Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Umeshawahi kuletewa nyodo na mhudumu wa kike?

Kuna bar moja nikwenda. Kufika tu akajipendekeza bar maid mmoja kuja kunihudumia. Basi nikamwambia akaniletee supu ya kuku jikoni na yeye achukue yake. Dakika tano nyingi supu hizi hapa. Huku nnaendelea kusoma gazeti na kunywa supu. Nikamwambia aniletee castle baridi na yeye achukue yake. Dakika nyingi beer ziko mezani. Nikaagiza castle ya pili na yeye nikamwambia achukue yake. Baadae kidogo nikaomba bili nilipe niondoke. Kabla sijawasha gari namuona huyu ananikimbilia na kuniambia. Kaka umesahau kuchukua namba yangu......
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Enzi hizo nakunywa safari beer baridi nilikua na rafiki yangu tajiri wa mabasi ya mikoani, lkn huyu jamaa vaa yake usingejua kwamba Ni tajiri. Tulikwenda bar moja Ina wahudumu wawili, jamaa akamtaka mmoja white lkn white akajifanya matawi. Basi jamaa akamjaribisha yule sura mbaya na sura mbaya akakubali.
Jamaa yangu kila siku Basi likitoka mikoani lzm lije na Michele, samaki, ndizi, kuku ndio usiseme. Baadae akaamua kuoa kabisa.
Tukamwacha white na uzuri wake akiendelea kuuza bar.
Hahahahaaa!dahh!yaani usidharau usiemjua!!!
 
Ngoja nishee habari Moja kuhusu ma secretary wenye nyodo mwaka ya 98 nilikuwa na mgogoro wa ardhi na mtumishi mmoja wa umma akiwa Ni afisa ardhi.Baada ya suala kuwa halishughulikiwi nikaamua kwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa kupata msaada nilikuwa na miaka16 kipindi hicho.
Sasa nilipofika kwa katibu muhutasi huyo ili kupata ruhusa akanikatalia eti nimwambie shida yangu halafu akamwambie bosi wake akikubali ndo ataniruhusu, Katibu muhutasi akaniuliza kwa ukali "UNATAKA NINI NAWEWE KIBWENGO" Nikamjibu NIMEKUJA kuongea na Baba kwani Mimi hunijui? Basi akajifanya kunijua akaniruhusu nikaingia.
Muda kidogo akaniletea chai nzitoooo. Mkuu wake akashikwa na butwaa.alipotoka Yule muhutasi nikamueleza Miuu Yule shida yangu Mambo yakaenda sawa.nkatoka na kumuaga.INA MAANA NISINGE MDANGANYA NISINGE WEZA KUFIKISHA UJUMBE WANGU KWA MKUU WA MKOA NA HUWENDA TATIZO LISINGEPATIWA UFUMBUZI
What a perfect movie...!!!hahaha
 
Kairuki hospital dada wa mapokezi namuongelesha ananipuuza huku anapiga stori na mwezake .

Moto niliomuwashi hatukuja sahau

Wabongo customer care tuko shallow Sana .

Ukishashiba mshahara unaanza fanya kazi kwa mazoea .

Mi sikukopeshi nakulipa hapo hapo
Upo sahihi mkuu. Majirani zetu wakenya wametuzidi kwenye customer care.. Hii kitu hata marehemu Sitta akiwa waziri wa wizara ya afrika mashariki aliwasifu wakenya bungeni.
 
Vihudumu vya bank hasa visichana vinakuaga na dharau sana. Mimi sehemu ninayokua mpole ni hospital na polisi tena kama ninayemfahamu hayupo. Sehemu nyingine moto nauwasha saa yoyote
Vipi wanavyowahudumia nyie wanawake wenzao? Nadhani bora ya sisi wanaume
 
Bora wanaume jamani wengii wana customer care nzuri. hata kwenye restaurants nyingi visichana vidomo juu juu. Mimi sipendi dharau ukiangalia vijicent vyangu vinahusika kwenye kukulipa mshahara
Ata wamama nao ni tatizo
 
Daah nakumbuka mkonge hotel nilikua na appointment na don flan sasa kufika nikaagiza soda sa sijui wale ma maid waliona mm mchovu ukizingatia ulikua msimu wa uefa wakajua navizia mpira
Tu.. basi nikamuita muhudum ili nimuulize issue za pale kama kuna live band we aliniangalia kwa nyodo nikamuiliza vp mbona unaniangalia kwa dharau akasema we sema unashida gani nikamwambia bas nenda..akaondoka kwa dharau.. kodgo yule don akaingia alikua mshkaj wa marehem mshua wangu so ali ni treat kama mtoto wake na alikuja nipa dili zito..alipo ingia akawaambia wale maid nyie mmemsikiliza huyu bosi huku akianza kutaja tittle yangu kisha jina..wakajiuliza huyu dogo nani mpk doni anamuita bosi..?nikaambiwa agiza menu nikaagiza menu ya maana baada ya maongezi mzee akasepa akaniachia kama 200k za kazi aliyo nituma.. baada ya mzee kuondoka Ndo nikaanza kuona mhaho wa hao ma maid nikawaona [emoji90][emoji90] nikaagiza maji makubwa nikanywa nusu glas nikaacha na kusepa..thats why kwenye kazi zangu huwa sibagui naelewa ubaya wa kubagua usie mjua..nishamsadia mtu wa kawaida sana wkt anaondoka akasema kaka anataka akushukuru alivyo nipa simu kuongea na kaka yake hahahaha nikasema dharau hazifai maana alikua mzee wa jengo jeupe na ni mkubwa tu..the rest ikabaki story…USIDHARAU WATU ENEO LA KAZI YAKO
 
