Umeshawahi kuzulumiwa na ndugu kisha ukaona Mungu akitenda maajabu yake?

Umeshawahi kuzulumiwa na ndugu kisha ukaona Mungu akitenda maajabu yake?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Nakumbuka 2018 niliacha kazi ya house boy nikarudi kijijini kulima, wakati huo tayari nilishatanguliza pesa ya kukodi shamba heka 70000 moja na kulima na trecta 45000 kurudia na ng'ombe 2500 mbegu 35000 ukijumlisha na zakutolea na mpokeaji inakuja kwenye 200000.

Sasa muda wa kurudia na n'ombe nikawa tayari nipo kijijini nyumbani ni singida ila nililima manyara kwa kaka yangu, kwasbabu mvua ilishaanza na muda wa kupanda ulishafika kaka akawa ametoa mbegu za maharage tukachanganya na mahindi, sio kwamba nilishindwa kununua mbegu za maharage, hapana kwani nilikuwa na uwezo wa kwenda na baiskeli nyumbani nikachukua halafu kesho yeke nikarudi.

Yeye alilima heka mbili mimi moja, tulipalilia wote kwa pamoja , alikuwa bado hajaoa huyo kaka yangu muda wa kuvuna maharage ulipofika tukaanza na mashamba yake maana yeye alikuwa wa kwanza kupanda tukvuna tu freshi, baadae wakati tunavuna maharage kwenye shamba langu akaniambia.

Unajua dogo hapa hivi mwaka huu ungetoboa mazima ila ndo hivo maana mbegu ya maharage ni ya kwangu.

Mimi nikajibu tu poa haina shida ila nikajua kabisa huyu kaka yangu ameshaingia tamaa, sikumwambia kitu
tukamaliza kuvuna tukapata gunia mbili ndo hivo yakawa mali yake wakati huo gunia moja ni 200000.

Baada ya kuona hivo nikamuomba hata debe moja niuze nipate nauli nirudi mjini wakati nasubiria mahindi yafike muda wa kuvuna, akakataa bahti nzuri bosi alinitumia.

Nilipofika mjini muda wa kuvuna nikamwambia tu anivunie maana nilikosa muda wa kwenda,
akavuna nikamuuliza umepata gunia ngapi? akaniambia amepata 6 tu wakati ukweli ni kwamba pale ningekosa sana ningepata gunia 9 kwa jinsi mahindi yalivyo enda vizuri.

Baadae kuna mtoto wa mama mkubwa nilimuuliza maana walisaidiana kuvuna, akaniambia kwamba mahindi yote ya mashamba matatu yaani heka zake mbili na yangu moja wakati wanavuna walichanganya pamoja
nikasema poa maana gunia moja wakati huo ilikuwa ni 60000 nikasema nisiuze nisubiri bei ipande
muda huo kaka yangu alikuwa anafunga ndoa mwezi wa 8 kabla ya mwezi wa nane nikamwambia auze kwa bei iliyopo anitumie hela ninunue laptop.

Akaniambia alisafiri kwenda nyumbani baada ya kurudi akakuta magunia yote mpaka yakwake yameliwa na mchwa, nikapotezea na kumwachia mungu, ila tu ukweli ni kwamba kuna kipindi baada ya pigo la mungu alikimbilia mererani pesa ya kula nilimtumia saana tu pesa ya kutoka mererani kuja arusha mjini nilimtumia mimi na pesa ya kutoka arusha mjini mpaka singida kijijini nilimpa mimi, cha ajabu hakujifunza nimempa simu ampelekee mama yeye akampa mke wake.

