Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Acheni uongo. Hivi mnadhani wote humu hawajaenda shule kama ninyi?Hao wayahudi walishaingia contracts na lucifer mwenyewe. Sasa ufanye uchawi WA kumuibia aliyeleta uchawi[emoji23][emoji23]
Waganga wazushi tu niliibiwa simu ktk mazingira ya kutatanisha simu kala na gharama sn.
Ss mm sio mtu wa ulozi kama mshana jr, akaja mwanangu mmoja na kuniambia anipeleke kwa mganga hiyo simu aliyeiba atarudisha.
Tumefka kwa sangoma baada ya kuelezea shida zetu mixer akasaga majanimajani si jui ni ya aina gani akasema nichemshe ninywe simu itarudi.
Sasa nipo njiani najiuliza simu aibe mwingine mijani ya dawa ninywe mie, halafu kuna uhusiano gani Kati ya kurudi kwa simu na mm kunywa Yale majani
Aahh kudadeki niliitupilia mbali ile mijani na mpaka ss siamini ulozi na hiyo simu nishasamehe[emoji3061]
Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
Liwale bwana waganga wakikupenda wanakusaidia ila kama wakikupenda majini Yao wanakusahaulisha kabisaa usiende kusema ahsantee Ili wakutoe kafara ya damu
🤣🤣Nillifikiri wanatibu magonjwa tu.Kumbe kuna waganga wa kuleta utajiri huku Nchi inanuka umasikini kila kona.
Ni hivi mkuu.Sasa boss mimi huwa najuulizaga mbona sasa watu wengi hawana yale mafanikio makubwa ya kutisha. Au ndo mpaka umwage damu?
Nilienda kwa mganga ni sheikh yupo migo migo kusema ukweli hakunisaidia kupata ajira ndio kwanza mambo yalizidi kuwa meusi.
Ila dawa zake ukichoma na ukioga wanawake unafanya kuwakimbia simu zinaita kutwa nzima na mtaani mpaka unatongozwa. Demu alikupiga kibuti miaka imepita unaona annanzisha convo inbox
Sema ilinikuta sina nguvu nikawa nawapotezea ingekuwa enzi zangu nna mkwanja sijui ingekuwaje.
Migo migo pale sehemu gani
Uzi wa kumpigia upatu mganga kwangu nipate cha udalaliNaomba hapa wale watembea kwa sangoma mtoe shuhuda zenu mliyokutana nayo kwa waganga na toka umeanza kwenda Mganga.
Alikusaidia nini ukaona kabisa shida yako imetatuliwa kwa nguvu ya mganga.
Ikiwezekana mtaje mganga alipo na wengine wakauone uwezo wake
Tutaendelea kuwashuhudia watu weupe wakiishi maisha halisi mpaka mwisho wa Dunia.Nilikuwa nasafirisha mkaa mpaka dar bila vibali!
Nikikaa mbele ya gari trafiki na watu wa maliasili hawaioni gari mpaka Dar.
Kwa nin niliacha....with time mganga aliniambia kwa sasa nadaiwa sadaka ya damu ya mbuzi watatu, nikatoa
Baadae akaniambia nipate mimba niitoe nimpelekee.
NIKACHAPA LAPA ILA NILIZULUMIWA HELA, VIWANJA, GARI nikabaki kama mwanafunzi wa secondary
Namshukuru MUNGU nimeanza upya bila ndumba
Nyongeza: Kwa huyo mganga nilikutana na vigogo kadhaa wa mashirika na idara za serikali na NGO ...wakuu wa vyombo vya usalama.
UNAJUA KWA NIN WATU WANANUNUA VX?
UKIONA mtu ana Vx posta anatoka kazini saa 9:30 anakimbia kwa mganga , anajigangua asubuhi saa tisa ,kumi anaanza Safari kurudi kazini.
Nilishangaa kuona VX kibao zikiingia usiku nikawauliza hawa wote ni watoto wa hiki kijiji, mmebarikiwa...jibu hawa ni mabosi na vigogo wa posta.
Ulichoandika hakiendani na madaTutaendelea kuwashuhudia watu weupe wakiishi maisha halisi mpaka mwisho wa Dunia.
Mtu mweusi linapokuja suala la msimamo ni ngumu saana kudumu. Atayumba tuu katikati.
Unafiki umetawala sana maisha ya mtu mweusi. Hayuko real hata.
Utajiri sio lelemama, upo kwa ajili ya watu makini na majasiri tuu.
Yawezekana ikawa ni kweli ila nimeandika kulingana na mchangiaji alichoeleza hapo.Ulichoandika hakiendani na mada
Inaonekana mganga wako sio masihara. Anachecha mnyanga kweli kweli.Nilikuwa nasafirisha mkaa mpaka dar bila vibali!
Nikikaa mbele ya gari trafiki na watu wa maliasili hawaioni gari mpaka Dar.
Kwa nin niliacha....with time mganga aliniambia kwa sasa nadaiwa sadaka ya damu ya mbuzi watatu, nikatoa
Baadae akaniambia nipate mimba niitoe nimpelekee.
