Umeshawahi kuzulumiwa na ndugu kisha ukaona Mungu akitenda maajabu yake?

Dili na watu kulingana na tabia zao wanazokuonyesha kwa kujirudia rudia. Ukiona anakuonyesha tabia za kutaka kukudhuru usipoteze muda kulalamika.

Mkalie mbali, usijihusishe nae punguza mazoea. Inasaidia sana kupunguza majeraha, lawama, na kukosa.

Kuna watu umezaliwa nao tumbo moja au ukoo m'moja ila inapokuja kukudhuru wao hawawazi mara mbili na wanaweza kukufanyia kitu mbaya muda wowote alikuomba msamaha ni ile tu kukuzuga ila ndani ya nafsi anakuwa anakuchora tu uingie kumi na nane nyingine akubutue.
 
Oktoba 2020 tulidhulumiwa na ndugu yetu mbabe lakini march 2021 Mungu akatenda maajab yake
 
kuna jamaa anaitwa Ajay n mwalimu sitamsahau maisha yangu yote alinidhulumu m1.5 klhali ye ana mshahara wakati huo ni mwanafunzi Mi nafunga na kusali tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…