Naamini mungu atakuwa anambadilishia pigo japo mimi nisha msamehe.
 
nakumbuka 2018 niliacha kazi ya house boy nikarudi kijijini kulima,
wakati huo tayari nilishatanguliza pesa ya kukodi shamba heka 70000 moja na kulima na trecta 45000 kurudia na ng'ombe 2500 mbegu 35000 ukijumlisha na zakutolea na mpokeaji inakuja kwenye 200000

sasa muda wa kurudia na n'ombe nikawa tayari nipo kijijini nyumbani ni singida ila nililima manyara kwa kaka yangu, kwasbabu mvua ilishaanza na muda wa kupanda ulishafika kaka akawa ametoa mbegu za maharage tukachanganya na mahindi, sio kwamba nilishindwa kununua mbegu za maharage, hapana kwani nilikuwa na uwezo wa kwenda na baiskeli nyumbani nikachukua halafu kesho yeke nikarudi

yeye alilima heka mbili mimi moja, tulipalilia wote kwa pamoja , alikuwa bado hajaoa huyo kaka yangu muda wa kuvuna maharage ulipofika tukaanza na mashamba yake maana yeye alikuwa wa kwanza kupanda tukvuna tu freshi, baadae wakati tunavuna maharage kwenye shamba langu akaniambia,

unajua dogo hapa hivi mwaka huu ungetoboa mazima ila ndo hivo maana mbegu ya maharage ni ya kwangu

mimi nikajibu tu poa haina shida ila nikajua kabisa huyu kaka yangu ameshaingia tamaa, sikumwambia kitu
tukamaliza kuvuna tukapata gunia mbili ndo hivo yakawa mali yake wakati huo gunia moja ni 200000

baada ya kuona hivo nikamuomba hata debe moja niuze nipate nauli nirudi mjini wakati nasubiria mahindi yafike muda wa kuvuna, akakataa bahti nzuri bosi alinitumia
nilipofika mjini muda wa kuvuna nikamwambia tu anivunie maana nilikosa muda wa kwenda,
akavuna nikamuuliza umepata gunia ngapi? akaniambia amepata 6 tu wakati ukweli ni kwamba pale ningekosa sana ningepata gunia 9 kwa jinsi mahindi yalivyo enda vizuri,

baadae kuna mtoto wa mama mkubwa nilimuuliza maana walisaidiana kuvuna, akaniambia kwamba mahindi yote ya mashamba matatu yaani heka zake mbili na yangu moja wakati wanavuna walichanganya pamoja
nikasema poa maana gunia moja wakati huo ilikuwa ni 60000 nikasema nisiuze nisubiri bei ipande
muda huo kaka yangu alikuwa anafunga ndoa mwezi wa 8 kabla ya mwezi wa nane nikamwambia auze kwa bei iliyopo anitumie hela ninunue laptop,

akaniambia alisafiri kwenda nyumbani baada ya kurudi akakuta magunia yote mpaka yakwake yameliwa na mchwa, nikapotezea na kumwachia mungu,

ila tu ukweli ni kwamba kuna kipindi baada ya pigo la mungu alikimbilia mererani pesa ya kula nilimtumia saana tu pesa ya kutoka mererani kuja arusha mjini nilimtumia mimi na pesa ya kutoka arusha mjini mpaka singida kijijini nilimpa mimi, cha ajabu hakujifunza nimempa simu ampelekee mama yeye akampa mke wake

naamini mungu atakuwa anambadilishia pigo japo mimi nisha msamehe
Ni MUNGU sio mungu.
 
Ndugu sio lazima mzaliwe pamoja hata yule mnayekutana kwa upendo tu ni ndugu pia. Kuwa makini na kaka yako hakujali na wala hakupendi anasubiri use ale rambirambi...
 
Hi ndo mioyo ya wale watakao shinda vita hongela sna kwa kuwa na moyo usiotaka makuu

Kwa kua umemuelewa basi jiepushe kufanya naye shughuri yeyote au kumuamini kivyovyote
Bali msaidie tu panapo hitajika.
 
hafai kuitwa ndugu kaanae mbali
Hachelewi kufanya jambo lolote baya juu yako endapo utapata maendeleo zaidi yake
Anaonekana ni mtu wa tamaa asiyependa maendeleo ya wengine
Na ameshajua wew ni mtu wa namna gan atakusumbua so kaa pembeni
 
Nakumbuka 2018 niliacha kazi ya house boy nikarudi kijijini kulima, wakati huo tayari nilishatanguliza pesa ya kukodi shamba heka 70000 moja na kulima na trecta 45000 kurudia na ng'ombe 2500 mbegu 35000 ukijumlisha na zakutolea na mpokeaji inakuja kwenye 200000.

