Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Kuna dada alipiga yowe kama wewe na anachagua watu wakuuliza mimi nilivaa suruali ya kitambaa kubwa nimekula mkanda nje ndio akanifuata kuniuliza alizunguka kuanzia saa nne asubuhi Hadi nakutana naye saa kumi
Alinunua kandambili baada ya viatu vya mchuchumio kumchosha kwa kuzunguka
Alikuwa anataka atoke akapande bus za mbagala
Hahahaha
 
Siku moja natoka tegeta na lift ya gari la mshikaji mida ya saa moja usiku,tulipofika k/koo jamaa kanishusha akaelekea zake ferry anaenda kigamboni mm ikabidi nichukue usafiri wa home kule gerezani..nikikumbuka Ile siku kilichotokea nachekaga tu maana jamaa tulipofika k koo aliniamsha Tu oya mwanangu kariakoo hii km vp tomorrow basi..nikashuka!!

usingizi jumlisha usiku sikujua kbs nimeshuka mtaa gani. Akili iliganda km nusu saa najiuliza jamaa kanishusha wapi hapa? Ikanibidi nitembee Tu mm mtoto wa mjini bn siwezi potea k/koo lkn bado akili haisomi kbs ninakoenda ni wapi

Nikasema isije nikatokezea kusikojulikana maana nimetembea kishenzi sifiki gerezani ngoja niulize.Nikamcheki muuza mayai kumuuliza asee naelekea iliko stend ya mwendo Kasi akanijibu sasa huku unakoenda mbona unakaribia kufika mnazi mmoja[emoji1787] ..nikamwambia niitie bodaboda akanijibu labda bajaji.Nikakodi bajaji Kwa buku 4 Hadi gerezani..nikikumbuka najiuliza hivi ilikuwaje nikapotea k/koo siku ile.Sipati jibu
HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA
 
Hii mada inawalenga sana wale wenye mishe misheza manunuzi kariakoo.
Aisee kama huna uzoefu na ile mitaa, hasa ile ya nguo, nakushauri ukinunua mzigo wako ukiona huwezi tembea nayo bora utafute hoteli ulipie uwe unakusanyia mizigo yako hapo...

Mimi sio mgeni wa k.koo hata kidogo, ila juzi ni kama ndio nimefika kwa mara ya kwanza,

Ipo hivi
Nimefanya manunuzi yangu ya nguo za jumla, Ikawa kila ninapochukua mzigo sababu ni mkubwa na bado naendelea basi naufunga namwachia mwenye duka mpaka nitakapo maliza nazungukia kote nabeba,

Pasipo kuelewa jinsi ninavyoiacha ndio nazidi kuchanganya mambo, imefika saa 9 hivi nikawa nishamaliza, ni kuanza ku kusanya sasa,...

Nilikua na location 9..., Nikaanza moja baada ya nyingine, Zikabaki 3, hizi sasa ndio kimbembeee,

Siku za nyuma ilikua kila nikiacha mzigo basi na kalili ule mtaa na duka ili iwe rahisi baadae, Sasa juzi kwa haraka niliyokua nayo na huku nikiamini sijawahi potea na nishakua mzoefu nika ignore hilo swala,

Aloo, Nilizunguka ile mitaaa huku machozi yakinilenga kadiri mda unavyopita,

Duka la kwanza kati ya yale matatu nililipata baada ya 2hrs, kumbuka hizo 2hrs zote nilikua natafuta bila kupumzika,
Na sio kama nililiona mwenywe ila nilikua napita lesi ndio jamaa akaniita akaniuliza "bro vipi bado sana maana ndio tunakaribia kufunga...."?

Nikajifanya "Ahaaa basi poa ngoja tuu nitembee nao" nikachukua mzigo huku moyo ukiruka ruka kwa kushukuru, Yaani pale ndio kabisaa nilikua sipawazi kama nilifanya manunuzi....

