Umeshawahi kupendwa na Mwanamke usiyempenda?

Umeshawahi kupendwa na Mwanamke usiyempenda?

Ilishawahi nitokea , kuna wadada wawili walikua barabarani mmoja ni mkali kinyama ndie nilie mpenda wa pili ni mmasai mmoja mwenye sura yake personal.

Lengo langu niwafuate niombe no ya yule pisi ,ili kutomfanya yule mwingne asijiskie vibaya nikajifanya kuomba no zao wote, mbaya zaidi asiye kwenye lengo ndio akajitia kiherehere cha kunipa no ,yule pisi yeye kimya tu , nikaichukua kishingo upande ,,nikajua kwa sababu ni marafiki naweza pata ukaribu na huyo, ila lengo nisijempoteza yule pisi kupitia mwenzake.

Kufupisha tu ni kwamba yule dada wa kimasai aliniganda hatari zaidi ya mwaka , ili kutomfanya asijisikiie vibaya sikudhubutu kumwambia ukweli , nikawa nawasiliana nae kishingo upande ,alipo kuja kuharibu zaidi alinitambulisha kwa yule pisi kama mimi ni mtu wake, na ile pisi ikawa inaniita shem.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaid pale nilipotambulishwa umasaini ikafika hatua mpka kaka wa binti walipo diriki kutamka watanipa n'gombe 100 .

Kilichonifanya nikaingia mitini kabisa ni pale binti alipo fikia hatua ya kutaka kunitunuku zawadi ya bikra yake na akaniambia hiyo kwao ni zawadi kubwa kabisa ya kimila .

MpKa Leo sikuwahi kukutana na pisi kali kama yule rafiki wabinti wa kimasai , nilikuja kupata fununu karudi kwao Rwanda baada ya kumaliza masomo yao pale KCMC .
Kha! Wengine mnachezea bahati nyieee. Ngombe 100 plus bikra juu umeacha mzeya
 
Ni viherehere vyao mwanamke yake adabu na utii sio kumpenda mwanaume ndo maana ke akitangulia kukupenda mnapoteza msisimko nao
 
Huyu huwa ni kweli anaiona kuwa mimi ni mme ila huwa anaruka na wanaume huko akitendwa ndio anawekeza jitihada kwenye kunisaka.
Nina mke na watoto,mimi ni shaabiki mkubwa na wa uhakika timu iitwayo familia yangu
Mimi ni muumini mkuwa wa dini iitwayo familia yangu.
Mimi ni mwachama muaminifu wa chama kiitwacho familia yangu.
Mimi ni mrahibu niliyeshindikana wa kilevi kiitwacho familia yangu.

NB;
HUYO ALISHAPITA VICHOCHOLO VINGI MNO kumzidi YUDA ESIKALIOTI asije akanipiga bei,ni bora kuwa mbali naye kabisa.

Kataa hela yake marioo
 
Kwenye maisha kuna muda wanaume tunapendwa na wanawake tusio wapenda kwa mfano kwangu mimi niliwaigi kupendwa na mwanamke nisiye mpenda kiasi kwamba hadi aliniomba namba za simu ili tuwe tunawasiliana.

Mwanamke mwenyewe alikuwa mzuri tu, kwahiyo sikumkatalia nilimkubalia kiubishi bishi lakini kutokana na matendo yangu alijua simpendi lakini hakuniacha, ila mbeleni nilimchana ukweli kama simpendi tukaacha but aliumia sana na mimi sikujali nikapotezea, sasa cha ajabu baada ya muda mrefu kupita ni kaanza kumpenda lakini kwa sasa ameshaolewa ila bado ananipenda nasiwezi kumludia kwasababu kaolewa.

Je, na wewe ushawahi kupendwa na mwanamke usiyempenda? Kama umewahi tueleze ilikuwaje na nini uliamua.
una maana hukumtafuna kabisa?
 
Acheni kutesa wenzenu bhn upendo upewe thamani yake endapo kuna mtu atakuonesha huo upendo msijisifie kwa mambo ya kishenzi sisi sote ni wapitaji tu na haya mambo yanapita tu kama kweli wewe ni mjanja basi uishi milele usife umalize hata karne moja na nusu hapo utakuwa ni mjanja sababu wote ulio watesa watakuwa wamekufa ila kama na wewe upo sawa na wao tena huenda utatangulia utawaacha hao unao watesa saizi acheni ujinga wala hao wanao hangaika na nyie sio wapuuzi
Achana naye huyu ni mtoto bado. Anajiona mwamba kwenye ujinga bado hajakuwa
 
Back
Top Bottom