Sasa muda wa kurudia na n'ombe nikawa tayari nipo kijijini nyumbani ni singida ila nililima manyara kwa kaka yangu, kwasbabu mvua ilishaanza na muda wa kupanda ulishafika kaka akawa ametoa mbegu za maharage tukachanganya na mahindi, sio kwamba nilishindwa kununua mbegu za maharage, hapana kwani nilikuwa na uwezo wa kwenda na baiskeli nyumbani nikachukua halafu kesho yeke nikarudi.

Yeye alilima heka mbili mimi moja, tulipalilia wote kwa pamoja , alikuwa bado hajaoa huyo kaka yangu muda wa kuvuna maharage ulipofika tukaanza na mashamba yake maana yeye alikuwa wa kwanza kupanda tukvuna tu freshi, baadae wakati tunavuna maharage kwenye shamba langu akaniambia.

Unajua dogo hapa hivi mwaka huu ungetoboa mazima ila ndo hivo maana mbegu ya maharage ni ya kwangu.

Mimi nikajibu tu poa haina shida ila nikajua kabisa huyu kaka yangu ameshaingia tamaa, sikumwambia kitu
tukamaliza kuvuna tukapata gunia mbili ndo hivo yakawa mali yake wakati huo gunia moja ni 200000.

Baada ya kuona hivo nikamuomba hata debe moja niuze nipate nauli nirudi mjini wakati nasubiria mahindi yafike muda wa kuvuna, akakataa bahti nzuri bosi alinitumia.

Nilipofika mjini muda wa kuvuna nikamwambia tu anivunie maana nilikosa muda wa kwenda,
akavuna nikamuuliza umepata gunia ngapi? akaniambia amepata 6 tu wakati ukweli ni kwamba pale ningekosa sana ningepata gunia 9 kwa jinsi mahindi yalivyo enda vizuri.

Baadae kuna mtoto wa mama mkubwa nilimuuliza maana walisaidiana kuvuna, akaniambia kwamba mahindi yote ya mashamba matatu yaani heka zake mbili na yangu moja wakati wanavuna walichanganya pamoja
nikasema poa maana gunia moja wakati huo ilikuwa ni 60000 nikasema nisiuze nisubiri bei ipande
muda huo kaka yangu alikuwa anafunga ndoa mwezi wa 8 kabla ya mwezi wa nane nikamwambia auze kwa bei iliyopo anitumie hela ninunue laptop.

Akaniambia alisafiri kwenda nyumbani baada ya kurudi akakuta magunia yote mpaka yakwake yameliwa na mchwa, nikapotezea na kumwachia mungu, ila tu ukweli ni kwamba kuna kipindi baada ya pigo la mungu alikimbilia mererani pesa ya kula nilimtumia saana tu pesa ya kutoka mererani kuja arusha mjini nilimtumia mimi na pesa ya kutoka arusha mjini mpaka singida kijijini nilimpa mimi, cha ajabu hakujifunza nimempa simu ampelekee mama yeye akampa mke wake.

Naamini mungu atakuwa anambadilishia pigo japo mimi nisha msamehe.
KWAMBA ANAMBADILISHIA PIGO!!!!!!!!!! 😀 Kwenye familia zetu za Kiafrika ( hata za wazungu kidogo)wapo wengi sana mwisho wa siku wanakuwa LIABILITY.
 
Write your reply...omba mungu siku akienda kwa mganga..lazima atakutoa kafara
 
Legye kelele,uliacha kazi ya house boy, lakini bahati bosi akakutumia nauli urudi mjini halafu kaka akutumie hela za mavuno ununue laptop dah u houseboy wako safi sana.Ila maharage yalikuwa halali yake sema alikuwa na roho ngumu kukunyima hata kidogo ya kupata nauli.
 
Back
Top Bottom