Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Kuna bar moja nikwenda. Kufika tu akajipendekeza bar maid mmoja kuja kunihudumia. Basi nikamwambia akaniletee supu ya kuku jikoni na yeye achukue yake. Dakika tano nyingi supu hizi hapa. Huku nnaendelea kusoma gazeti na kunywa supu. Nikamwambia aniletee castle baridi na yeye achukue yake. Dakika nyingi beer ziko mezani. Nikaagiza castle ya pili na yeye nikamwambia achukue yake. Baadae kidogo nikaomba bili nilipe niondoke. Kabla sijawasha gari namuona huyu ananikimbilia na kuniambia. Kaka umesahau kuchukua namba yangu......
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Vihudumu vya bank hasa visichana vinakuaga na dharau sana. Mimi sehemu ninayokua mpole ni hospital na polisi tena kama ninayemfahamu hayupo. Sehemu nyingine moto nauwasha saa yoyote
[/QUOTE
Mkuu mi hata hao wakinizingua wajipange kichwani
 
sijamzingatia mkuu maana kulikuwa na kagiza ka asubuhi ila nahisi atakuwa yy nilimpelekea moto karbia kumpga makofi dogo akanishika nadhani akirudi atamwambia jinsi nilivyo maana yule dogo nahisi wanamfaham

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo Hilo Kuna siku tulikuwa na brother tunahitaji mafuta linaleta mashauzi nikampigia Meneja kumbe Meneja ni ndugu yake yaani anamwita baba mkubwa, jamaa alipofika akamfokea sana lakini bado Kuna matatizo
 
mimi nimekiwasha leo nimeamka asbh nakuta mtoto kachemka kwenye mida ya saa 11 asubuhi hivi ikabidi nimkimbize hosptal ya makole, kwenda kuwasha gari nikakuta haiwaki betri limezima, ikabidi nuimtafte dereva wangu wa bajaji ile asubuhi chap akaja akatupakia na dogo kutukimbiza hospital agakani tumefika SHELI YA PUMA iliyopo oposite na JENGO LA TANESCO jirani kidogo na ofisi za yadi ya jiji la Dodoma dogo kaingia sheli cha ajabu mwanamke mmoja mhudum anatuanfgalia kama boss alafu anatufokea kwa kweli mungu anisamehe nilitoka bila dogo ningemwasha vibao yaani yule mjinga anatuvimbia na ni kazi inayompa ugali>?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo Yule mzee ambae sijui ndo meneja kawajaza wanafamilia pale hivyo wengine hawajali Wateja
 
Kuna bar moja nikwenda. Kufika tu akajipendekeza bar maid mmoja kuja kunihudumia. Basi nikamwambia akaniletee supu ya kuku jikoni na yeye achukue yake. Dakika tano nyingi supu hizi hapa. Huku nnaendelea kusoma gazeti na kunywa supu. Nikamwambia aniletee castle baridi na yeye achukue yake. Dakika nyingi beer ziko mezani. Nikaagiza castle ya pili na yeye nikamwambia achukue yake. Baadae kidogo nikaomba bili nilipe niondoke. Kabla sijawasha gari namuona huyu ananikimbilia na kuniambia. Kaka umesahau kuchukua namba yangu......
We jamaa ni pimbi sana ila tu haujui
 
Mkuu ukiweka uzi, bas jarib kutupa maelezo kuhusu hyo story, tupe pa kuanzia na sisi wachangiaji. Kutupa tuu tiltle ya uzi bila kutupa maelezo yako kama ilitokutokea ww au jamaa yake wa karib haionog kabisaa
 
Dah mimi leo nimeenda banda la Mpesa natuma hela, namsalimia huyo dada haitikii afu kakaa ananiangalia kidharau, nikaanza kupaza sauti nimekusalimia unamaanisha hujasikia ama? Eti kinabinua mdomo, karibu, nikamuuliza nataka kutuma pesa kiasi fulani eti ndiyo kamenuna kabisa hadi ikabidi nihudumiwe na kaka mwingine waliekua wote hapo ofisini.

Mwingine mkoani huko tena mbaba, nilikua naulizia mifuko fulani hivi ya kuvunia mpunga, huwa inatofautiana size, nikamuuliza ipo akajibu ipo na bei akasema, eti namuambia naomba niione size yake hee akanijibu vibaya 'nimekwambia mifuko ipo huniamini ama? Duh namimi nikapata hasira nikamwambia basi acha tu si wewe peke yako unayeiuza bana. Nikaenda next duka akiwa ananiona huyo akanionesha ilivo hiyo mifuko na akaikunjua kabisa nikaridhika nikanunua tena mingi tu. Nikaona ananicheki nikajisemea nimekukomesha.
 
Miaka hiyo,nilipeleka maombi ya kazi sehemu,mama wa makamo ndiye alikuwa mapokezi,akaichukua bahasha yangu na kuitupa pembeni kwa dharau,nikaondoka nikisononeka....nikaitwa kwa usaili,na kupata ajira pale,yule mama akaondolewa kule mapokezi akawa muhudumu na kutuhudumia chai,....basi siku moja nikamkumbusha,alijisikia vibaya na kuanza kuniogopa na kunikwepa...lakini baadae tuliyamaliza angekuwa binti ningemtafuna tu aisee.
Sasa uliitwaje kwenye interview wakati unasema bahasha aliitupa pembeni kwa dharau?
 
Mara kibao tu, ila unaishia kuwaacha na maisha yao siku moja watajifunza heshima.

Kuna mmoja huyo alikuwa demu wa rafiki yangu, tumekutana fresh tumesalimiana na mshikaji yeye akawa kimya nkamsalimia akajibu kama hataki vile, haikuwa ishu kwangu.

Mara jamaa akamwambia huyu ndio yule jamaa nilikuambia nitaku connect naye ufanye intern firm yao, ndio demu akajichangamsha na kuita ita shemu.
 
Enzi hizo za ujana wangu, kuna kipindi nilipeleka maombi ya kazi PPF, kuna mama wa makamo mapokezi aliniambia niweke bahasha langu tu mezani yamefika.

Kuondoka nikawa tu na wasi wasi sijasaini popote kuwa nimeyafikisha maombi yangu salama nikarudi lile bahasha halikuwepo mezani kuangalia vizuri niliona tu bahasha la kaki limewekwa kwenye dustbin zile nyeupe na linafanania na langu 100%(kuna mikunjo kabisa ya ile bahasha nilikuwa naiona).

Nikazuga kwa upole kuna sehemu juu sijaandika vizuri anuwani ili anipe nifanye marekebisho ili nione kama ndio hilo alilolitupa akakataa, niliwaka aisee nataka nionyeshwe bahasha yangu au anaona aibu kwa kuwa ameitupa, mwisho wa siku kuna braza mmoja na suti yake aliita mlinzi mmoja nikatupwa nje, sikuitwa hata interview😡
Daaah watu wana roho mbaya dunia hii, hv inakuaje unamfanyia mwenzako roho mbaya kiasi hicho jaman, daaah pole bro, mm naamini MUNGU ndio mgawa ridhiki, na sikuzote MUNGU mwema, we endelea kuamini katika ahadi za MUNGU cha muhimu uvumilivu tuu
 
Kwa roho yangu ilivyo mtu asinifanyie ubaya utakaoniumiza. Maana nikilipa kisasi nakifanya vibaya.
Eg. Kuna nesi sehemu flani ana mdomo anafokea sana wajawazito, mimi nikaenda pale kupigwa sindano akanifokea pia maana alinihudumia yeye. Juzi nimemrudia niliplan nimdunge sindano ya shavuni
 
Back
Top Bottom