Umeshawahi kusikia mtu kufa na kufufuka? Nimewahi kushuhudia mtaani kwetu

Umeshawahi kusikia mtu kufa na kufufuka? Nimewahi kushuhudia mtaani kwetu

Ukiwa muongo usiwe msahaulifu mara jeneza mara shehe wap na wap
 
Mimi pia nimewahi kusikia matukio kama haya huko Tabora wilaya jirani na nilipozaliwa, japo sijashuhudia kwa macho yangu, lakini ni mambo ambayo yapo kwenye jamii nyingi za kiafrika na sababu kuu ni imani za kishirikina. Kuna mwaka JK alikiwa Raisi muhula wa kwanza nafikiri alienda huko na zawadi nyingi alizopewa na wananchi zilikuja kugundulika kuwa na ulozi, miezi kadhaa baadae ikapelekwa timu ya wataalamu wa haya maswala kusafisha vijiji kwenye ile wilaya
Nikitulia nitaandika vizuri.
Duh watu wana roga hadi Rais
 
Mkuu ngoja Yoda aje atasema ni hadithi tu!
Mimi nimeshuhudia hili maana Alikuwa mtoto tunayemfahamu na Tulimzika Sisi wenyewe. Na alitangazwa Hadi kwenye Gazeti siku anapatikana sema ni muda mrefu sikumbuki ni Gazeti gani lilikuwa kipindi hicho.

Baba yake mtoto alipogundua ni mama yake (bibi wa mtoto) ndie kafanya Vile alitaka kumuua Mama yake tukamzuia.

Mtoto hakudumu sana hapo hospital alifariki tena, serikali ikachukua jukumu la ikazika maana Wananchi tayari walishazika hawawezi zika mara mbili.

Bibi yake baada ya Mjukuu wake kufa kifo cha Pili naye Hakukaa Muda Aliumwa Kichwa kisichosikia Dawa naye Tukazika
 
Mambo yenu ya dini na imani za kipumbavu usiniite , kabisa mimi sipo kwenye level za upumbavu uliopo asee
Tembea Tembea Na Ishi Sehemu ambazo Kabila Kubwa ni Moja. Yaani Usiishi Dar Maana Dar Imeshachanganyika watu wengi

Nenda Sehemu zenye Kabila Moja Hasa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Vijijini Huko Utarudi Mwenyewe Utasema Tofauti na Maneno Yako Hapo
 
Back
Top Bottom