Pung'o boy
JF-Expert Member
- Aug 1, 2013
- 685
- 305
Mi nimesoma boys school ambayo ilikua inaogopeka moshi nzima kutokana na historia yake ya vurugu. Kwaio tulikua hatuna disco wala match za mpira kila shule tukiialika ilikua inaogopa kuja kwaio sisi ilikua ni misuli kwa kwenda mbele. Ila kituko msichana akipita maeneo ya skuli atapigiwa shangwe had anapoteza mwelekeo haijalishi umri wake ilimradi awe ana shepu nzuri ama sura nzuri.yani hiyo hata kama tukiwa parade mbele ya master au ticha yoyote shangwe lazima lipigwe. Afu tena tulipokua form 5. Vyoo vilikua vichache so full kupanga foleni hadi chooni. Kingine tulikua hatuendi parade ya asubui had walimu waje watufukuze mabwenini. Tuliwahi leta mgomo walipotaka watufanyie inspection nakumbuka tulimuweka master juani toka asubui had sa kumi na 1 jioni afu sisi tupo kivulini tukimpiga maswali ya hapa na pale. Mambo ya msosi yalikua poa 4 meals per day. Wali 4 times pa week. Tea na mikate 3 times pa week matunda nini kama kawa.tukimis wali wanatupikia jioni.kuoga ndo lilikua janga la kitaifa kwa pale skuli mtu kukaa wiki bila kuoga ilikua kawaida sana kuna rafiki tulivoripot form 5 alikaa siku 21 bla ya kuoga me nshawai kukaa siku 12 bila kuoga ratiba yangu ilikua ijumaa had ijumaa ila inachange nikinyuka(wet dream) lazima nioge na siku zingine hiyo ijumaa kuna kua na mvua na ukungu mbele hauoni na shower hazitoi maji so siogi hio ni kwa kipind cha winter na kwa wiki mara mbili hadi 3 kwa summer coz kulikua kuna baridi ya hatari sabuni ya kuogea 1 unaweza tumia miez miwili na isiishe watu tulikua tunasubiri shower zitoe maji ndo tuoge maji yalikua yanatoka kuanzia saa kumi jioni yanafungwa sa 4 ucku yanatoka tena saa 11 alfajir ad sa 4 asubuh mana zilikua zinatumia maji ya kisima yanayovutwa na pump za umeme kuna kipindi pump ilipga shoti shower zilikua hazitoi maji kwa miezi kama mi3 hivi watu hapo ndo tulivunja rekodi za kuto kuoga mana kulikua kuna maji ya idara ya maji ambayo yalikua yanatoka direct from mount kilimanjaro yani hayo yalikua hayaogeki mana niyabaridi 24/365 afu sasa inabidi uchukue ndoo uchote ukayaoge yani kuyanywa tu hadi meno hua yanakufa ganzi so kuoga hadi ujifikirie mara mbili mbili Maisha ya boarding bhana.... #team umbwe boys mti safi