Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Hizi shuhuda nyingi humu ni z kutunga na kama mna bisha jaribu kuomba connection yayote ......utaskia hayo mambo nlisha achaga sikunyingi as if sahv amekuwa mtakatifu acheni hizo bwana kama huwezi tupa connection bora utulie tu

Shuhuda ni za ma dalali wa waganga wajinga ndio waliwao.

Acha kuamini watu kwa urahisi. Dunia nyoko hii
 
Nilikuwa nasafirisha mkaa mpaka dar bila vibali!

Nikikaa mbele ya gari trafiki na watu wa maliasili hawaioni gari mpaka Dar.

Kwa nin niliacha....with time mganga aliniambia kwa sasa nadaiwa sadaka ya damu ya mbuzi watatu, nikatoa
Baadae akaniambia nipate mimba niitoe nimpelekee.

NIKACHAPA LAPA ILA NILIZULUMIWA HELA, VIWANJA, GARI nikabaki kama mwanafunzi wa secondary

Namshukuru MUNGU nimeanza upya bila ndumba
Nyongeza: Kwa huyo mganga nilikutana na vigogo kadhaa wa mashirika na idara za serikali na NGO ...wakuu wa vyombo vya usalama.

UNAJUA KWA NIN WATU WANANUNUA VX?

UKIONA mtu ana Vx posta anatoka kazini saa 9:30 anakimbia kwa mganga , anajigangua asubuhi saa tisa ,kumi anaanza Safari kurudi kazini.

Nilishangaa kuona VX kibao zikiingia usiku nikawauliza hawa wote ni watoto wa hiki kijiji, mmebarikiwa...jibu hawa ni mabosi na vigogo wa posta.
Duh!!,Dada umepitia mengi sana,lkn pole kwa yote.Kumbe nikiona mtu anamiliki VX nisimuone gere Maana sijui kaipataje na sijui anapitia,hali gani.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Asee nilikua nadaiwa kodi mwenye nyumba kidogo anitolee vyombo nje lakin mpaka leo nadunda tu.

Haji wala hanipigii simu ila mganga kanambia nitafute hela maana hiyo dawa haidumu mi namwambia ikiisha makali nakuja kuongezea
Huo sasa ni uonezi,kumbuka mwenye nyumba wako ametumia gharama Kujenga nyumba sasa Kwanini umfanyie hivyo?.Lipa kodi ya pango bhana!,sio fair kabisa.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Nikuweke kundi lipi we jamaa?
Vyovyote unavyoona wewe ni sawa. Kwa sababu sikuandika kwa kutaka sifa na wala sijataka kuendelea kwa sababu niliyoyafanya ktk Maisha nayajua mwenyewe na bado naishi, haina Maana ya kukusimulia wewe kila kitu ama nikulazimishe nyuma ya keyboard uniamini, ili iweje? Kuniita Muongo na hujui Hustling za wengine ni Upuuzi..watu wana mavitu ya kishenzi, kibishi, kinyama, kipumbavu, ko akili, ufedhuli na kila aina ya ambayo hujawahi ata kujaribu kufanya, wameyazika na wametulia tuli wanakuchora tu. Watu hubadilika, usichukulie watu kirahisi inaweza kukuponza, labda kama utaishi na wazazi wako tu. Jiongeze
Mpe ukweli

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
sijawai kusikia ana mizimu wala majini
Yeye hutuambia ni dawa za asili alifundishwa akiwa mdogo kusaidia kupata mifungo iliopotea , kuikinga mifugo dhidi ya wanyama wakali
na kujua mtu aliekwenda safari ya mbali kama bado yupo hai ama alishakufa

Dawa hizo pia hutumika kuwaita watoto waliokwenda mjini kutafta maisha na kusahau kurudi kijijn kusalmia wazee ,unambiwa ukifanyiwa hizo dawa utatafta kila njia urudi kwenu hata kwa mkopo ama kutembea kwa mguu

Na kuna ingine alinambia ikitokea hataki mtoto wake aende kutafuta maisha mbali na nyumban anachota unyayo wake anamix dawa na kwenda kuufunika na chungu
kuanzia hapo aliefunikwa hawez hata kufikiria kusafiri wala kwenda kuishi mbali na nyumbani.
Mwana mwambie bibi aturudishie cousin wetu kazamia south mwaka wa 11 huu
 
Ni story kweli ya jamaa yangu wa karibu sana.