Sikutaka hata kuchelewa nikaupeleka guest, inshu ni hayo maduka mawili, Kazi ikaanza tena, hapo mda umeenda, watu washaanza kufunga, kila nikisikia wanashusha yale ma milango yao ya bati, napanick natoka nduki....

Nikatafutaweeeeee, inafika saa 12, nimechoka, nimepanick, nimekata tamaa, Jasho na kiu haviniishii Nishanunua maji kama katoni nzima na henganjifu za kutosha ila vyote kila ninapo simama nikiondoka nimesahau.

Ikafika saa moja, Hapo sasa wengi washafunga, nikawa natembea kinyonge, machozi yananilenga nikiona magrili yanashushwa tuu, nikakaa sehemu ilibakia nukta nipige mayoweee....

Sikua na la kufanya zaidi ya kusubiri kesho yake ambayo ni jana, Akili ilikua ishachoka, nikampigia Rafiki yangu aje tuu anitoe pale nilipokuwepo, maana niliona kabisa mwendokasi ikinivaa, ..

Asubuhi, nikaingia tena, Inafika saa 6, bila bila, hapa nikaanza kupiga hesabu namna ya ku compensate hasara ya kama 900k na usheee(almost 1M kasoro).

Nikakaa tena sehemu, hapa ndipo nikagundua kweli akili ya binadamu kuna mzingira inafanya kazi baadae ukikaa ukijiuliza ni wewe huamini....

Nilianza kuvuta kumbukumbu za kuanzia Mwanzo naingia k.koo ile jana asubuhi, nini nilianza nacho, wapi nilianzia, basi kuanzi hapo mtiririko wa mazingira ya nje ya kuanzia duka la kwanza mpaka la 9 ukanijia,
Hayo ni mazingira ya pale dukani, inshu ni mtaa na njia gani??? Kwa kumbukumbu hivyo hivyo nikaja nikajua ni duka la ngapi na la ngapi katika ule mtiririko ndio nimeyapoteza,

Njia kila nikivuta kumbukumbu haziji, nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi...
Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo....


Mpaka nikakumbukaga kale ka meme, watu wanakatumaga kiutani ila kumbe inaonesha wao yalishakuta..

"Ulishawahi kupotea kariakoo mpaka ukapita sehemu ukawauliza watu, mliniona nikipita hapa?"
Hahaha aisle nimecheka Sana 😀😀Pole Ndugu
 
Hapo k.koo majuzi tu mwezi wa sita nimepotea nilipopaki kigari changu

Ilikuwa hivi nimetoka uelekeo wa fire pale kituo cha mafuta nikaja mpk kwnye mataa ya msikiti pale magari ya muhimbili-Kiwalani yanapoingilia nikaingia kama naenda jangwani vuup mpk mtaa wa nyuma kidogo ya China plaza nikapark pale.
Nilikuwa na shida ya kutengeneza Pc nikamaliza shida zangu fresh njaa ikauma nikaenda kula sehemu flani karibu na Kanisa la KKT lile nadhani.

Sasa nikasema acha niondoke nirudi nyumbani eee bwana eeh tafuta mtaa niliopark gari naona hola. Kila nikienda mtaa huu naona mbona kama nilipita hapa nafuata mtaa mpk barabara ya mwendokasi kule hola narudi tena mtaa wa pili hola.

Nilipoteza kama masaa mawili kila nikienda nakuta gari si yenyewe mpk nikasema nimeibiwa gari mana nilipark hapa na siioni.

Ubaya ni kwamba wakati naingia kuna jamaa alinipigia simu hivyo akili ilikuwa kwenye simu badala ya kukariri sehemu mpk nashuka nilikuwa bado naongea na simu tu.

