ni C. Athlete, Royal Saloon au Majesta?
 
tatizo la madada wengi kwenye customer care na utoaji wa huduma huko maofisini ni namna walivyozipata hizo kazi... kwa binadamu aliyefuata taratibu za ajira na kupata ajira kwa haki hawezi kudharau mtu yeyote....
sahihi kabisa mkuu. wengi wenye nyodo wanajiona kama wana-godfather wao
 
tatizo la madada wengi kwenye customer care na utoaji wa huduma huko maofisini ni namna walivyozipata hizo kazi... kwa binadamu aliyefuata taratibu za ajira na kupata ajira kwa haki hawezi kudharau mtu yeyote....

Kuna ukweli sana kwny hili.
 
MWECAU umewasingizia tu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…