NIKACHAPA LAPA ILA NILIZULUMIWA HELA, VIWANJA, GARI nikabaki kama mwanafunzi wa secondary
Namshukuru MUNGU nimeanza upya bila ndumba
Nyongeza: Kwa huyo mganga nilikutana na vigogo kadhaa wa mashirika na idara za serikali na NGO ...wakuu wa vyombo vya usalama.
UNAJUA KWA NIN WATU WANANUNUA VX?
UKIONA mtu ana Vx posta anatoka kazini saa 9:30 anakimbia kwa mganga , anajigangua asubuhi saa tisa ,kumi anaanza Safari kurudi kazini.
Nilishangaa kuona VX kibao zikiingia usiku nikawauliza hawa wote ni watoto wa hiki kijiji, mmebarikiwa...jibu hawa ni mabosi na vigogo wa posta.
Mganga wako kiboko aiseeAsee nilikua nadaiwa kodi mwenye nyumba kidogo anitolee vyombo nje lakin mpaka leo nadunda tu.
Haji wala hanipigii simu ila mganga kanambia nitafute hela maana hiyo dawa haidumu mi namwambia ikiisha makali nakuja kuongezea
Uchagani ni dawa za miti mkuu dawa za utajiri mvuto nuksi limbwata sijui kama wapo ninchojua ni magonywa Zaidi mkuuNimeamini sehemu watu wanapenda sana dini si sehemu shwari kuishi.....Kilimanjaro watu ni washirikina mno sijapata ona jamani. Zamani nilikuwa naamini kuwa wachagga si wachawi kumbe ni kinyume na hivyo....Kina Harawa jamani ni noma hawa watu.
Mateso niliyopitia na niliombewa mfululizo kila wiki miezi saba ndio nikawa sawa sitaki mtu mwingine yampateInaonekana mganga wako sio masihara. Anachecha mnyanga kweli kweli.
Huwezi tupalocation na sie ambao tuna maradhi ya muda mrefu.
Yumkini uzi huu ukawa nafuu kwetu mkuu
Please tunaomba hii storyKuomba nini sasa? Siendelezi sababu sio jambo la kufurahisha wala kujivunia, hapo kuna sehemu unaona kabisa sikufanya uungwana. Kwa mara yangu ya kwanza naiba, unadhani nilipenda kumuibia mganga Mkuu? Au ni sehemu ya maisha yangu? Hapana nilifanya upuuzi ule ambao umekuja nikost kwa Miaka, nimesema siendelei sababu najutia nilichokifanya na kinaniumiza mpaka leo hii. Sasa ni hivi kama unahisi ilikuwa ni rahisi kiivyo, baada ya boti kuzama kila tulichokuwa nacho kilibaki ndani ya maji. Na hata kuokoka humo ilikuwa ni miujiza tu. Unajua tulikuwa tukienda wapi? Ni safari iliyochukua zaidi ya miaka 3 kufika tulikotaka kufika. Sipendi kuendelea sababu kuna Mengi, ya kufurahisha, kusikitisha, kuchukiza na kuogopesha pia. Destination ilikuwa Canada imagine.
Nakuona my 😜Niliacha kazi nikawa home tu sina mbele wala nyuma, maisha yameninyoosha kisawasawa. Nikawa mshkaji wa kijiweni tu nimenyonda atari, washkaji wananinyanyapaa usiombe.
Kuna jirani chinga kila akipita ananiona nimejiinamia mande to sande. Ikabidi aje tupige story. We si umesoma sana? Nikamwambia kawaida tu. Basi akawa rafiki yangu alinikubali tu na hali yangu. Ananipeleka sehemu tunamwagilia moyo kiroho safi kifupi akawa best.
Ndio siku akafunguka akanipa kontack na bibi Liwale. Nenda kaweke mambo sawa. Kwakua alishakua mshkaji sikutaka kumdissappoint na nauli alinipa. Nikapanga safari huyoo kwa bibi liwalee.
Bibi kafanya yake hakudai hata sumni ila kanichimba beat tu nikifanikiwa nisiporudi imekula kwangu.
Ndani ya wiki tu napigiwa simu niende sehemu nikafanyiwe intavyuu sikumbuki niliomba lini. Kufika intavyua anajigamba kabisaa kua ananijua ila sometimes anajistukia anasema umeletwa na Boss? Kumbe hata boss mwenyewe simjui.
Nikala shavu kimasikhara nikampigia bibi sikusubiri hata kumaliza mwezi nipate salary, nilikopa nikaenda kwa bibi nikampa asante yake nikarudi zangu.
Salary ilivyoingia nikamtafuta rafiki yangu chinga tulikunywa sanaaa siku ile nikajua itakua ni siku ile tu. Kumbe chinga naye kwa furaha akipata mkwanja lazima anicheki tukagambeke.
Maisha yakawa gambe ile deile, mpaka nilivyohama kazi nyingine mbali na rafiki yangu chinga.
Check inboxMimi nina sheikh wangu mmoja hapo Magomeni Mwembe Chai, ni noma kishenzi. Yeye hakopeshi, ukitaka kuua mtu au kumpa mtu laana ya kuokota makopo anakuambia niletee kuku tu au nyama kilo mbili ale na familia yake.....anadedisha mtu bila hata huruma.