mimi binafsi huwa nina kawaida ya kujishusha sana kupita kiasi.
huwa napenda sana kupima busara za watu mbali mbali na hulka zao,baada ya kumbaini mtu huwa namfundisha hapo hapo,sio kumfokea ni kumuelekeza,dunia ndogo sana hii unawezakuta mtu sio hulka yake,ni kwamba hayuko sawa tu siku hiyo.ukamwongezea shida zaidi.
kuna wakati nilikuwa nafatilia pensheni ya mzee hazina,ilikwama kwa miezi mitatu haikuonekana,akaagizwa alete taarifa zake kisha aziache hapo,sababu anaishi mkoani jukumu la kufatilia likabaki kwangu.
nikapiga route sana hazina kimala-kwa wiki kama mara 3 kama miezi miwili hivi,kila nikienda naambiwa file lako halijapitishwa ofisi hii.
siku moja nikaenda ofisi ile ile nikakuta kuna wadada wa makamo kama wa5 hivi wanafanya kazi huku story kibao,mama wa kila siku ninayemkuta kiti kile hayupo,nikamuulizia nikajibiwa simple tu,sema shida yako yule hayupo kaenda likizo.ok,nikaeleza pale shida yangu dada yule akajibu,wewe sio mhusika inabidi aje mzee wako,dah.
nikamwita kiupole tu,dada ndio maana nilimuulizia yule mama sababu anamjua mpaka mzee wangu,dada kusikia vile akawa kama ameamua kujishughulisha kiasi ili aniridhishe,akanijibu hapa acc ya mzee wako inaonyesha iko domant[emoji1][emoji1].nikamwambia wewe dada wewe,hiyo acc haijamaliza mwezi imewekwa pesa kutoka acc yangu,ndio inapitisha pensheni ya mzee kila baada ya miezi mitatu,domant acc inaingiaje chini ya miezi sita???embu nionyeshe screen,akanikazia tena kwamba screen ni info za mhusika sitakiwi kuona,dah nikahisi shetani anataka anipande ofisi nyeti za uma,nikamtuliza.
nikamuuliza,anyway tatizo linawezakuwa nini?? kwanini file halionekani hapa kwenu na limeshatoka mapokezi kule??akajibu tu sijui.
ikabidi nishuke mapokezi,kule nikakutana na mama mmoja mtu mzima mhaya,ana wito sana na kazi yake,akanisikiliza kwa umakini mno,akanambia nianze kujaza info upya kwa niaba ya mzee,kisha nimpe yeye mkononi,baada ya wiki niende.
wiki ilipofika nikarejea pale,aliponiona tu anakaniagiza niende ofisi ya wale madada ya story.
kufika pale nikamkuta yule mama ambaye awali sikumkuta nikaambiwa ameenda likizo,mama aliponiona tu akaniita jina,na kunambia file limefika kwake,asijue kazi ilianza upya.
nilipomsogelea nikampa mkasa mzima,na kumwambia awaelekeze wale wadada namna nzuri ya kufanya kazi,kuna wazee pale wamechoka na kazi hawahitaji usumbufu wala majibu yenye kero kama wanayotoa.
akanipa hundi nipandishe nayo floor ya juu,nilipokuwa nashuka nikamfata yule dada na kumwabia,ni jinsi gani anapaswa kuwa akiwa eneo lile.si kila anayeenda hapo ni wa kujibiwa vibaya vibaya kivivu,wengine wanaondoka na majina yenu.
akabaki katoa macho tu.