Yalinifika!
Ila kilichompata huyo dada, inabidi anikumbuke vizuri kadri atakapofanya kazi ya benki.
Kwa kifupi nilikopa benki, na kutokana na biashara kusua sua dada mmoja kila nikiitwa kujieleza akawa kama ananitukana kimafumbo.
"Ati mnakopa halafu kurudisha fedha hata hujui utarudishaje, tutawafilisi, msikope hovyo" alisema huyo dada.
"Kukopa harusi, kulipa matanga" aliendelea.
Nikajikaza nisijibu neno.
Alahamdulilahi, pesa hiyo ikaingia benki kutokana na biashara zangu, tena siyo vijisenti, bulungutu lililo mara tano ya mkopo!
Nikalipa mkopo mara moja na kuagiza fedha iliyobaki kuhamishia akaunti benki nyingine.
Na nikawaandikia benki kurudisha mara moja dhamana zangu!
Meneja akaniita.
"Vipi tena bro, kwa nini unafunga akaunti tena?"
Nikawaambia tu, muulizeni yule dada wa mikopo.
Huyo dada alikoswakoswa kufukuzwa kazi, ila walimpunguza cheo.