Umeshawahi kupitia situation gani ukasema hii ni habari njema ya kusikitisha?

Umeshawahi kupitia situation gani ukasema hii ni habari njema ya kusikitisha?

kengele maziwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2015
Posts
431
Reaction score
647
Weekend ndio hivyo imeshafika wandugu wa jukwaa hili habari zenu nyote.

kama tittle inavyosema umeshawahi kukutana na situation gani ukasema hii ni HABARI NJEMA YA KUSIKITISHA .

Miaka flani muda kidogo nilishawahi kuwa na mpenzi ambaye akapata mimba japo sikuihitajia kwa kipindi kile.
Lakini changamoto ilianza kwa nongwa ndogondogo zile mara mimba hivi mara vile mara nataka matikiti, mara pepsi nikaanza kuichoka mapema sana.

Kufupisha story siku hiyo alfajiri ananipigia tumbo limemshika na damu zinatoka kwenda hospital akaambiwa mimba imeharibika. Baada ya kupewa taarifa hizo nikasema alhamdulilah. Hizo ni habari njema za KUSIKITISHA vipi wewe ushawahi kukutana nazo changamoto hiyo. Karibu kwa kisa chako.
 
Kuna bro mmoja alipata bahati ya kuwa na mapacha wakufanana wawili, lakini alikuwa na maisha magumu sana pesa ya kula ikawa mtihani kwake na mama watoto na watoto pia, watoto (vichanga) wakaanza kuumwaa sana na pesa hakuna. Bahati mbaya katoto kamoja kalifariki.

Msibani baada kuzika nakumbuka yule bwana alikuwa anaongea na bimkubwa mmoja kwamba anamshukuru sana Mungu kwa huo msiba wa mwanae maana alikuwa anaenda kuchanganyikiwa kwa jinsi majukumu yalivyomzidi msuli. Mimi kama mpenda watoto mapacha sikumuelewa kabisa. Labda ndio HABARI NJEMA YA kusikitisha.


 
Back
Top Bottom