Mimi ilinikuta, muhudumu wa hotel alinionesha dharau,
Nikamchunia siku hiyo, nikapanga kukipiza,
Nikamtongoza na nikahakikisha amedata nami nikala mzigo halafu nikapiga chini!
Na nikamchana ukweli, nilikuwa nakuonyesha mie ni zaidi yako!
Mpaka leo mnyonge!
Huyo alikuwa hakudharau.. alikuelewa akajikuta ana play hard to get.
Hao design hiyo ukiwauliza kitu anakujibu akiwa overconfidence unaweza hisi ni dharau.. kumbe sio..
Dem akisha kudharau kuna kazi kubwa sana kugain respect na kumattract tena
 
Nilipiga simu nmb nilikuwa na shida fulani kuhusu AC yangu , kapokea customer care Representative ni mwanaume, kila swali nililokuwa namuuliza jamaa ananijibu shortcuts tu yale majibu ambayo mtu anaona "unampotezea muda".. kabla hajakata simu nilimuwashia moto sana nilichukia..

Kesho yake nikapigiwa simu na boss wake na kuniomba radhi -- sasa sijui yeye huko alikuwa kwenye hali gani!
 
ndio ccbrt hospital ness pale kwenye kupata risiti baada ya malipo ukamuone dr hataki umuulize mara mbili hata kama hujasikia na ubaya kavaa barakoa sauti haitoki wanaudhi sana 3/9/21
Ccbrt hawana nyodo boss tena kuna vipaza sauti kabisa kazi yako ni kusikiliza tu.
 
Huyo alikuwa hakudharau.. alikuelewa akajikuta ana play hard to get.
Hao design hiyo ukiwauliza kitu anakujibu akiwa overconfidence unaweza hisi ni dharau.. kumbe sio..
Dem akisha kudharau kuna kazi kubwa sana kugain respect na kumattract tena
"play hard to get" inaingiaje hapo mkuu 6Was9 wakati jamaa Fmruma amekwenda kama mteja tu ila mhudumu akamuona mshikaji kama mlalahoi tu?
 
Likizo moja,baada yakutoka farm kusimamia uvunaji mpunga wa mzee,nilienda duka la vipodozi kununua mafuta ya kupaka,ambayo huwa nayatumia.
Nilimkuta jamaa(muuzaji)akiwa na demu wake.
Mimi:Ebwana vipi?mafuta fulani unayo hapa?
Yeye: Duh kaka utayaweza bei yake?
Mimi: Yapo?
Yeye: Ndiyo,ila bei yake sioni kama utaiweza.
Mimi: Ni tsh ngapi?
Yeye: Ni tsh elfu............
(Wakati huo demu anautazama mchezo)
Mimi:Hiyo ndiyo hela kubwa?ambayo siwezi kuilipa?
Nikamwonesha pesa nilizokuwa nazo,around 2m tu+working ID,nikatoa kiasi hitajika nikalipa.
Then,nikamgeukia demu wake.
Mimi:Sister,mambo?
Demu: Poa,za kwako?
Mimi: Poa,huyu ni boyfriend wako?
Demu:Mmh(huku anaona aibu)
Mimi:Mbona umekubali kuwa na boy masikini kiasi hiki?
Hivi anauwezo wa kukuhudumia kweli huyu,ambaye kiasi kdg tu cha pesa ya mafuta anaona ni kikubwa,hadi anadharau watu?
Demu: (Kimya)
Jamaa: (Kijasho chembamba+kupanic)
Baada ya hapo nikasepa.
 
Bora wanaume jamani wengii wana customer care nzuri. hata kwenye restaurants nyingi visichana vidomo juu juu. Mimi sipendi dharau ukiangalia vijicent vyangu vinahusika kwenye kukulipa mshahara
wengi ni kama hawatambui pesa ya mteja ndio chanzo pia cha mshahara wao.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Huyu Bar maid alikua sahihi sana
Kuna bar moja nikwenda. Kufika tu akajipendekeza bar maid mmoja kuja kunihudumia. Basi nikamwambia akaniletee supu ya kuku jikoni na yeye achukue yake. Dakika tano nyingi supu hizi hapa. Huku nnaendelea kusoma gazeti na kunywa supu. Nikamwambia aniletee castle baridi na yeye achukue yake. Dakika nyingi beer ziko mezani. Nikaagiza castle ya pili na yeye nikamwambia achukue yake. Baadae kidogo nikaomba bili nilipe niondoke. Kabla sijawasha gari namuona huyu ananikimbilia na kuniambia. Kaka umesahau kuchukua namba yangu......
 
Back
Top Bottom