Umeshawahi kupitia situation gani ukasema hii ni habari njema ya kusikitisha?

Umeshawahi kupitia situation gani ukasema hii ni habari njema ya kusikitisha?

Kuna bro mmoja alipata bahati ya kuwa na mapacha wakufanana wawili, lakini alikuwa na maisha magumu sana pesa ya kula ikawa mtihani kwake na mama watoto na watoto pia, watoto (vichanga) wakaanza kuumwaa sana na pesa hakuna. Bahati mbaya katoto kamoja kalifariki.

Msibani baada kuzika nakumbuka yule bwana alikuwa anaongea na bimkubwa mmoja kwamba anamshukuru sana Mungu kwa huo msiba wa mwanae maana alikuwa anaenda kuchanganyikiwa kwa jinsi majukumu yalivyomzidi msuli. Mimi kama mpenda watoto mapacha sikumuelewa kabisa. Labda ndio HABARI NJEMA YA kusikitisha.

Ni kweli kuna matukio unakutana nayo kwa uwezo wako huwezi kuyamudu kwa kipindi hicho Mungu anaingilia kati, hapo ndio unaona ukuu wake.
 
Tuna mtoto wa miezi 8 wife akapata mimba, tulifadhaika kwa kweli ila ilipofika miezi miwili ikaharibika. Ilikuwa ni

HABARI NJEMA YA KUSIKITISHA​

Miaka kadhaa iliyopita nilimpoteza mpwa wangu wa miaka mitatu kwa ajali ya moto, mwili wake uliungua kwa karibia 80%.

Zile siku 3 alizokuwa hospitali nililia sana kwa mateso aliyokuwa anapitia. Maumivu aliyopitia yalikuwa ni makali sana kwa umri aliokuwa nao.

Siku aliyofariki niliumia sana ila baadaye nilishukuru kwa maisha mafupi ya mpwa wangu na kuona ameachana na mateso ya Dunia.
Pole sana Kaka
 
Siku nikisikia Bibi Nyau amepata ajali ya ungo huko mawinguni na ameteketea kabisa hiyo ndiyo itakuwa Habari njema ya kusikitisha kwangu maana ndiyo utakuwa mwisho wa kuwatesa Watanganyika kwa wanga wake.
 
Ulikuta wanachinja mbwa?😄
Jana usiku nilijuta mitaa yote imezubaa nikaishia kulala
Jana mitaa lilikuwa na mixed feelings yaani ile Kariakoo halafu Staz na mengine mengi ndio maana uliona hivyo.
 
Weekend ndio hivyo imeshafika wandugu wa jukwaa hili habari zenu nyote.

kama tittle inavyosema umeshawahi kukutana na situation gani ukasema hii ni HABARI NJEMA YA KUSIKITISHA .

Miaka flani muda kidogo nilishawahi kuwa na mpenzi ambaye akapata mimba japo sikuihitajia kwa kipindi kile.
Lakini changamoto ilianza kwa nongwa ndogondogo zile mara mimba hivi mara vile mara nataka matikiti, mara pepsi nikaanza kuichoka mapema sana.

Kufupisha story siku hiyo alfajiri ananipigia tumbo limemshika na damu zinatoka kwenda hospital akaambiwa mimba imeharibika. Baada ya kupewa taarifa hizo nikasema alhamdulilah. Hizo ni habari njema za KUSIKITISHA vipi wewe ushawahi kukutana nazo changamoto hiyo. Karibu kwa kisa chako.
Wavulana wakianza kubalehe huwa wanawaza ngono sana
 
We jamaaa...eti habari njema za kusikitisha.
 
Honestly umekosea sana ulichoandika.... You could have kept it with you ... Umenisikitisha mnooo
 
Back
Top Bottom