Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Wapi wanatoa imei za samsung
 
Kwa maelezo yako inaonesha manunuzi yako uliyafanya madukani...ningekuwa Mimi kila duka ningechukua mawasiliano yao tena nikitoka kwa nje kidogo napiga picha lango la duka.....tusioijua kariakoo vizuri tuko wengi.
 
watu bwana mnapoteaje kkoo yaani ww unakodi bajaji toka mnazi mmoja mpka gerezani kwa 4000 wa mikoani mnachekesha
 
Nimewahi poteana hapo Kariakoo mtaa wenyewe sio complicated
Lengo langu niende NMB nyuma ya kituo cha polisi msimbazi ,nimepanda costa natokea manzese ,badala ya Costa kupita fire ikakatisha mitaa ambayo siijui nadhan ni kwenye ofisi za mwendo kasi pale ila sikunote nilikuwa nimelala,
Tukaenda shushwa mitaa siko familiar nayo
Nikaona isiwe tabu nikachukua bodaboda nikampa maelekezo anishushe BIG BON
Nikapelekwa ila akili yangu ikagoma kbsa kuwa pale ni big bon ,
Petrol station naiona,na kituo cha polisi nakiona ,Ili viko upande tofauti na vinapotakiwa kuwa(KWA mujibu wa akili yangu)
Yaani mfano akili inaniambia kituo cha polisi kinatakiwa kiwe upande wa kushoto kwako mimi naona kiko Kulia kwangu ,nikadaka wenge
Najua kbsa Nmb wako nyuma ya kituo cha polisi ,ila akili yangu inageuza mazingira
Nikaamua kujiripua kwenda mtaa unaonipeleka huko nyuma ya kituo cha polisi Ndo kama nikawa nimeRESET akili
Vitu vyote vikarudi kama vinavyitakiwa kuwa.
 
Wakati unanunua si pia unaandika kwa kitabu yako ? Basi pale juu andika jina laduka na number zao

Dubai wanakupa busness card
Maana kama unanunua sehemu zaidi ya 9 hata kama ni mzoefu ni rahsi kusahu

Mali bila daftari ....
Hapo ndiyo sahihi. Kila unaponunua andika address, jina na namba ya simu. Itakusaidia kuweka kumbukumbu vizuri.
 

Mkuu kupotea sio ujinga ni kawaida na kulijua jiji pia sio ujanja bali ni mazoea na sehemu hiyo
Wakati mwingine yanatokea mashariki we unaona ni magharibi
 
Dah nakumbuka kabla ya mwendokasi madaladala ya Mbezi tulikua tunapandia hapa msimbazi karibu na sheli ya big bon, kuna siku nimezunguka madukani wee! Kurudi kituo cha daladala nimesahau wala sheli siioni😂 nilizunguka siku ile na kuuliza watu naogopa wasijekua vibaka wakanipora so naitafuta ile sheli siioni kumbe nazidi kuelekea mnazi mmoja huko. Nikaona basi sasa kama ntaibiwa kwa kuuliza basi! Nikamfata machinga mmoja ndiyo akaniambia huku mbali rudi na njia ileee nikafata nikaona big bon hii hapa nilifurahii fasta nikaingia kwa bus😂😂😂

Siku nyingine ndugu yangu katoka mkoani kaja kununua mzigo kariakoo akaniomba nimsindikize yeye ni mgeni, tumeenda tumenunua kurudi tupande bus tena sioni kituo dah alinikejeli eti "nilidhani wewe ni mwenyeji kumbe mshamba tu kama mimi"😂😂 hadi tukaulizia kituo kilipo ndiyo tukaoneshwa.

Siku nyingine naenda kariakoo huku congo, hilo bus linaenda Machinga complex! Tumeshushwa hapo sielewi nimeuliza naambiwa nenda njia ile dah naendaa hata sifiki aah nikachukua boda kumbe nilikua nimevuka congo bila kujua naenda mnazi mmoja hivooo😂
 
Nimeona huu Uzi nikamkumbuka juzi ,ijumaa nilipotea , ni zaidi ya miaka mitano sijaingia kariakoo ndani ndani ,Sasa hiyo juzi ndo nikaenda, kilichonitokea stki ata kukumbuka🤣,

Nilienda asubuhi Kwa dhumuni la kununua kitu ambapo ingechukua Kama 2hrs niwe nimerudi, yaani nilinunua nilichokifata lakini cha ajabu nilorudi jioni baa da ya kupotea njia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila inataka moyo sana kupotea kariakoo
 
Mkuu kupotea sio ujinga ni kawaida na kulijua jiji pia sio ujanja bali ni mazoea na sehemu hiyo
Wakati mwingine yanatokea mashariki we unaona ni magharibi
Mtu unaweza ukapotezwa na akili yako japo ile sehemu unaifahamu,unaweza kupotea coz akili yako inakua ipo mbali sana,ndio maana mtu akitulia,akili nayo hutoa ushirikiano na utakumbuka unapokwenda,

Kupotea ni jambo la kawaida hasa kama mtu ana mawazo,kupotea sometimes hakuhusiani na uenyeji au ugeni.
 
🤣🤣🤣🤣kariakoo Haina mwwnyeji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…