Umeshawahi kusikia mtu kufa na kufufuka? Nimewahi kushuhudia mtaani kwetu

Medecin

Platinum Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
8,836
Reaction score
24,344
Mtaani kwetu miaka ya nyuma kuna jamaa alikuwa mgonjwa, akapelekwa hospitali na ndugu zake akalazwa, baada ya siku kadhaa akafariki dunia na madaktari wakathibitisha amefariki wakawajuza ndugu zake.

Akapelekwa mochwari then ndugu wakachukua mwili kwa ajili ya maandalizi ya maziko. Akasoshwa na kufanyiwa hatua zote anazofanyiwa maiti, ajabu wakati wanataka kuswalia maiti watu wa karibu na jeneza wakasikia mtu amepiga chafya kama mara tatu na kama mnavyojua muda wa kuswalia maiti kunakuwa na ukimya, ghafla wakaona jeneza linatikisika.

Watu waliopo msibani wakaanza kukimbia huko na huko, masheikh na watu kadhaa ikabidi wachukue jeneza kulirudisha ndani, kufungua wakakuta jamaa macho yamemtoka, wakamtoa na kushauriana kumpeleka tena hospitali.

Kufika hospitali ikawa gumzo ika akalazwa tena na baada ya wiki akaruhusiwa kurudi nyumbani.

Ajabu ni kuwa hata baada ya kupona akawa sio mtu wa kuongea sana, akitaka kitu anaomba basi ila akiulizwa jambo lolote anajibu tofauti na swali, ni kama alichanganyikiwa. Hata watoto wake na mkewe akawa amewasahau hana habari nao. Kubwa kuliko yote ni kuwa wakati kabla hajafa alikuwa ni mkulima tu wa kawaida ila baada ya kufa na kufufuka akawa halimi tena akaanza kuuza pilipili mtaani ndio ikawa shughuli yake kuu.

Ikapita tena kama miaka mitatu hivi akagongwa na gari la kusomba magogo akafariki hapohapo ndio ikawa kifo chake halisi maana kwenye ile ajali hakuomba hata maji.

Nimekumbuka sana hili tukio leo
Nikawa najiuliza lile tukio nilihusishe na sayansi, dini au utamaduni.

Karibuni wanajf na wewe uelezee kama ulishawahi kuona au kusikia tukio mtu kufa kisha kufufuka
 
Sijui kama ni kweli unaweza kufa na kurudi lakini nachojua mpaka mtu afe kabisa na umauti umfike 100% pumzi ya uhai imtoke. Wengine wanakufa kifo nusu wanapata kama Coma, mnaenda kumzika akiwa hajafa kabisa inaitwa Premature Burial.
 
Marehemu akipelekwa mochwari hawekwi kwenye friji siku hiyo hiyo kuna chumba cha reseption ya marehemu anawekwa mezani au chini hadi kesho yake au baada ya masaa kadhaandio anahamishiwa kwenye jokofu mle
 
Tushazika mtaani kwetu mtoto wa darasa la 7 baada ya miaka 4 akakutwa sehemu , kumbe alichukuliwa msukule na Bibi yake. Alipookotwa alilitaja jina la Baba yake tu na Akanyamaza hakusema Chochote tena akapelkewa hospital wodi ya Vichaa maana alikuwa ameota nywele na Meno hana.

Baba yake alimtambua baada ya Kumuona. Wananchi tulizika miaka 4 iliyopita tukabaki tunashangaa tu.

KANDA YA ZIWA HUKO MAMBO NI KAMA HAYO(kabila kuu la kanda hiyo) . NDUGU kuchukuana misukule na Watoto kufariki hasa watoto wa kwanza
 
Kumbe hua hivi🤔
 
Mkuu ngoja Yoda aje atasema ni hadithi tu!
 
Hatari sana
 
Mhm!
 
Na bado sitakubali kuliingiza akilini 😅
Kwa akili ya kawaida tu tukio lenyewe limekaa kitapeli tapeli
Mnganga mmoja hapa Kijijini mweti alitengeneza dili na jamaa mmoja. Huyo jamaa alijifanya amekufa, halafu yule mnganga ni kama alimfanyia tiba, jamaa alafufuka hadi watu tukaanza kumuamini huyo mnganga, yaani hadi watu kutoka nje ya nchi wakawa wanakuja kutibiwa pale.

Baada ya wiki mmoja yule jamaa aliyeigiza kufa alikufa tena, lakini kwa kuwa mnganga mfufua watu alikuwepo wala hatukulia kwani tuliamini kuwa angefufuliwa kwa mara nyingine.

Cha kushangaza mganga akashindwa kumfufua, na tunavyozungumza jamaa yuko ahera 🥲
 
😅😅 asalaleeeeee ati wala ham kumwaga machozi maana mganga mfufua wafu yupo 😁
 
Mimi pia nimewahi kusikia matukio kama haya huko Tabora wilaya jirani na nilipozaliwa, japo sijashuhudia kwa macho yangu, lakini ni mambo ambayo yapo kwenye jamii nyingi za kiafrika na sababu kuu ni imani za kishirikina. Kuna mwaka JK alikiwa Raisi muhula wa kwanza nafikiri alienda huko na zawadi nyingi alizopewa na wananchi zilikuja kugundulika kuwa na ulozi, miezi kadhaa baadae ikapelekwa timu ya wataalamu wa haya maswala kusafisha vijiji kwenye ile wilaya
Nikitulia nitaandika vizuri.
 
Back
Top Bottom