Mungu si athumani mida ya saa kumi hivi nikapata hiyo sehemu ndio naenda kuikuta gari na dada wa parking anasubiri chake nimpe.
Hapo nimechoka mpk akili majasho kama yote sitaki kukumbuka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji28]
 
Nimewahi potea kkoo ila usiku[emoji23][emoji23]
Day time ni poa maana tumekua kkoo zaidi ya 20 years. Ila hutaamini, kkoo usiku ni sehemu nyingine kabisaa. Yaani nilikikuta nimefika karume[emoji23][emoji23] hapo ndo nilianzia moja. Sehemu napoteaga day time sometimes ni posta kuanzia mnazi mmoja mpaka posta hapa katikati. Yaan na kusoma kwangu posta 4 years haijawa msaada. Yaani napoteza mwelekeo kabisaa[emoji23][emoji23] kuna siku nikasema nitoke mnazi mpk posta vinjia vya kati lwa mguu. Nilikikuta mara 2 narudi mnazi palepale. Niliumiaaaa[emoji119][emoji119] sikutaka tena nikapanda daladala. Halaf nakua nimefika kamtaa ka posta kabisa hivi viroundabout vya ndani huko kama hindu mandal etc. Dar pa kijinga sana
 
nikaona best option ni kwenda kuanzia duka la kwanza kutembea huku nikivuta kumbukumbu, ile ndio ilikua pona yangu, Mzigo wa kwanza nikaupata duka namba 4 mtaa wa Congo na agrrey, mzigo wa pili duka namba 7 Mchikichi na Nyamwezi...
Bahati nzuri ni waaminifu, nikakuta mizigo yangu salama, nikabeba, huyoooo....
Pole sana kiongozi.

Kariakoo inabadilika kwa kasi sana.
 
Njia rahisi sana ya kufanya ni kuchukua contacts zao
Maduka yenyewe 9 hapo ungechukua namba zao kwani lolote laweza tokea na moja wapo ni hili la kusahau mzigo wa thamani umeuacha wapi

Lingine la kufanya ni kujua location kwa google map na kuweka point zako zote
Hii itakusaidia kwa mizunguko yako

Mimi miji yote ninayoenda kama natamani kutembea kwa miguu natumia ramani tu na itanirudisha nilipokuwa hata kama ni Paris
Mi pia natumia Google map, iliniokoa nisipotee pale Italia, Jiji la Genoa
 
Njia rahisi sana ya kufanya ni kuchukua contacts zao
Maduka yenyewe 9 hapo ungechukua namba zao kwani lolote laweza tokea na moja wapo ni hili la kusahau mzigo wa thamani umeuacha wapi

Lingine la kufanya ni kujua location kwa google map na kuweka point zako zote
Hii itakusaidia kwa mizunguko yako

Mimi miji yote ninayoenda kama natamani kutembea kwa miguu natumia ramani tu na itanirudisha nilipokuwa hata kama ni Paris
Huyu jamaa Pantomath anaonekana ni wale watu wa mikoani waliozoea kuendesha taratibu kwa zao kwa njia za kijima. Ununuzi wa bidhaa wa kukariri namna hii ulikuwa unafnyika miaka hiyo wakati hakuna njia nzuri za mawasiliano au kuweka kumbukumbu. Eti unanunua mzigo maduka 9 halafu unang'ang'aniza yote uyakariri kwa kichwa!
 
Nimewahi potea kkoo ila usiku[emoji23][emoji23]
Day time ni poa maana tumekua kkoo zaidi ya 20 years. Ila hutaamini, kkoo usiku ni sehemu nyingine kabisaa. Yaani nilikikuta nimefika karume[emoji23][emoji23] hapo ndo nilianzia moja. Sehemu napoteaga day time sometimes ni posta kuanzia mnazi mmoja mpaka posta hapa katikati. Yaan na kusoma kwangu posta 4 years haijawa msaada. Yaani napoteza mwelekeo kabisaa[emoji23][emoji23] kuna siku nikasema nitoke mnazi mpk posta vinjia vya kati lwa mguu. Nilikikuta mara 2 narudi mnazi palepale. Niliumiaaaa[emoji119][emoji119] sikutaka tena nikapanda daladala. Halaf nakua nimefika kamtaa ka posta kabisa hivi viroundabout vya ndani huko kama hindu mandal etc. Dar pa kijinga sana
Hahahaha
 
Back
Top Bottom