Mkewe alianza kuumwa pressure akiwa na ujauzito wa miezi 6.

Wiki nyumbani, wiki hospitali yalikuwa ndiyo maisha yake.

Tulifikia wakati tulishauri daktari atoe mimba mama apone. Daktari alikataa kabisa. BP ilikuwa inapanda hadi 180.

Huwezi amini, alijifungua salama japokuwa mtoto alikuwa njiti.

Cha ajabu, baada ya kujifungua tu, tumbo lilijaa mara mbili ya alipokuwa na mimba. Alivimba miguu kiasi cha kushindwa hata kusimama. Daktari anasema licha ya hali hiyo, hawaoni tatizo lolote katika kupima na hata BP imerudi hadi 110.

Ikawa mshikemshike, hali tete. Si mgonjwa wala watunzaji na daktari mwenyewe tumekata tamaa. Ndipo mmoja wa ndugu akasema nitatenda dhambi mgonjwa apone.

Alikuwa mkristo wa imani ya juu. Wale wa kusali na kulala kanisani. Alikwenda kwa witch doctor. Hakupewa chochote zaidi ya kuambiwa arudi hospitali na kwamba atajua yeye cha kufanya na mgonjwa baada ya saa 3 atasimama.

Alipofika hospitali mgonjwa alishazima. Anasubiriwa tu akate moto.

Baadaye akawa kama ameshtuka fulani, akafungua macho. Akaonekana kurejea uzimani.

Kweli baada ya saa 4 hivi, mgonjwa aliweza kusimama kwa kujitegemea. Akawa mzima tena.

Sote tulimwamini yule witch doctor. Shemeji yetu mzima hadi leo, tena kwa gharama ya sh. 30000/= tu.
Toa location please
 
Kuna dawa alinipa ya ku-deneutralize misala job, kila nikiharibu au ikiitishwa vikao naichoma asubuhi nikienda msala unawaangukia wengine tu wanachambwa vilivyo mm kimyaaa hakuna kima yeyote wa kutaja jina langu au wa kuniassociate na chochote hata kama nilishiriki, nikitoka hapo break ya kwanza bar napiga lite tano fasta huku nikitafakari maajabu ya miti aliyoiumba mnyazi Mungu.
Kaka tupe location please
 
Baada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,

Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,

Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,

Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,

Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,

Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]

Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.

Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,

Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.

Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
Hahajaja hapa ni wapi boss
 
Nakumbuka nilianza kuumwa siwezi kula kulala kusimama hata mkuyenge ukagoma kusimama nikawa nawaza kufa tu kwani nilikuwa sioni faida ya kuishi mwili umegomea Kila kitu nywele zikaanza kupunyuka hovyo hovyo nikampigia simu broo kumueleza ndipo akaniita haraka akanipeleka sehem flani ndipo huyo mganga akasema zingepita siku 4 asingeweza kufanya chocchote kwani nilikuwa kwenye process za mwisho za kuchukuliwa msukule test alonipa ni kusimama juani na hakukua na kivuli changu kiukweli nilishangaa sana ndipo shughuli ya kunirejesha duniani ikaanza hatimae baada ya siku mbili nikaanza kula kulala kutembea Hadi Leo, Kuna wale wenye bahati ya mtende watasema hakuna uchawi au ushirikina wasiombe yawakute Kuna ushenzi mwingi sana hapa duniani
 
Nakumbuka nilianza kuumwa siwezi kula kulala kusimama hata mkuyenge ukagoma kusimama nikawa nawaza kufa tu kwani nilikuwa sioni faida ya kuishi mwili umegomea Kila kitu nywele zikaanza kupunyuka hovyo hovyo nikampigia simu broo kumueleza ndipo akaniita haraka akanipeleka sehem flani ndipo huyo mganga akasema zingepita siku 4 asingeweza kufanya chocchote kwani nilikuwa kwenye process za mwisho za kuchukuliwa msukule test alonipa ni kusimama juani na hakukua na kivuli changu kiukweli nilishangaa sana ndipo shughuli ya kunirejesha duniani ikaanza hatimae baada ya siku mbili nikaanza kula kulala kutembea Hadi Leo, Kuna wale wenye bahati ya mtende watasema hakuna uchawi au ushirikina wasiombe yawakute Kuna ushenzi mwingi sana hapa duniani
Hatarii mkuu.

Kuna watu walikufanyia ubaya??

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom